FRANCIS DA DON
JF-Expert Member
- Sep 4, 2013
- 40,941
- 47,028
Nasikia kuna lawama juu ya kuongezeka kwa kasi kwa deni la taifa, naomba kuuliza, mwisho wa kuhimilika kwa deni la Tanzania ni trilioni ngapi?
Kama ni trilioni 50, au 60, au 70 au pengine hata trillion 100, basi tukope haraka haraka kwa kasi zaidi hadi pale deni litakapokuwa halihimiliki ili waache kutukopesha.
Tukishakuwa hatukopesheki basi tatizo la kukua kwa deni litaisha maana hakuna atakaetukopesha tena, hapo sasa ndio tutaona kitu kinaitwa 'Austerity measures' kama zile zilizoikumba Greece.
Yaani mtu aliyekuwa anafanya kazi BoT na ana mshahara mzuri wa kuishi kama mfalme anaanza kuokota makopo ili auze apate 200/= ya kunywea chapati, na katika hili hakuna utani, wote tulishuhudia kilichowapata wagiriki pale walipoacha kukopesheka.
Tujiandae hicho kipindi cha msoto wa kutokopesheka kinakuja, maana hata wenye majumba ya kupangisha yatabaki matupu maana watu hawana hata pesa za kupanga nyumba, hakuna atakaepona. Labda wakulima wa mazao ya vyakula na wafugaji.