Emanueli misalaba
JF-Expert Member
- Dec 12, 2016
- 1,113
- 1,659
Wana jukwaa pendwa la Jf habarini za leo!
Katika kuja kwangu mara moja Dar es salaam nikitokea zanzibar niliamua nichukue zawadi walau kiduchu kwa ajili ya shemeji yangu sukari kilo 5, cha ajabu nilipofika bandarini Dar kulingana na maelezo ya wakanguzi wa bandarini wamenifanya niwe na maswali kadhaa moyoni mwangu na hasira zikawaka sana nafsi mwangu, wakasema sukari kutoka zanzibar kuja bara hairuhusiwi hata kama ni nusu kilo hata kama ni kwa matumizi ya nyumbani.
Mm najiuliza kwani zanzibar si sehemu ya Tanzania?
Kwani sukari ya zanzibar ina madhara kwa mlaji?
Uharamu wa sukari ya zanzibar kuja nayo Bara ni upi?
Hivi mtu akiwa anatoka na sukari kutoka Mwanza anahojiwa? Hivi ile kamati ya kushughulikia kero za Muungano hili hawajaliona?
Wiki iliyopita nilisafiri na mchele kilo 10 kutoka Dar es Salaam kwenda nayo zanzibar sikuulizwa na mtu yeyote wa bandari zote mbili.
Niwaombe wizara ya Muungano ituambie wananchi ni bidhaa zipi haziruhusiwi kutoka bara kwenda zanzibar na kutoka zanzibar kuja Bara.
mmmmmh nusu nasadiki na nusu sisadiki.Bidhaa nyingi kutoka Zanzibar huzuiliwa bandari za Bara kwa sababu ya kuchanganyikana na bidhaa za kimagendo, dumped cheap products na maswala ya kodi
Kiufupi ndugu zetu wanateleza na huu muungano kuliko sisi.
Wewe peleka hata ubuyu kule hakuna wa kukuuliza, ila beba hata mchanga kule uone kimbembe hapo ferri.
Hebu kaa angalau dakika moja ufikirie.Huu ni Muungano wa Kipekee duniani, Mtanzania Bara anaye ung'ang'ania ndo Ananyonywa, anayetaka uvunjike ndo mnyonyaji mkuu
Britannica
umeona nadhani ile asubuhi kwa namna ambavyo nilivimba ningekuwa na bastola leo ningekuwa ndani,Kero aswaa
Zanzibar ni nchi ya kigeni... muungano ni kung'ang'anizana hautofautiani na nyumba ya mabua...Wana jukwaa pendwa la Jf habarini za leo!
Katika kuja kwangu mara moja Dar es salaam nikitokea zanzibar niliamua nichukue zawadi walau kiduchu kwa ajili ya shemeji yangu sukari kilo 5, cha ajabu nilipofika bandarini Dar kulingana na maelezo ya wakanguzi wa bandarini wamenifanya niwe na maswali kadhaa moyoni mwangu na hasira zikawaka sana nafsi mwangu, wakasema sukari kutoka zanzibar kuja bara hairuhusiwi hata kama ni nusu kilo hata kama ni kwa matumizi ya nyumbani.
Mm najiuliza kwani zanzibar si sehemu ya Tanzania?
Kwani sukari ya zanzibar ina madhara kwa mlaji?
Uharamu wa sukari ya zanzibar kuja nayo Bara ni upi?
Hivi mtu akiwa anatoka na sukari kutoka Mwanza anahojiwa? Hivi ile kamati ya kushughulikia kero za Muungano hili hawajaliona?
Wiki iliyopita nilisafiri na mchele kilo 10 kutoka Dar es Salaam kwenda nayo zanzibar sikuulizwa na mtu yeyote wa bandari zote mbili.
Niwaombe wizara ya Muungano ituambie wananchi ni bidhaa zipi haziruhusiwi kutoka bara kwenda zanzibar na kutoka zanzibar kuja Bara.
Kwa vile mnazidi kutuita watanzania bara nchi ambayo haipo na haijawahi kuwepo tutawtoza ushuru mpaka mtuite watanganyikaKero aswaa
Huo ndo ukweli.... Zanzibar biashara za magendo na dumped cheap products ni kwa sana licha ya kuwepo TRA na Vyombo vya Ulinzi na Usalama (Polisi, JWTZ navy command, Uhamiaji na TISS).mmmmmh nusu nasadiki na nusu sisadiki.
Kwani TRA, TIIS na majeshi mengine ya kupambana na magendo zanzibar hawaruhusiwi kufanya kazi kule?