Umenikumbusha jirani yetu kulikuwa wanandoa fulani, wana Watoto wao wawili wa kike.
Miaka kadhaa baadae Mzee akapoteza kazi yake tena ya maana tu baada ya kampuni ya Wazungu kufunga shughuli zake nchini...na bahati mbaya elimu ya yule Mzee haikuwa na soko sana kibongobongo, hivyo alisota kwelikweli.
Mama alikuwa kigogo wa serikali ya mkoa, kwa hiyo alikuwa na uwezo mkubwa tu.
Siku zilienda Mother akawa ana mnyanyapaa Mzee wazi wazi, mpaka Watoto waliweza kunotice...akigombeza Watoto anamchanganya na Mdingi, yaani ilikuwa kama mpo around mna watch video (enzi zile) mnasikia noma.
Sijui yaliyokuwa yanaendelea ndani ila kulikuwa na kila dalili kuwa kila mmoja alikuwa analala chumba chake.
Baadae yule Dingi alipata kwa kujishikiza akasepa zake, na Mother alikuwa na uwezo mkubwa tu, karibu kila kitu alikuwa anahudumiwa na serikali, sio kodi ya nyumba, usafiri n.k.