Je ni kweli kuwa Waziri wa mazingira Theresa Huvisa aliondolewa kwa mafisadi kumshinikiza kikwete?

Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
14,211
13,725
Sio siri kuwa aliyekuwa waziri wa mazingira Theresa Huvisa alikuwa mwiba sana kwa wale wote waliokuwa wamejenga nyumba zao ufukweni kwa kuvunja sheria; alisimamia sheria na kusababibisha nyumba nyingi za matajiri kubomolewa kule ufukweni na hivyo kuchukiwa sana na hao waliohusika wakiwemo wabunge wenzie!!!

Mbunge mmoja wa chama tawala amejenga hekalu lake huko Mbezi beach kinyume na sheria na pale sheria ilipotaka kuchukua mkondo wake akakimbilia mahakamani kuweka stop order iliyoinusulu nyumba yake isivunjwe mpaka hivi sasa!! Toka huyu mama kuondolewa kwenye madaraka, kasi ya kujenga ufukweni kinyume na sheria imerudi tena na cha kushangaza zaidi ni kuona kuwa hapo karibu ya nyumba ya huyo mbunge aliyejenga huko Mbezi beach kinyume na sheria fisadi mwingine anajenga hekalu lake kwa kasi ya ajabu ingawa mamlaka husika zimemuwekea notisi kuwa asiendelee kujenga!! Je serikali itakaa kimya mpaka amalize kujenga hilo hekalu lake ndio ilibomowe? Je,kasi hii ya ujenzi holela huko Mbezi beach baada ya yule mama kuondolewa ni ushahidi kuwa mafisadi wameiweka serikali mifukoni kwa sababu ya hela zao?
 
.....Waache wafu wawazike wafu wenzao. Walio hai hawahusiki katika suala hili.

Walio hai wanahusika na suala hili kwani hawa mafisadi wanakata mikoko ambayo ndio mazalia ya samaki ili kujenga mahekalu yao!!! Kama samaki hawana mahala pa kuzaliana watoto wetu watapata wapi kitoweo sisi tukishakwenda mbele ya haki?
 
Si umtajae tu huyo mbunge mwanamke wa chama tawala anaitwa Mch. Dr. Mhe. Gertrude Rwakatale!
 
Walio hai wanahusika na suala hili kwani hawa mafisadi wanakata mikoko ambayo ndio mazalia ya samaki ili kujenga mahekalu yao!!! Kama samaki hawana mahala pa kuzaliana watoto wetu watapata wapi kitoweo sisi tukishakwenda mbele ya haki?
Upo sahihi mkuu ila nilikuwa namahanisha katika huo mtifuano wao wa kufukuzana sisi wengine hatuhusuki. Hata hivyo sitarajii kama kuna mtu mwenye akili timamu ndani ya CCM anayeweza kuwaza hayo unayoyawaza wewe juu ya vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom