Je ni kweli kuwa wanaume(SINGLES) hawana imani na wanawake wanaojishugulisha?

futikamba

JF-Expert Member
Jan 18, 2010
243
13
Habari MMU,
Kwa muda mrefu sana, nimekuwa nikisoma mada za hapa MMU ili kujipatia mauozefu.

Ila leo, na mimi napenda nilianzishe ili tulijadili wote.
Nimefanya kautafiti kadogo na kugundua kwamba baadhi ya wanaume ambao bado hawajaoa wanakuwa hawana imani sana na wapenzi wao wenye juhudi katika kujishughulisha.
Unakuta kijana ana mpenzi wake, mathalan anafanya kazi na pia anamilikia biashara. Unaweza ku-imagine ni jinsi gani mtu huyu anakuwa busy at times.
Lakini, mpenzi huyu wa kiume anakuwa hajiamini amini. Ukimwambia mpenzi leo nikitoka job kuna masoko naenda kuyafuatilia, yeye kwa sababu ya kutojiamini kwake au kutokukuamini analeta kauzibe ya subiri nikupeleke, na mwishowe hatokei na ishu inabuma.
Au mawasiliano ya simu na wateja yanakuwa frequent kutokana na biashara mpenzi wake anayofanya. Basi ukipokea simu hata hujamaliza kuongea unaanza kumsikia "huyo nani, mwambie hivi na hivi, usiongee hivo, n.k n.k"
Pengine una contacts na watu unaowajua kabla hujakutana nae. Awe mfanyakazi mwenzako, uliyesoma nae au mfanya biashara mwenzako. Ukimpigia simu au sms, maswali kibao.
Je, ni kwanini wanaume hasa walio single hawana imani na wapenzi wao wanaojishughulisha.
Tujadili.....
Nawakilisha

FK
 
Inaonekana kama wewe ni mdada.....

Well ushauri wangu...tafuta a more matured guy
 
Sijui kwanini utafiti wako umeonesha ni single men tu ndio wenye tatizo hili? Sample ipi ulitumia?

Kwa observation zangu ni mostly married ndio si tu hawaamini but also hawawaruhusu wake zao kujishughulisha! Mimi nafikiri single men wana kaunafuu kuliko wengine!
 
Wewe ni mdadaau mkaka? Na ilishawahi kutokea?

Mi naona hapa swala la gender halihusiani sana. Ningependa tulijadili swala hili kama lilivo ili pande zote mbili zijifunze.

Asante,
FK
 
Sijui kwanini utafiti wako umeonesha ni single men tu ndio wenye tatizo hili? Sample ipi ulitumia?

Kwa observation zangu ni mostly married ndio si tu hawaamini but also hawawaruhusu wake zao kujishughulisha! Mimi nafikiri single men wana kaunafuu kuliko wengine!

Mkuu Kaunga,
Hata singles wapo hivo. Ni baadhi, si wote... ila nashangaa kwanini wawe hivo!?

FK
 
Yaa, uko sahihi kabisa! Ni kweli hali kama hiyo huwa ipo, lakini huchangiwa sana na namna ambayo mdada amekutwa nayo wakati wanaanza ku-date. Unajua ikoje? Mara nyingi huwa watu wana-win mioyo ya wapenzi wao wakiwa tayari wako na wapenzi, hivyo a bit more competiotion huwa ni chance kwa mapenzi mapya kushamiri na mtu akampiga chini aliye naye kwa wakati huo. Trust huwa ina-build up pale tu wahusika wote wawili wanapoachana kabisa na wapenzi wao wa zamani. Sasa iwapo kuna namna yoyote ya mawasiliano iwe ya kibiashara au la, kati ya mdada na mpenzi wake wa zamani, unadhani jamaa atamfikiriaje?
 
ok!
Tukianzia hapo, huyo ambae yupo above 30, kwanini awe hivo? Nini hasa kinachokuwa kinam-drive kuwa wa namna hiyo? Wivu au?

sio kila above 30 ni mature
wengine still bado watoto

halafu hujajibu
are you female?
 
Yaa, uko sahihi kabisa! Ni kweli hali kama hiyo huwa ipo, lakini huchangiwa sana na namna ambayo mdada amekutwa nayo wakati wanaanza ku-date. Unajua ikoje? Mara nyingi huwa watu wana-win mioyo ya wapenzi wao wakiwa tayari wako na wapenzi, hivyo a bit more competiotion huwa ni chance kwa mapenzi mapya kushamiri na mtu akampiga chini aliye naye kwa wakati huo. Trust huwa ina-build up pale tu wahusika wote wawili wanapoachana kabisa na wapenzi wao wa zamani. Sasa iwapo kuna namna yoyote ya mawasiliano iwe ya kibiashara au la, kati ya mdada na mpenzi wake wa zamani, unadhani jamaa atamfikiriaje?

Chris, Na je kama hakuna mawasiliano kama hayo? Je ni nini kinamfanya mtu awe over-protective?
 
Ni kwa sababu wako single...."wanakuwa katika protective mode"

Mmmmmh! too much protection can ruin everything... alafu inakuwaje hapo?
Unakuta jamaa mwenyewe hawezia hata kukusaidia vitu vidogo vidogo kama kuchangia rent ya nyumba n.k. Inakuwaje akubane kupambana iwapo yeye mwenyewe hawezi kutoa msaada?
 
it does....matter a lot
since hii mada una complain about men....
Ungekuwa mwanaume ingekuwa rahisi kuelewa some of the
answers here

Naelewa sana.... the thread is still going on. We changia tu kwa faida ya gender zote mbili.
 
Back
Top Bottom