Je ni anguko la jukwaa la wahariri wa habari?

Mugabe one

JF-Expert Member
Nov 15, 2016
2,327
1,684
Baada ya star TV kutangaza kurusha LIVE kipindi cha mahojiano na RC MAKONDA Siku ya tarehe 22/5/2017 kinyume na tamko la jukwaa la wahariri chini ya Neville Meena, Sasa vituo vingine vya TV vimeoganaizi kipindi na RC Makonda tarehe 10/6/2017 Azam, na Tarehe 28/6/2017 Sibuka Tv.
Je anguko la jukwaa la wahariri wa habari litakamilika dhidi kumpa kisogo RC Makonda?
 
Kwa mtu anayeelewa misingi ya nchi ya kidemokrasia na wajibu wa vyombo vya habari kutoa habari, pamoja na haki za wananchi kupata habari, hili zoezi zima la vyombo vya habari kumsusia mtu kwa pamoja ni ujinga.

Waandishi wa habari wana wajibu wa kuandika habari.

Wananchi wana haki ya kupata habari.

Waandishi kutoandika habari za mtu fulani ni kufanya makosa kwa namna mbili.

Namna moja, wanashindwa kutimiza wajibu wao wa kutoa habari kwa wananchi.

Namna ya pili, wanawanyima wananchi haki yao ya kupata habari.

Maamuzi kama haya ambayo hayajatokana na kanuni zenye kina hufa kifo cha asilia tu.

Hata kama Bashite kaharibu- pengine hususan kwa sababu kaharibu- anahitaji kuandikwa na kuwa covered zaidi na zaidi.

Kumsusia ni sawa na kusema afanye anachotaka hatujali.

Na haya yote yanasemwa nami, mtu asiyemfagilia Bashite.

Makonda hatakiwi kususiwa.

Makonda anatakiwa kuzidishiwa kuhojiwa na kumulikwa.
 
Bashite naye kwa nini asiyende kwenye telepicha ya baba yake angejifanyia mambo yake pale kwa uhuru na angeondoka kwa sarutti au na yeye amagundua kuwa TBC haina watazamaji hahaa
 
point mkuu
 
Hili jambo lenyewe limeegemea mahala fulan kama ukilitizama kwaundan.ila nimependa maon ya al watan kama kwel hatupo kimirengo bas maon yake mazur sana.jukwaalahabar linakutana naaibu nyingine mudasio mref
 
Wacha wakandamizwe na serikali hadi akili ziwakae sawa kama wameshindwa kuungana!
Wenye nguvu wanaungana kumkabili mnyonge ila wanyonge hawaoni umuhimu wa kuungana(shame on you waandishi wa habari)
Mtaendelea kukamatwa hovyo
 
>>> njaaa bwana njaaaaaaaaa hizi stations hizi HATA kama zinamilikiwa na MABILLIONER njaa IPO >>>
 
Kwa mtu anayeelewa misingi ya nchi ya kidemokrasia na wajibu wa vyombo vya habari kutoa habari, pamoja na haki za wananchi kupata habari, hili zoezi zima la vyombo vya habari kumsusia mtu kwa pamoja ni ujinga.

Waandishi wa habari wana wajibu wa kuandika habari.

Wananchi wana haki ya kupata habari.

Waandishi kutoandika habari za mtu fulani ni kufanya makosa kwa namna mbili.

Namna moja, wanashindwa kutimiza wajibu wao wa kutoa habari kwa wananchi.

Namna ya pili, wanawanyima wananchi haki yao ya kupata habari.

Maamuzi kama haya ambayo hayajatokana na kanuni zenye kina hufa kifo cha asilia tu.

Hata kama Bashite kaharibu- pengine hususan kwa sababu kaharibu- anahitaji kuandikwa na kuwa covered zaidi na zaidi.

Kumsusia ni sawa na kusema afanye anachotaka hatujali.

Na haya yote yanasemwa nami, mtu asiyemfagilia Bashite.

Makonda hatakiwi kususiwa.

Makonda anatakiwa kuzidishiwa kuhojiwa na kumulikwa.

Kwa aliyoyafanya Bashite wana haki ya kumsusa wakimuendekeza basi wajiandae kunyanyaswa hivyo kila siku halafu mbona Mabaya yake bado yanatolewa tu Ila hapewi kiki kwa lolote linaloonekana jema waendelee hivihivi.
 
