Danken Mbombo
JF-Expert Member
- May 30, 2015
- 651
- 339
Kumekuwa na tetesi za muda mrefu eti dawa ya kuhifadhia maiti inatumika kuhifadhia samaki tunaokula. Tetesi hizo zinachagizwa na ukweli kwamba siku hizi samaki hawana radha tulioizoea.
Mfano samaki sato na sangara wanaoletwa Dar wamepoteza ladha. Awali samaki hao walikuwa wanasafirishwa kwa ndege toka Mwanza kuja Dar bila kutiwa dawa hivyo walikuwa na ladha yao ile ile.
Lakini siku hizi sato na sangara wanasafirishwa toka Mwanza kwa malori huwekewa dawa ya kuhifadhia maiti ili wasiharibike.
Matokeo yake siku hizi samaki hao hawana utamu wowote kama walivyokuwa zamani. Vivyo hivyo samaki wanaovuliwa bahari ya Hindi ukiwapata waliovuliwa leo leo wanakuwa watamu lakini ukipata walio lala hawan ladha kabisa sababu wanakuwa tayari wamewekewa dawa ya maiti.
Kwa mada hii tunategemea TFDA wafanye utafiti kujua ukweli kama samaki wanatiwa dawa ya kuhifazia maiti na ni nini madhara kwa mlaji, na kama hawatiwi hiyo dawa ni kwa nini basi samaki hawana ladha kama zamani.