Je ni kweli wanawake hawapendani?

mhalisi

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
1,181
318
Kuna msemo wa kiswahili unaosema "wanawake hawapendani", je ni kweli wadau? Kama kweli wanawake hawapendani, ni sababu ipi inafanya wasipendane?
 

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,390
8,150
Hawapendani pale mmoja anapokuwa na kitu na akaonyesha uwezo wake wakipesa basi tambua hapo anakuwa ametengeneza maadui wengi utakuta wanachukiana pasipo kuwepo na sababu.
 

Raimundo

JF-Expert Member
May 23, 2009
13,419
12,548
Tukumbushane hii!!

Mwanaume alilala nje usiku kucha na alipoulizwa na mke wake akamwambia nililala kwa rafiki yangu, mama wa watu alipopiga simu kwa marafiki wa mumewe anaowajua wote wakakubali tena wa kumi akajibu akisema bado yuko hapa anajiandaa kuja nyumbani. Ukawa ugomvi na ukaisha.

Sasa ilipotokea mke akalala nje na akajitetea kwamba alilala kwa rafiki yake, mume naye akapiga simu kwa rafiki wa mkewe hakuna hata mmoja aliyekubali kati ya wote kumi aliojaribu kuwapigia.

Hapo utaona wanawake wasivyopendana.
 

arabianfalcon

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
2,291
583
Sio kweli tuna pendana,ila mapenzi yana haribika pale utakapo nitilia kitumbua changu mchanga hapo mapenzi hakuna....
 

Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
3,896
1,698
Nakumbuka nilipokuwa form five, kulikuwa na wasichana wawili marafiki sana wakati tunaanza A-level, urafiki wao uliendelea mpaka muhula wa kwanza ulipoisha, muhula wa pili nakumbuka upepo wa urafiki wao ulibadilika sana tena sana, no mawasiliano wala nini ni kuchuniana tu, sasa kuna mmoja hadi tunamaliza six alikuwa tayari alibadilisha marafiki wanne tofauti kwa vipindi tofauti na mwingine alibadilisha marafiki watatu kama sikosei. Hapo ndo niligundua kuhusu tabia za hawa viumbe juu ya urafiki!! Mweee!!
 

BPM

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,761
572
hawapendani wanawake kwani wanapimana kwa ubira wao akiona kazidiwa basi anajenga chuki
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom