Je ni kweli Pamba Jiji yatimua viongozi wake?

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,679
2,232
Hatimaye, timu ya Pamba Jiji ya Mwanza imefanikiwa kurejea tena Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Mbuni FC katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi ya NBC Championship katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Kwa ushindi huo unaifanya Pamba FC imalize Ligi ya NBC Championship na pointi 67, nyuma ya mabingwa, Ken Gold ya Mbeya iliyomaliza na pointi 70 na wote wanapanda Ligi Kuu moja kwa moja.
1716184953246.png
Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry.
Mabingwa wa zamani wa soka wa Tanzania, Pamba Jiji ya Mwanza wamefanikiwa kurejea ligi kuu ya nchi hiyo baada ya miaka 22 ya kucheza madaraja ya chini. Mara ya mwisho kucheza ligi kuu ilikuwa mwaka 2001 iliposhuka daraja. Kupanda daraja kwa Pamba kumerejesha kicheko kwa mashabiki wa kandanda wa Mwanza, Jiji la sato na Sangara. Kabla ya Pamba kushuka daraja, iliwahi kuwa bingwa wa ligi kuu ya Muungano ya mwaka 1990, huku ikitoa changamoto kwa timu za Simba, Kikwajuni, Yanga, Malindi, Coastal Union, pamoja na Mlandege.

Niliwahi kupiga stori na Mzaramo Mbwiga Mbwiguke na kunipa taarifa kuwa Pamba ilianzishwa mwaka 1968, huku kumbukumbu yake kubwa ikiwa ni kucheza na Anse-Aux- Pins mwaka 1990 na kuicharaza magoli 17 kwa 1 katika raundi ya awali ya lililokuwa Kombe la Washindi Afrika, mchezo wa kwanza Pamba akishinda magoli 5 kwa sifuri akiwa ugenini na kisha kushinda magoli 12 kwa 1 akiwa Jijini Mwanza huku Fumo Felician akipiga goli 8 peke yake.

Pamba iliyoanzishwa mwaka 1968, iliwahi kupata matokeo ya kukumbukwa sana miongoni mwa wapenzi wa soka ilipoinyuka timu ya Anse-Aux- Pins kutoka mji wa kibiashara Anse Boileau kusini mwa Shelisheli jumla ya magoli 17-1 mwaka 1990, katika raundi ya awali ya lililokuwa Kombe la Washindi Afrika. Pamba ilishinda 5-0 ugenini katika katika mchezo wa kwanza na 12-1 nyumbani Mwanza huku mshambuliaji wake Fumo Felician akipachika magoli 8 katika mchezo huo wa marudiano.
1716185184010.png
Picha kwa hisani ya MAMBO UWANJANI.
Sasa miaka 22 imetosha kurejea ligi kuu, je Pamba Jiji itavimudu vishindo vya ligi kuu ya sasa ambayo ina mabadiliko makubwa kuliko ile ya miaka ya 1990 na kurejesha ushindani wa enzi zile? Hilo ni jambo la kungojea na kuona. Ingawa wiki ilioisha kumekuwa na taarifa za chini chini ndani ya Viunga vya Mwanza kuwa gari limewaka huku Uongozi wa Klabu hii ukifanya kuwaondoa viongozi katika safu yake ya uongozi wakiwa wanaelekea kwenye maandalizi ya msimu wa 2024-2025. Viongozi hawa waliotemwa wakiwa ni wale ambao sio watumishi wa Halmashauri ya Jiji huku kiongozi pekee aliyesalia akiwa ni Mheshimiwa Evarist Hagila. Wale wote waliopambania timu ipande tokea msimu ulipita kwa sasa wameachwa kwenye mataa na viongozi ambao wana uhusiano na Halmashauri ndo waingia kazini.
1716184953246.png
Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry.
Swali langu hivi kuna ulazima wa kuwaondoka viongozi ambao hawana uhusiano na Halmashauri ya Jiji? Ama ndo timu imepanda Ligi Kuu ndo imekuwa timu ya Jiji, ila ikiteremka inarudi mikononi mwa wanamwanza tena? Ila tuongeeni ukweli Pamba Jiji msimu wa 2024-2025 anateremka kama alivyopanda! Chap kwa sana! Mzee wangu, Mheshimiwa Said Mohamed Mtanda una kazi kubwa sana kuifanya Pamba Jiji ilete ushindani Ligi Kuu ya NBC.​
 
Hatimaye, timu ya Pamba Jiji ya Mwanza imefanikiwa kurejea tena Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wenyeji, Mbuni FC katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi ya NBC Championship katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Kwa ushindi huo unaifanya Pamba FC imalize Ligi ya NBC Championship na pointi 67, nyuma ya mabingwa, Ken Gold ya Mbeya iliyomaliza na pointi 70 na wote wanapanda Ligi Kuu moja kwa moja.
View attachment 2994763
Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry.
Mabingwa wa zamani wa soka wa Tanzania, Pamba Jiji ya Mwanza wamefanikiwa kurejea ligi kuu ya nchi hiyo baada ya miaka 22 ya kucheza madaraja ya chini. Mara ya mwisho kucheza ligi kuu ilikuwa mwaka 2001 iliposhuka daraja. Kupanda daraja kwa Pamba kumerejesha kicheko kwa mashabiki wa kandanda wa Mwanza, Jiji la sato na Sangara. Kabla ya Pamba kushuka daraja, iliwahi kuwa bingwa wa ligi kuu ya Muungano ya mwaka 1990, huku ikitoa changamoto kwa timu za Simba, Kikwajuni, Yanga, Malindi, Coastal Union, pamoja na Mlandege.

Niliwahi kupiga stori na Mzaramo Mbwiga Mbwiguke na kunipa taarifa kuwa Pamba ilianzishwa mwaka 1968, huku kumbukumbu yake kubwa ikiwa ni kucheza na Anse-Aux- Pins mwaka 1990 na kuicharaza magoli 17 kwa 1 katika raundi ya awali ya lililokuwa Kombe la Washindi Afrika, mchezo wa kwanza Pamba akishinda magoli 5 kwa sifuri akiwa ugenini na kisha kushinda magoli 12 kwa 1 akiwa Jijini Mwanza huku Fumo Felician akipiga goli 8 peke yake.

Pamba iliyoanzishwa mwaka 1968, iliwahi kupata matokeo ya kukumbukwa sana miongoni mwa wapenzi wa soka ilipoinyuka timu ya Anse-Aux- Pins kutoka mji wa kibiashara Anse Boileau kusini mwa Shelisheli jumla ya magoli 17-1 mwaka 1990, katika raundi ya awali ya lililokuwa Kombe la Washindi Afrika. Pamba ilishinda 5-0 ugenini katika katika mchezo wa kwanza na 12-1 nyumbani Mwanza huku mshambuliaji wake Fumo Felician akipachika magoli 8 katika mchezo huo wa marudiano.
View attachment 2994773
Picha kwa hisani ya MAMBO UWANJANI.
Sasa miaka 22 imetosha kurejea ligi kuu, je Pamba Jiji itavimudu vishindo vya ligi kuu ya sasa ambayo ina mabadiliko makubwa kuliko ile ya miaka ya 1990 na kurejesha ushindani wa enzi zile? Hilo ni jambo la kungojea na kuona. Ingawa wiki ilioisha kumekuwa na taarifa za chini chini ndani ya Viunga vya Mwanza kuwa gari limewaka huku Uongozi wa Klabu hii ukifanya kuwaondoa viongozi katika safu yake ya uongozi wakiwa wanaelekea kwenye maandalizi ya msimu wa 2024-2025. Viongozi hawa waliotemwa wakiwa ni wale ambao sio watumishi wa Halmashauri ya Jiji huku kiongozi pekee aliyesalia akiwa ni Mheshimiwa Evarist Hagila. Wale wote waliopambania timu ipande tokea msimu ulipita kwa sasa wameachwa kwenye mataa na viongozi ambao wana uhusiano na Halmashauri ndo waingia kazini.
View attachment 2994763
Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry.
Swali langu hivi kuna ulazima wa kuwaondoka viongozi ambao hawana uhusiano na Halmashauri ya Jiji? Ama ndo timu imepanda Ligi Kuu ndo imekuwa timu ya Jiji, ila ikiteremka inarudi mikononi mwa wanamwanza tena? Ila tuongeeni ukweli Pamba Jiji msimu wa 2024-2025 anateremka kama alivyopanda! Chap kwa sana! Mzee wangu, Mheshimiwa Said Mohamed Mtanda una kazi kubwa sana kuifanya Pamba Jiji ilete ushindani Ligi Kuu ya NBC.​
Pale siasa inapotaka kuvuruga mpira...ikiwa hizi taarifa ni za kweli basi Pamba haina mda mrefu itashuka tena bila ubishi.
 
Siasa na Mpira huwa havichangamani kabsa
Pale sasa inapotaka kuvuruga mpira...ikiwa hizi taarifa ni za kweli basi Pamba haina mda mrefu itashuka tena bila ubishi.
Kuna watu wasio wa mpira wameingia kwa kigezo cha uzalendo wa Pamba Jiji
 
Siasa na Mpira huwa havichangamani kabsa

Kuna watu wasio wa mpira wameingia kwa kigezo cha uzalendo wa Pamba Jiji
Kwel kabsa mkuu hili jambo sio rafiki kabsa katika mpira wetu ...wanataka kuwaweka watu wasio hata Na uchungu kwenye timu
 
Hata wachezaji ni muda wa kuwapa 'thenki yuu' watupishe tusajili upya.
 
Hizo ni juhudi za Amos Makala, ueye ndiye aliyeitoa mavumbini pamba ns kuikabidhi mikononi mwa manispaa.

Ulikuwa ndio mpango wake, unadhani wangetoa wapi pesa ya kuendesha timu? Ndio sababu mwanza hakuna timu ya mpira . Hivyo hivyo kwa arusha
 
Back
Top Bottom