Je, ni kweli baadhi ya wanawake/wanaume wana mikosi hapa Duniani?

Habari hapa kuna mada 2 alafu zimechanganywa , kiufupi MWANAMKE ulie nae hana mikosi,isipokuwa ww umefanyiwa mambo ya kichawi ili ufilisike uwachane na mkeo,cha kufanya pambana kurudisha nyota yako mambo yako yatakaa sawa, kuhusu ukoo wa nane hiyo ni kweli watu wanawake au wanaume wenye mikosi yaani ukishirikiana nao kila kitu chako kinapote hata kama kazi unaweza ukasimishwa, kwa hiyo mkeo hana tatizo ww ndio umefungwa jifungue sasa
Ahsante mkuu. Nitalifanyia kazi mkuu.
 
Kumbe haya mambo yapo, Kuna kijana mmoja kila akipanga mambo yake yakae kwa namna anavyotaka yanagonga mwamba, Nashindwa kuelewa anafeli kwenye mikakati yake au nae ndio wale wenye mikosi.?..!
 
Kumbe haya mambo yapo, Kuna kijana mmoja kila akipanga mambo yake yakae kwa namna anavyotaka yanagonga mwamba, Nashindwa kuelewa anafeli kwenye mikakati yake au nae ndio wale wenye mikosi.?..!
Yapo sana tu mkuu. Usiombe ukapigwa uchawi wa mikosi/nuksi.
 
Hata vidume wana gundu sana. Angalia mume wa janet Magu. Sijataja Rais,
Tangu jamaa ni waziri lkn mama kachokaaa hakuwa na usafiri wala ghorofa. Shamba la maana hana mpaka leo.
 
Hata vidume wana gundu sana. Angalia mume wa janet Magu. Sijataja Rais,
Tangu jamaa ni waziri lkn mama kachokaaa hakuwa na usafiri wala ghorofa. Shamba la maana hana mpaka leo.
Ndio maana yule amekuwa mwanamke mvumilivu kuliko watanzania wotee amekaa ktk miaka kibao hakuna malalamiko lkn cc tunamlaumu huyu mzee mpaka pasi embu tuwe na moyo WA yule mama tuache lawama siziso na msingi
 
Waganga Wa Tanga wanawaza mapenzi tu.. Hebu Jaribu Kigoma na Sumbawanga
Hahaha kaenda kwa yule Mzee wa Maguzoni ilitakiwa aende Pangani au Handeni, Lushoto na yenyewe si pabaya sana.....
 
Omba tu kwa imani yako muombee na huyo mwanamke ..hakuna mikosi/laana mbele ya Mungu.
 
me nahis kuna kaukweli flan asee..binafs kuna binti nilikuwa na mahusiano nae miaka kadhaa iliyopita,kila jambo langu nililokuwa nalifanya lilikuwa halifanikiwi ,mwisho wa siku nilivyokuja kuachana nae nikashangaa milango ya neema inafunguka .mpaka nikawa nahis ni yeye alikuwa kanifunga au nyota zetu hazikuendana tu
 
Mtu mwenye gundu anaweza kukabidhiwa ikulu na kuongoza watu milioni 60?Anashindwaje kujenga gorofa wakati ana uwezo wa kuchota pesa atakazo na hakuna wa kumuuliza?
Hata vidume wana gundu sana. Angalia mume wa janet Magu. Sijataja Rais,
Tangu jamaa ni waziri lkn mama kachokaaa hakuwa na usafiri wala ghorofa. Shamba la maana hana mpaka leo.
 
Huwa siyo gundu huwa ni nyota kutoendana. Kwa wavuvi, wawindaji na wachimba madini haya mambo huwa yanajionyesha kwa uharaka sana. Wanasema nyota zimegawanyika katika makundi manne

Maji
Upepo
Moto
Udongo

Hivyo unatakiwa nyota yako iwe upande unaosapoti juu ya nyota ya mwenzako
Ukiwa na nyota ya upepo harafu mwenzio yuko maji maisha yenu yatakuwa ni tufani tu

Ila kama ni upepo mwenzio ni moto maisha yenu yatakuwa fuel mteremko

Kama we ni udongo mwenzio ni moto basi ni kuunguzana tu bila la maana ila akiwa ni maji basi mtamea kama muwaridi ndani ya bustani
 
😂😂😂 ila nahisi ni tabia yao yakimatumizi kwa wiki anahudhuria shuhuli 10 na Kila shuhuli na nguo yake pesa itakaa saa ngapi
 
Kwa wale mliopata bahati wa kutinga kakola mining pale..kuna Dada alikuwa na uzuri wa kila Aina...ila kila mtu aliyemgusa hakumaliza wiki lazima kibarua kiote nyasi..
Hizi mambo u knever know..
 
Inawezekana hilo mkuu,mahali ninapokaa kuna mama ni mama ntilie nyumba jirani,sasa anabinti yake ambaye angeweza kuwa anamsaidia mama yake kazi hiyo......nilikuwa nikimuuliza mara kadhaa why hamsaidii mama yake hakuwa ananipa majibu sahihi sana anakwepa kwepa.....kuna siku aniambia nilishangaa.......anasema akienda kuuza yeye chakula hakiuziki na kina lala.....akaenda mbali zaidi akidai ameolewa mara 2,wote alioolewa nao walirudi nyuma kimaendeleo ila soon baada ya kuachika wakarudi kawaida.....mmoja alikuwa na kiduka 'mangi stole" huyu ndani ya mwezi tu alifunga.......bodaboda alipata misukosuko mingi ya kutosha tu nusura afe kwa ajali.....ila wote baada ya kuachana nao wanaendelea vizuri na maisha yao.

Alinishangaza kwa hiyo mikasa sana.......mama yake akaja kuniongezea facts zingine mpaka leo sijapata majibu
 
Back
Top Bottom