Je ni kweli MUZIKI unaelimisha jamii ?

Je ni kweli MUZIKI unaelimisha jamii ?

Kisai

JF-Expert Member
Joined
Apr 6, 2018
Posts
29,126
Reaction score
29,352
Kuzua mambo kumekuwa tabia sugu na ya kale kwetu sisi binadamu,kuzua kunapelekea kusingiziana na matokeo yake huzaa chuki na maangamivu.

Kusingiziwa au kusingiziana hakuishii tu kwetu sisi binadamu bali mpaka kwa wale au kwa visivyokuwa sisi. Muziki ni miongoni mwa vitu vilivyosingiziwa hasa katika kazi zake.

Kwangu mimi muziki ni pumbazo na hauna faida yoyote kwa binadamu.

Huwa tuna ambiwa na kukaririwa ya kuwa miongoni mwa kazi za muziki ni kuelimisha jamii. Swali la msingi je ni vipi muziki huelimisha jamii ? Huku ukiwa muziki umepewa majukumu au jukumu usio liweza tuna ambiwa yule msanii ni kioo cha jamii.

Sasa huwa najiuliza,Je ni kweli muziki unaelimisha jamii au umesingiziwa na kama kweli ubaelimisha ni kivipi ? Wenye kujua ni vipi muziki huelimisha jamii,uwanja wao huu watupe faida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siamini kama dhamira yako ni kupingana na ukweli juu ya dhima ya tasnia ya muziki katika jamii hasa hususani katika Elimu, bali unataka mdahalo jamvini Wa jambo ambalo linaeleweka sana.
 
Mziki wa sikuhizi sio ule wa kuelimisha bali umekuwa wa kuwafanya watu wawe walevi na mashoga tu. Hayo maoni yangu tu kila binaadamu na maoni yake

Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Miziki ya 1960s 70s 80s and 90s ilielimisha sana sana na ilikua na ujumbe lakini Bongo flava ni hovyo hakuna kitu
 
Muziki wowote una ujumbe ndani yake. Sasa huo ujumbe kama unakuelimisha au kukupotosha, hapo ndio utaona faida au hasara ya huo muziki husika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siamini kama dhamira yako ni kupingana na ukweli juu ya dhima ya tasnia ya muziki katika jamii hasa hususani katika Elimu, bali unataka mdahalo jamvini Wa jambo ambalo linaeleweka sana.
Linaeleweka sana kivipi ? Kwamba unaelimisha jamii au kinyume chake ? Maana mimi nimeshaonyesha msimamo wangu hapo ya kuwa muziki hauna uwezo wa kuelimisha jamii wala haukuwahi kuelimisha jamii. Sasa nachotaka kujua au kuona ni ule upande wa pili,ule upande ambao watu hudai muziki unaelimisha jamii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miziki ya 1960s 70s 80s and 90s ilielimisha sana sana na ilikua na ujumbe lakini Bongo flava ni hovyo hakuna kitu
Kwako ni masharti gani au vigezo gani hufanya kitu kiwe na sifa ya kuelimisha jamii,yaani jambo liwe na sifa ya kuelimisha jamii ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tafuta miziki ya Mbaraka Mwinshehe uwata jazz,sikinde hasa (barua kutoka kwamama) marijani rajab ( ndoa ya mateso,rufaa ya kifo,ukeeenza ni mateso) less wanyika :sikujua kama utabadilika,amigo,pesa inaua tena maua nk .
Kumbuka paulo na sila waliimba gerezani.............. Hiyo ni bibilia .aisee acha tu mziki ni maisha
 
Back
Top Bottom