Je? Ni kweli kuhusu tarehe 21/5/2011..???? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je? Ni kweli kuhusu tarehe 21/5/2011..????

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sizinga, May 18, 2011.

 1. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #1
  May 18, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Mi sijui bwana!! Labda nianze kwa kusema hivyo. Je ni kweli siku ya tarehe 21/5/2011 tusubirie hukumu ya Muumba apendae vitu vyake vyote alivyovifanya na kuviumba, Mungu mwenye neema tele, alete maafa katika hii dunia? Niseme tena mi sijui. Kwa kujikumbusha tu nimeona ngoja niilete hii mada hapa JF ili tuwe macho siku hii na tuone nguvu za hawa watabiri wetu tulio nao ni za kweli au ndio kujitafutia umaarufu tu.
  Nitakachokiongea/kuandika katika hii sredi ni 'just fiction', sina lengo la kumuogofya mtu(scary) or whatever, nikama mada nyingine tu. Najua hapa JF na kwingineko kuna Bilevers na Non-bilivers, Muslims, Christian, Hindus, Bhudhist and more, kila mtu na lwake!! Haya tuanze sasa...!!

  Kuna 'rumours' kibao zinaendelea mtandaoni na katika media kuhusu 21/5/2011. Wengi wanasema hii siku ni 'Judgement day' au kwa lugha nyingine ni 'Doomsday' ikiwa na maana kwamba siku ya maafa makubwa(Time when we expect something terrible or unpleasant) kwa hiyo tutegemee smthng differnt on this day. Swali langu kubwa ni je,endapo hivi vitu havitatokea, hawa watu watakuja na majibu mengine kuhusu hii siku??
  Sasa hawa watu prophets and preachers are trying to tell us the End of the World is on the 21st of October 2011, na kabla ya hii siku basi kuna judgemnt day, na wamefikia kusema hizi si kwa kukurupuka bali ni kwa kufuatilia kwa karibu sana matukio yanayoendelea duniani na maandiko matakatifu(Bible na Quran) wakajaribu kurelate na mwishoni wakaja na conclusions, ambazo ni nataka wanaJF tuzijue na kuchambua ikibidi. Sababu zao za msingi ni kama ifuatavyo:

  Ujio wa Barrack Obama-'The coming of Anti-Christ'.
  Ma-prophecy wanasema kwamba Barrack Obama Rais wa marekani ni antichrist-mpinga kristo, na sababu zao kubwa ni kwamba:
  -Mpinga kristo atatokea katika familia ya politics and he will come as a man of peace. Na ndiyo hii Obama anapigana nayo kila kukicha ili ahakikishe amani inakuwepo ulimwenguni ni kila kona ya dunia na akiweza hii ina maana kwamba mataifa yote yatakuja kumsujudia. He will make himself the most powerful man on earth.
  Tumeona na tunaendelea kuona mapigano huko Libya kwa Gaddaf, Afghanstan,Pakistan,Ilani na sehemu nyinginezo . Kikubwa zaidi huyu mtu anajaribu kwa ukaribu zaidi kuwapatanisha Waisrael na Palestina, and He will try to destroy the Jewish People and Israel. Mtu atakayefanikiwa hii kuleta amani kwenye mataifa haya 2 ni antiChrist, kwani katika biblia haya mataifa tangu waingie kwenye nchi ya ahadi yamekuwa sumu iliyowekwa na Kuumba mwenyewe.

  -Sera za Obama kipindi anagombea urais zilihusisha sana mambo ambayo kristo aliyakemea kwa asilimia 100, lakini ujio wa Obama, umepromote vitu vyote ambavyo Imani ya wakristo,waislam inasimamia. Mfano alipitisha sharia za Ndoa za Jinsia moja, aliruhusu kisheria Ushoga, aliruhusu kisheria utoaji mimba-ili tu kuwe na regular and countable population, matumizi ya condoms..nk. Na hivi ndio sera zake kubwa zilizompatia ushindi. Na hii amediriki kuisimamia kiukamilifu, na kikubwa zaidi hata kama kanisa katoliki linapinga hivi vitu, dunia imepata kushangaa!!Obama alivyoenda Roma kuonana na Pop Benedikt, huyu Pop hajaongea na wala hajaonyesha msimamo wake kwenye masuala haya,till today,Pop is silent.

  -Obama anadai ni mkristo. Lakini kiukweli huyu jamaa hana dini 'maalum'. But actually he practised Islamic religion as well, na hata alipotembelea India alienda kwenye Temples kuabudu.

  -The winning lottery number-ile namba yake ya ushindi katika jimbo la Illinois ilikuwa ni 666 ambayo ni alama ya Beast.

  -Antichrist will be the king of South as predicted in the bible(Daniel 11). Hapa tunaona kwamba Kenya ipo South of jerusalem, ambako Obama ana asili ya huko.

  Sababu ya pili ni Rupture.
  Hapa kuna vitu vingi vinaingia. Hii inaweza kuwa ngumu kidogo kueleweka. Infact watabiri wanasema kwamba mwaka 2011 ni mwaka wa 7000th from the flood of Noah's day. It will be the end of the length of time given to mankind to find grace in God’s sight(hapa kuna maelezo marefu sana ambayo siwezi kuyaandika kwa sasa).
  Mapigano ya vita and rumours of war, na hapa wanajaribu kuongea kwamba kifo cha Osama bin laden kinaweza kibua mapigano makubwa duniani.
  Njaa, matukio ya mitetemeko ya ardhi-earthquakes. This is the God’s signs to the sinners that Doomsday is on the 21st of May, or rather, so they say.

  Kama nilivyosema hapo juu, hatujui kipi ni kipi, na kila mtu na imani yake..na ndio maana hata hapa kwetu kumeibuka ''vikombe'' vingi sana kwa magonjwa sugu ambayo wanasayansi wengi duniani wamejaribu na wameshindwa kupata ufumbuzi wa dawa,lakini hapa bongo kuna watu kibao washaraise-kinara wao Babu Ambilike wa Samunge na wengine kufuata, hii inaweza ikawa ishara flani ya matukio ya Doomsday.

  So nimeandika hii mada zikibakia siku 3 kufikia tarehe 21, tusubirie hapahapa JF na tuone what will happen on that day kama watabiri wanavyodai,wakihusisha matukio kama ya Japan na haiti ni mwanzo tu wa siku hiyo.

  Nakaribisha michango ya wengine.
  Love u all....Usiku mwema!!:A S-rose::A S-:focus:rose::focus::welcome::welcome::amen::wave:
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  May 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Dini mbili zenye asili ya Abrahamic zinaamini kuwa moja wapo ya ishara ya mwisho wa dunia ni kuja kwa Nabii Yesu/Issa/Yeheshua.

  Je Ashakuja, au atakuja siku moja kabla ya hiyo 21 ambayo ni siku ya Jumamosi?

  Je uoni kuwa ni kumzilia uongo bwana Yesu, pale aliposema kuwa hakuna mtu yeyote anayejuwa siku hiyo isipokuwa M'Mungu peke yake, maana hata yeye mwenye pamoja na malaika wote duniani hakuna ajuae siku wala saa, ila zimewekwa dalili tu.
   
 3. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #3
  May 18, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  labda uwe mwisho wa gadafi ila si ulimwengu!
   
 4. f

  fizzmann New Member

  #4
  May 18, 2011
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hamna ukweli wowote kwamba 21 may 2011 ndio mwisho wa duniam. Hizo ni rumours!
   
 5. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #5
  May 18, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Labda wa Loliondo!
   
 6. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #6
  May 18, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,479
  Likes Received: 12,758
  Trophy Points: 280
  !!!!!!!!!!!!!!!!!! itavyokuwa na iwe ila kifo cha wengi ni harusi
   
 7. LOOOK

  LOOOK JF-Expert Member

  #7
  May 18, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,392
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Kuna habari hizi na hata pia nina makala yahusu huo mwisho,,, huo hapo udownload na uusome ulikuwepo kwa lugha zooote ila nlichagua wa kiswahili ila lazima computer yako iwe na adobe reader
   
 8. Kalunguine

  Kalunguine JF-Expert Member

  #8
  May 19, 2011
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 2,544
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  asiyeijua biblia anaweza daganyika na hizo sababu za hapo juu. katika ndoto za daniel tunaona jinsi pembe ndogo inavyoibuka na kuitawala dunia, hiyo pembe ndogo ndiyo marekani, bado kuna mengi hayajafikiwa, maybe in 200years ndio dalili zote za mwisho wa dunia zitajuwa zimefika.
   
 9. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #9
  May 19, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
 10. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #10
  May 19, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wizi mtupu!
   
 11. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #11
  May 19, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  labda uwe mwisho wa magamba
   
 12. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #12
  May 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,791
  Trophy Points: 280
  afrodenz huogopi?
   
 13. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #13
  May 19, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,923
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Subirini muone hizo sababu watakazokuja nazo tar 22.
  kuna mwingine alitoa siku saba kwa watu fulani, hii ni siku ya 14, lakini yupo kimya.
  nafikiri hata hawa jamaa itabidi wakae kimya.
   
Loading...