Saafi sana! Yule Balile na timu yake walifanya maamuzi ya kukurupuka sana. Inabidi wake wajitafakari kama wanatisha kwenye hicho chombo chao
 
Mkulu kawapa Hela ya kutosha TBC wajipange upya
Baada ya star TV kutangaza kurusha LIVE kipindi cha mahojiano na RC MAKONDA Siku ya tarehe 22/5/2017 kinyume na tamko la jukwaa la wahariri chini ya Neville Meena, Sasa vituo vingine vya TV vimeoganaizi kipindi na RC Makonda tarehe 10/6/2017 Azam, na Tarehe 28/6/2017 Sibuka Tv.
Je anguko la jukwaa la wahariri wa habari litakamilika dhidi kumpa kisogo RC Makonda?
A
 
Kwa aliyoyafanya Bashite wana haki ya kumsusa wakimuendekeza basi wajiandae kunyanyaswa hivyo kila siku halafu mbona Mabaya yake bado yanatolewa tu Ila hapewi kiki kwa lolote linaloonekana jema waendelee hivihivi.

Kwa nini unafikiri kuandika habari zake ni kumuendekeza?

Mimi naweza kukuambia kwamba, kama unaelewa jukumu la vyombo vya habari, kutoandika habari zake ndiyo kumuendekeza.

Any attempt at a synchronized reporting (or non-reporting) of the news is one step towards Orwellian totalitarianism.

As a civil libertarian, I oppose Orwellian totalitarianism in all its forms.

Hayo mambo za habari za kuchaguliwa ndiyo tuliyoyakataa enzi za RTD. Sasa tunaotaka mageuzi na maendeleo tukiwa bado tunataka habari za kuchaguliwa tutakuwa tunajichanganya.Tutakuwa hatueleweki kwamba tunaenda au tunarudi.

Ukishaanza kukubali baraza la habari lipange habari gani iandikwe na habari gani isiandikwe, kwa magazeti yote, kitu gani kitakufanya usikubali kazi hiyo aifanye Magufuli?

Kwa kweli baraza lolote la muungano wa wanahabari linalokaa chini na kuazimia kususia kuandika habari za mtu yeyote linanipa maswali mengi sana kuhusu ukomavu na weledi wa hilo baraza, kama kweli linaelewa jukumu la wanahabari katika nchi ya kidemokrasia.

Napenda kutoa mifano ya extreme ili kuelezea point yangu. Tuseme Bashite anafanya mambo mabaya sana. Ni kama muuaji anayetuua polepole. Tukubaliane hapo kwa minajili ya kuchunguza kama kumuandika ni jambo linalofaa au lisilofaa.

Hivi hapo mjini akiingia muuaji anakamata watu usiku na kuwaua, kila usiku anaua mtu mmoja, utasema muuaji huyu habari zake mbaya waandishi wasusie kuandika habari zake au utataka waandishi watuarifu kila siku yuko wapi ili tujihadhari na kujipanga kumkamata?

Sina tatizo na waandishi wa magazeti tofauti kama wanasema hawataki kumuandika vizuri Bashite (kama vile magazeti mengine yasivyotaka kuwatoa picha terrorists wanaotaka kujulikana). Kama Bashite anaitisha press conferences za kijinga, waandishi watakaoenda na kuacha kuandika habari za hizo press conferences na kuuliza habari za vyeti na matumizi mabaya ya ofisi nitawaelewa.

Lakini waandishi watakaokataa kwenda kabisa sitawaelewa.

Watakuwa wamepewa nafasi ya kuuliza chochote, na wameiacha. Wametupunja wananchi tunotaka kuona Bashite anaulizwa maswali zaidi. Wameshindwa kufanya kazi yao.

Tatizo naona tumeiga tu haya mambo bila ya kuyaelewa misingi yake ni nini.Ndiyo maana ninapoeleza kwamba wanahabari kumsusia Makonda ni kituko nakuwa sieleweki kwa wengine.

Makonda ana dhamana bado. Hata kama hatumtaki. Kama hatumtaki suluhisho si kumsusia habari zake. Suluhisho ni kummulika zaidi mpaka aondolewe.

Juzi rais Trump alitembelewa na rais wa Colombia White House. Waandishi wasiompenda hawajasusia kuandika habari zake.Wamejitokeza kwa wingi sana, ila, badala ya kuuliza kuhusu masuala ya biashara za Marekani na Colombia kama mtu angetegemea kutoka mkutano huo, wamemuuliza Trump habari zilizo katika headlines sasa kuhusu Russia.

Waandishi wa kibongo kwa nini hawawezi kufanya hivi? Wakishindwa kumbana Mkaonda na kuandika habari za uchambuzi nitawaona wameshindwa kufanya kazi yao.

Uhuru wa kutoa na kupewa habari ni wa muhimu sana kiasi kwamba umewekwa katika katiba ibara ya 18.

Na hili ni jambo la msingi nchi za kidemokrasia dunia nzima. Si Tanzania tu.

Unapotaka waandishi wa habari wamsusie Bashite, akiiba hela huko, akipanga uvamizi mwingine, akiharibu mambo zaidi, utasema wamsusie pia tusijue anachofanya?
 
Back
Top Bottom