Je, ni kweli tuna watalii wachache sababu hatuna ndege zetu wenyewe?


M

Massenberg

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
1,173
Likes
1,089
Points
280
M

Massenberg

JF-Expert Member
Joined Jun 4, 2011
1,173 1,089 280
Bwana yule anauaminisha umma wa Watanzania kuwa ndege zikija zitaongeza watalii na anatoa mfano wa Morocco.

Kuweka rekodi sawa ni kwamba Morocco haipati watalii wengi sababu ya shirika lao la ndege, la hasha, Morocco wana vivutio vichache ila wanajua kuvisimamia na kuvitangaza Ulaya na America ya Kaskazini ambako ndiko wanakolenga watalii wao.

Asilimia kubwa sana ya watalii wanaokwenda Morocco hutoka Ulaya na wanatumia budget airlines za Ulaya ambazo ni nyingi kama utitiri.

Shirika la ndege linaweza kusaidia lakini haliwezi kunadiwa kama kivutio kitakacholeta watalii.

Hatujaweza kukuza wigo wa vivutio vyetu na pia hatujui kutangaza biashara ya utalii. Ukiona mabanda ya maonyesho ya utalii ya Tanzania huko duniani ni vioja, hakuna kabisa creative thinking.

Lazima kuwepo na sababu za kumvutia mtu aje Tanzania lakini shirika la ndege siyo mojawapo ya sababu hizi.

Watanzania wasichotwe akili kwa bei nafuu namna hii.

Morocco kuna beach nyingi za kuvutia pamoja na hotel packages nzuri, sisi tangu Tanga mpaka Mtwara hakuna beach yoyote ya maana tunashindwa hata na Zanzibar.

Ndege haziwezi kubadilisha hii hali, tunahitaji akili mpya na za kisasa siyo za mtu kama Maghembe.
 

Forum statistics

Threads 1,273,867
Members 490,535
Posts 30,494,018