Je ni kitu cha hatari kinaninyemelea?

Je ni kitu cha hatari kinaninyemelea?

Dafugwadu

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2012
Posts
4,734
Reaction score
5,247
Habari wanajukwaa nimekosa amani tangu jumanne
ilikuwa hivi, nililala usiku nikaota ndoto nimepooza upande wa kulia,
Lakini ile kustuka kweli ule upande wote ulikuwa umepooza.

Nilikuwa na kiu kali sana ikabidi nimuamshe wife anipe maji ya kunywa.
Sikuweza kuyashika yale maji ikabidi aninyweshwe kwa mbinde sana nikayamaliza.

Basi nikarudi kulala huku nimepooza wife analia, ile kustuka asubuhi najiona mzima kabisa je ni dalili gani hizi?
 
Kama wewe ni mtu wa imani ingia kwenye maombi na kufunga,muombe Mungu akuonyeshe.
 
wahi nenda hospitali mzee,iwahi hiyo stroke haipo mbali hizo ni dalili...zingatia kwamba hiyo ni stroke inakuja na haipo mbali kukupiga
 
Mkuu, ingia rehema,katika ulimwengu wa roho hilo jambo tayari, na uharibifu umeshakupata, bado kudhibitika tu kwenye mwili... Tafuta msaada wa kiroho haraka
 
Pole sana Anguko Hilo linataka kukunyemelea nenda ukafanyiwe maombi Kwa watu sahihi
 
Habari wanajukwaa nimekosa amani tangu jumanne
ilikuwa hivi, nililala usiku nikaota ndoto nimepooza upande wa kulia,
Lakini ile kustuka kweli ule upande wote ulikuwa umepooza.

Nilikuwa na kiu kali sana ikabidi nimuamshe wife anipe maji ya kunywa.
Sikuweza kuyashika yale maji ikabidi aninyweshwe kwa mbinde sana nikayamaliza.

Basi nikarudi kulala huku nimepooza wife analia, ile kustuka asubuhi najiona mzima kabisa je ni dalili gani hizi?
Pole Mkuu hiyo ni dalili mbayaya wewe kupooza upande mmoja na ni dalili ya pepo mchafu anakunyemelea kutaka kukutia maradhi na hayupo mbali na wewe kukutia hayo maradhi nitafute mimi kwa wakati wako ili nipate kumuondoa huyo pepo mchafu anayetaka kukutia hayo maradhi ya kupooza upande mmoja aka stroke.
 
Yaani wewe unamtoa pepo kwa nguvu zipi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom