Je, ni kweli baadhi ya wanawake/wanaume wana mikosi hapa Duniani?

Arturo

Member
May 30, 2020
24
56
Salaam,

Ni matumaini yangu makubwa kwamba wote tu wazima wa afya njema. Na kama kuna mtu anaumwa au afya yake imetetereka kidogo basi mwenyezi Mungu atakusimamia ili uweze kupona haraka na kuriudi katika hali yako ya kawaida.

Kama kicha chwa huu uzi kimesemavyo ni kwamba nimekuwa nikisia watu wa rika tofauti tofauti wakisema kwamba kuna baadhi ya wanawake/wanaume wana mikosi wakiwa na maana kwamba itakapotokea umeanzisha mahusiano ya kimapenzi basi ujue hata harakati zako za kutafuta riziki zitakuwa ngumu sana au utakumbana na hali ngumu au changamoto mbalimbali za kimaisha.

Lengo kubwa la kuleta huu uzi ni kupata uzoefu kutoka kwa baba, mama, kaka na dada zetu ambao walishawahi kukumbana au kukutana na kitu kama hiki katika harakati za kutafuta maisha.

Bila kuwachosha ni kwamba nikiwa mwaka wa tatu mwaka 2014 katika chuo kikuu cha Dar es salaam nilianza kufanya biashara ya vipodozi na biashara ya uwakala wa tigo na Voda ambapo niliweza kupanga fremu kule kariakoo. Kiukweli, Mungu alinijalia katika biashara yangu na katika safari ya kutafuta maisha mazuri. Ilipofika mwaka 2015 nikiwa mwaka wa nne chuo nilikutana na mwanamke fulani pale ubungo-kibo tukajikuta tumeingia katika mahusiano ya kimapenzi. Niwe mkweli tu ni kwamba huyo mwanamke alikuwa ni mwanamke mzuri sana. Baada ya penzi kunoga, nilikuta nimeweka kule dukani ili aweze kusaidiana na mdogo wangu kutoa huduma nzuri kwa wateja.

Cha kusikitisha ni kwamba biashara ilianza kuyumba kwa kasi sana. Hata ile faida ambayo nilikuwa naipata ikawa imepotea kabisa. Pamoja na kuwa mkali na mwenye mashartui magumu kuhakikisha biashara inarudi ilipokuwa bado hali ya biashara ilizidi kudidimia kwa kasi sana. Wale wateja wote walihama hivyo mwisho wa siku mauzo yakapungua kwa kiasi kikubwa sana.

Katika kupambana kuhakikisha biashara inarudi kama ilivyokuwa ilibidi niuze IST yangu ili kuongeza nguvu katika bishara yangu. Pia ilibidi niisimamie mimi mwenyewe ikiwa ni pamoja na kwenda na kuhakikisha mauzo yanaratibiwa ipasavyo. Pamoja na kufanya hivyo hali ya biashara ilizidi kuwa mbaya sana mpaka ikafikia muda hata fremu ziwezi kulipia mpaka nichukue hela katika vyanzo vingine vya uchumi kulipia fremu. Katika imani ya kibiashara ukiona tu unaanza kutumia chanzo kingine kuboresha biashara nyingine tambua kwamba hiyo biashara imekufa kifo cha mende.

Baada ya kuona hali inazidi kuwa mbaya ilibidi nitafute njia mbadala ambayo nilishauriwa na rafiki yangu na maneno kibao kwamba pesa haitafutwi na namna navyitafuta. Nakumbuka alipinipa namba ya simu ya mzee mmoja yupo Tanga sehemu moja inaitwa maguzoni. Aliniambia kwamba kama kuna jambo umefanyiwa ili usipate pesa basi huyo ni mtaalamu mzuri sana atakutibu vilivyo.

Basi siku ya jumamosi asubuhi niliondoka kuelekea Tanga kwa ajili ya tiba. Nilipofika nilikaribishwa na yule mzee na mwisho wa siku nikamuelezea kinachonisibu katika maisha yangu ya kutafuta maisha. Baada ya kuchunguza katika mitambo yake akaniambia kwamba mwanamke wangu ndiyo chanzo cha pesa kunikimbia. aliendelea kunieleza kwamba kuna mtu ametokea kumpenda mwanamke wako na ametumia kila njia mbadala ya kukunyang'anya huyo mwanamke ameshindwa hivyo ameamua kwenda kuzika nyota yako makaburini ili usipate riziki yoyote na pindi utakapofulia huyo mwanamke kwa sababu utakuwa huna kipato chochote cha kumhudumia. I was really scared but sikuishia hapo nikamtafuta mtaalamu mwingine ikanipa jibu lilelile kwamba tatizo ni mke wako ndiyo mwenye gundu(nuksi).

Sikuridhika na majibu ya huyu mataalamu wa pili kama ambavyo sikumuamini yule mtaalamu wa kwanza. Ikabidi nizamie tena pangani. Nikapewa jibu lilele. Katika kutafuta hiyo tiba sijawahi kumwambia ukweli kuhusu hicho kitu.

Hivyo Kutokana na niliyoyaeleza hapo juu, Naomba tusaidiane haya maswali ya hapa chini waungwana.

1. Je ni kweli kuna watu (wanawakeau wanaume wana mikosi ambayo inaweza kumuathiri mtu mwingine?
2.Je ulishawahi kukutana na shuruba za namna hiyo?
3. Ulitumia mbinu gani kupambana na matatizo kama hayo
4. Nimwambie ukweli huyu mwanamke au nimpotezee tu kuhusu hayo magundu yake?

Waungwana, nimeshindwa kuandika kila kitu kwa sababu sipendi niwachoshe kusoma. Ingawa kama utakuwa na swali au unataka ufafanuzi basi nipo tayari kwa hilo.

Karibuni kwa michango na ushauri wana MMU.
 
Ni kweli Kuna watu wanamikosi Sana tena wengine wana laana za ukoo na familia sio kila MTU ni wakumvamia tu utapotea,wengine hata kwenye biashara ukishirikiana nao tu umekwisha Mimi Kuna ukoo mmoja niliambiwaga ukikanyaga shambani kwako tu basi mwaka Huo huvuni.Kuna binti mmoja pia namfahamu yeye Hana kasoro yeyote ile na nimcha mungu balaa lakini hakuna mwanaume anayethubutu kumtongoza na umri unazidi kwenda tu
 
Off course ni vitu vinavyopatikana kwenye jamii zetu pamoja na wengne kutokuamini uchawi lakini Ni vitu vipo binafsi nililisikia na wakati fulani iliwahi nitokea kuna mdada mmoja nlikua nae kwenye mahusiano kabla ya hapo Moshe zangu zilikua zinaenda vizuri tu lakni nilivoanza kua nae mambo yakaanza kubadilika pesa zikapotea ila nilivoachana nae mambo yakaanza kwenda poa tena nikaamini kweli kuna watu wana gundu
 
Shida ni uzinzi na zinaa mnayofanya. Oa kama mnapendana na mjiweke wakfu kwa Mungu au Allah
 
Maandiko gani? Mbona Mfalme Suleman alifanya zinaa na wanawake 300 na bado Mungu wa Israel alimpenda na kumpa baraka kama zote?
Quran Tukufu
[Surah Al-Isrā’ ayah 32]inasema.
Wala msikaribie uzinzi hakika huo ni uchafu na njia mbaya
 
Wabondei wanaitwa mlango wa nane
Habari hapa kuna mada 2 alafu zimechanganywa , kiufupi MWANAMKE ulie nae hana mikosi,isipokuwa ww umefanyiwa mambo ya kichawi ili ufilisike uwachane na mkeo,cha kufanya pambana kurudisha nyota yako mambo yako yatakaa sawa, kuhusu ukoo wa nane hiyo ni kweli watu wanawake au wanaume wenye mikosi yaani ukishirikiana nao kila kitu chako kinapote hata kama kazi unaweza ukasimishwa, kwa hiyo mkeo hana tatizo ww ndio umefungwa jifungue sasa
 
Back
Top Bottom