SI KWELI Sheikh Yahya Hussein alitabiri baada ya Rais Mwanamke kumaliza Mihula yake Upinzani utaongoza nchi

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Kwanza Kabisa nawatakieni ninyi nyote Sabato yenye Baraka.

Nimesoma mahali kwamba Mtabiri wa taifa enzi za Nyerere Shehe Yahya Hussein alitabiri Uongozi ujao kuanzia awamu ya 4 hadi ya 6 Watatawala CCM lakini awamu ya 7 atachaguliwa Kiongozi wa Upinzani Kuongoza nchi

Kwamba mwisho wa CCM. Je, ni Kweli?

sheikh-yahyabc.jpg
 
Tunachokijua
Sheikh Yahya ambaye wakati wa uhai wake alipata umaarufu mkubwa kutokana na kutabiri matukio makubwa katika maeneo mbalimbali duniani, alizaliwa wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, mashariki mwa Tanzania mwaka 1932.

Sheikh Yahya anakumbukwa kwa kutabiri mambo mengi ikiwemo matokeo ya mpira wa miguu, kutokea kwa majanga na vifo vya viongozi na watu maarufu duniani.

Hata hoja inayosambaa kwa kasi kwa siku kadhaa mtandaoni kama alivyohoji mdau johnthebaptist aliitoa Mwaka 2006 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa Habari kueleze Mambo kadhaa yaliyokuwa yanajiri wakati wa Utawala wa Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.

gpm26i4waaannal-jpg.3010197

Picha yenye Maneno yanayodaiwa kutamkwa na Sheikh Yahya Hussein
Pamoja na mambo mengine, Sheikh Yahya anadaiwa kutamka kuwa baada ya vipindi viwili vya Rais Kikwete atakuja rais ambaye ni mweusi mchapa kazi lakini mchekeshaji sana, hata hivyo atatawala kwa kipindi kifupi tu hapo ndipo Tanzania itapata rais mwanamke.”

Aidha, sehemu nyingine ya hoja hii inasema kuwa Sheikh Yahya aliendelea mbele kwa kusema Upinzani utatawala baada ya Rais mwanamke.

Ukweli upoje?
JamiiCheck imefuatilia madai haya na kubaini baadhi yana ukweli na mengine hayana ukweli.

Siku ya tukio hilo, aliyekuwa Mhariri wa Gazeti la Uwazi Elvan Stambuli alikuwepo na alishiriki kuuliza maswali.

Katika makala yake yaliyochapishwa na tovuti ya Global Publishers, Machi 20, 2021, Stambuli alimuuliza Sheikh Yahya kama Tanzania inaweza kupata Rais mwanamke baada ya kuisha kwa kipindi cha Kikwete ambapo alijibu “Baada ya vipindi viwili vya Rais Kikwete atakuja rais ambaye ni mweusi mchapa kazi lakini mchekeshaji sana, hata hivyo atatawala kwa kipindi kifupi tu hapo ndipo Tanzania itapata Rais mwanamke.”

Stambuli anafafanua zaidi kuwa Wahariri na waandishi waliokuwepo kwenye mkutano huo waliguna kuonesha kutokubaliana naye wakiwemo wahariri wakongwe Hemedi Kimwaga, Yasini Sadiki, Magnus Mahenge na wengine ambao hawezi kuwakumbuka.

Aidha, Shehe Yahya baada ya kuona wanambishia alichukua ubao kama ule wa darasani na mkononi alishika kutabu kilichoandikwa Astrology: Monthly numerology, akaanza kufanya hesabu kwa fomula anazojua yeye na akawambia kwamba kwa Jakaya inaonesha atamaliza muda wake wa miaka kumi na lakini ajaye ataongoza kwa kipindi kifupi. Hata hivyo, hakusema sababu itakayopelekea kutokea kwa hali hii.

Mazungumzo na Elvan Stambuli
JamiiCheck imefanya jitihada za kumtafuta Elvan Stambuli, ambaye pamoja na mambo mengine amethibitisha kuwepo kwenye kwenye mkutano huo na kuwa alikuwa miongoni mwa watu waliouliza maswali.

Katika majibu yake, amesema yeye binafsi alikuwa na urafiki wa karibu na Sheikh Yahya na alikuja kukumbuka utabiri huu baada ya kifo cha Hayati Magufuli.

"Walipoondoka (kwenye mkutano huo) mimi nikabaki naye sababu alikuwa rafiki yangu yule mzee (Sheikh Yahya), nikamhoji mambo mengi sana lakini akaniambia unajua utabiri sisi ni kama unaoteshwa halafu asubuhi unafanya hesabu zako unataja. Sasa litokee au lisitokee mimi utabiri nimeshautoa. Kwahiyo ilivyotokea baadaye kweli akaja huyu bwana akafa, hakumaliza, tukakumbusha heee kumbe lile jambo ni kweli" amesema Stambuli

Kuhusu madai ya upinzani kuchua nchi, Stambuli amesema "Ni porojo tu za watu, wanataka tu credit labda, upinzani hakuongelea kabisa"

Mnajimu maarufu wa Afrika Mashariki, Sheikh Yahya Hussein alifariki dunia nyumbani kwake jijini Dar es Salaam Mei 20, 2011 kutokana na maradhi ya moyo.
Hata mimi nmeona hayo.maandsh, kwan mam c anaupga had 2035😃 c ndio tumekubaliana hvyo

Na hilo mkalitazamee
 
mijizi CCM haing'oki mpaka kinuke.

Na kwa kizazi hiki cha sasa chenye masalia ya Nyerere hakiwezi kukinukisha.
 
Ni kweli, Shekh Yahaya Hussein nimeanza kumfuatilia tangu miaka ya sabini akiandika utabiri wake wa wiki kwenye magazeti ya uhuru na mzalendo. Kabla ya kifo chake alitabiri Rais mwanamke na upinzani kuingia Ikulu.
Tusubiri utabiri wake wa upinzani kushika Dola kama utatimia mwaka kesho. 😆
 
Ni kweli, Shekh Yahaya Hussein nimeanza kumfuatilia tangu miaka ya sabini akiandika utabiri wake wa wiki kwenye magazeti ya uhuru na mzalendo. Kabla ya kifo chake alitabiri Rais mwanamke na upinzani kuingia Ikulu.
Tusubiri utabiri wake wa upinzani kushika Dola kama utatimia mwaka kesho. 😆
Nadhani Tundu Lisu kauchungulia Utabiri 😂😂😂
 
2025 ni zamu ya upinzani kushika nchi,wamchukue Josephat Gwajima kama mgombea alafu waone kama nchi haijabebwa asubuhi na mapema.Lisu akae pembeni kidogo!
SH anachukiwa sana mitaani,watu wanataka mabadiliko ata kesho!!
 
ACT Wazalendo inakwenda kuchukua dola mwaka 2025, tanzania itakuwa na rais anayeitwa ZITTO KABWE Na zanzibar itakuwa na rais anayeitwa OTHMAN MASOUD OTHMAN. Umefika wakati sasa watanzania tufanye maamuzi ya kweli, kwa mustakabali mwema wa taifa letu na wananchi kwa ujumla !
 
ACT Wazalendo inakwenda kuchukua dola mwaka 2025, tanzania itakuwa na rais anayeitwa ZITTO KABWE Na zanzibar itakuwa na rais anayeitwa OTHMAN MASOUD OTHMAN. Umefika wakati sasa watanzania tufanye maamuzi ya kweli, kwa mustakabali mwema wa taifa letu na wananchi kwa ujumla !
Act katika ubora wao.
 
Ni kweli, Shekh Yahaya Hussein nimeanza kumfuatilia tangu miaka ya sabini akiandika utabiri wake wa wiki kwenye magazeti ya uhuru na mzalendo. Kabla ya kifo chake alitabiri Rais mwanamke na upinzani kuingia Ikulu.
Tusubiri utabiri wake wa upinzani kushika Dola kama utatimia mwaka kesho. 😆
Lete ushahidi
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom