Je, NEC itadhihirisha kuwa wagombanao ndio wapatanao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je, NEC itadhihirisha kuwa wagombanao ndio wapatanao?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 17, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145

  Na John M. Kibasso

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kinatarajia kufanya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) mwezi huu. Kikao hicho kitafanyika mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete.

  Wachambuzi wa siasa, wapenzi, wakereketwa na jamii nzima ya watanzania masikio, macho na fikra zao zitahamishia Dodoma. Wengi wanashauku kubwa ya kutaka kujua utekelezaji wa falsafa ya kujivua gamba ambayo iliasisiwa na Rais Kikwete mapema Februari 5, mwaka huu.

  Vyanzo vya habari za ndani ya sekretarieti ya CCM zimebaini kuwa pamoja na mambo mengine yatakayorindima kwenye mkutano huo, yapo masuala mengine ya msingi zitakazopewa kipaumbele ambazo ni kama zifuatazo; mdororo wa hali ya uchumi katika nchi yetu, tatizo la ajira kwa vijana, kupanda kwa bei ya bidhaa adimu na mgogoro uliopo ndani ya Umoja na Vijana wa chama hicho (UVCCM).

  Nafungua pazia ya makala haya kwanza kukitakia kheri na fanaka kikao hicho kijacho cha (NEC) CCM Taifa. Naamini Watanzania wote wenye mapenzi ya dhati na nchi hii watakubaliana nami kuwa kuteleza kwa CCM kinaweza kusababisha nchi kuyumba na kushindwa kutawalika.


  Kuna dhana iliyojengeka miongoni mwa watanzania wengi mijini na vijijini hususani wale wanaofuatilia siasa za nchi hii kwamba, kadri siku zinavyokwenda wamefikia tamati kuamini matatizo ya kiuchumi (ugumu wa maisha) yanayowatesa jamii yameletwa na utawala mbovu wa CCM.


  Wengine wakiyaita "Siasa mbovu za kifisadi" ilimradi mijadala na mambo mengine yanayovurumishwa na vyama vya Upinzani kama yale yanayoendelea katika mji wa Arusha, yote yanatafsiriwa kama ni udhaifu wa uongozi wa CCM na Serikali yake.


  Binafsi napenda kutofautiana kabisha na mtizamo wa baadhi ya wadau wanaodhani kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefilisika kisera na kiitikadi eti kwa sababu kimekumbatia mafisadi.


  Naomba kuweka wazi kuwa mdororo wa kiuchumi kilichosababisha bei za bidhaa adimu kupanda na ukosefu wa ajira haijatokana na utawala mbovu wa Rais Kikwete na chama chake.


  Wote ni mashuhuda kwa wale wanaofuatilia matukio katika mataifa mengine, watakubaliana nami kuwa si Rais Kikwete wala CCM kilichosababisha ugumu wa maisha kwa raia wa nchi hii.


  Kwingineko katika mataifa makubwa kutoka Bara ya Ulaya, Asia, Marekani na hapa kwetu Afrika, hakuna taifa lolote ambalo limetulia kisiasa, kiuchumi na kijamii.


  Baadhi ya nchi kama Ugiriki, Ureno, Italia n.k. kwa sasa uchumi wao umefikia mkanda mwekundu, kwa maana nyingine, nchi hizi zimefika ukomo wa kutokopesheka.


  Hali hii ilisababisha Waziri Mkuu wa Ugiriki kujiuzulu. Suala la kujiuliza je, ni kwa nini mataifa haya makubwa yanakumbwa na mdororo wa kiuchumi? Kwanini tumbebeshe lawama Rais Kikwete ilihali tukijua kuwa matatizo haya yameanzia katika nchi zilizoendelea kuliko nchi zetu hizi masikini za Kiafrika.


  Kimsingi, mdororo wa uchumi na mikwaruzano ya vyama ni kitu cha kawaida. Hizi minyukano tunazozishuhudia ndani ya CCM ni matukio madogo sana ukilinganisha na matukio katika nchi nyingine.


  Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na chombo cha umoja wa mataifa kinachosimamia haki za binadamu, Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazoongoza katika Bara la Afrika tukizungumzia uhuru wa vyombo vya habari, utawala wa sheria na haki za raia kutamka wanalotaka bila bughudha.


  Baadhi ya watu hususan vyama vya Upinzani wamediriki kuvurumisha kashfa nzito dhidi ya CCM ilimradi jamii waione kuwa CCM ni chama cha mafisadi. Watafiti wa maisha ya wanyama wanasema ni vigumu kutofautisha maumbile na tabia ya wanyama wa porini na wale wa kufugwa.

  Kwa mfano, ni vigumu kumtofautisha mnyama ngiri wa porini na nguruwe wa kufugwa, hali kadhalika ni vigumu kumtofautisha swala wa porini na mbuzi wa kufugwa. Watafiti wanasema kuwa wanyama hawa wote wana maumbile sawa na mfumo wao wa uzazi na kuishi ni sawa.


  Niseme tu kwamba haiingii akilini kutofautisha vyama vya kisiasa hapa nchini ilihali vyote vimefuata mchakato sawa ya usajili, wanachama wao ni Watanzania walewale, viongozi wao ni Watanzania walewale.


  Hakuna chama kinachoweza kujigamba kwamba kinaweza kuleta maajabu na kubadilisha sura ya nchi hii kisiasa, kiuchumi na kijamii. Wote wana maumbile sawa kama walivyo wanyama wa porini na wale wa kufugwa. Vyama hivi navyo vimejaa mafisadi.


  Nathubutu kusema kuwa hakuna kiongozi yeyote kutoka vyama vya upinzani ambaye anaweza kufanya miujiza ya kuleta mafanikio kiuchumi kumzidi Rais Kikwete. Au nani atathubutu kusema kuwa kuna chama makini kuzidi CCM. Kwanini tufichane kila kukicha tunashuhudia matukio ya ajabu yakifanywa na vyama hivi vya upinzani hata kabla hawajashika dola. Nchi gani imeendelea kwa sababu ya kusheheni maandamano yasiyokuwa na tija.


  Naam, napenda kujielekeza katika kikao kijacho cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Taifa (NEC). Nionavyo mimi, kikao hichi hakika kitawaumbua wale wote waliodhani kuwa kutofautiana kifikra na kimtazamo ndiyo mwisho (omega) wa chama. Kutofautiana kifikra ni dalili ya ukomavu wa kisia ndani ya chama husika.


  Hapana shaka mengi yanasemwa na hoja nyingi bado yanajadiliwa na weledi wa siasa hapa nchini kuhusu mpasuko ndani ya CCM.


  Wengine wameenda mbali kufananisha hali ya siasa ya Nchi hii na yale yanayotokea katika nchi za Kiarabu. Mataifa mengi ya Kiarabu yamekumbwa na michafuko ya siasa yaliyosababishwa na utawala wa kimla katika nchi hizo.


  Nashawishika kuamini kuwa kikao kijacho cha NEC (CCM) Taifa kitakuwa ni kikao cha kihistoria ambacho wajumbe wote watadhihirishia umma wa watanzania kuwa CCM ni chama kikongwe na hakuna chama kingine kinaweza kikafananishwa nacho hapa nchini hata katika bara zima la Afrika.


  Binafsi nachukulia kikao cha NEC Taifa CCM kwamba kitakuwa ni kipimo cha utendaji wa sekretarieti mpya. Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama ni jemadari hodari na mkongwe mwenye uwezo wa kusoma alama za nyakati katika kusimamia, kutetea na kulinda maslahi ya chama na wanachama wake.


  Kwa wale wanaofuatilia utendaji kazi wa Mukama, atakubaliana nami kuwa yeye siyo mtu wa maneno mengi bali ni mtendaji. Naamini kikao kijacho cha NEC kitawashangaza wafuatiliaji wengi wa siasa katika nchi hii. Amini usiamini CCM kitazaliwa upya huku makundi yaliyokuwa yakihasimiana yatabaki kuwa historia. Makundi yote yatarudi kuwa kitu kimoja kwa maslahi ya chama na taifa kwa ujumla.


  Kwa vyovyote vile, wajumbe wa kikao hicho cha NEC, watapaswa kutulia na kutumia busara ili kuepusha mgogoro wowote unaoweza kuzuka wakati wa majadiliano. Vinginevyo majibu mepesi kwa mambo muhimu yanayogusa Taifa, yanaweza kuyumbisha nafsi na matarajio mema ya jamii hatimaye wakaanza kukosa imani na Serikali yao.


  Sitaki kutabiri wala kupiga ramli, ninachotaka kusema ni kuwa, Mwenyekiti Rais Kikwete, ataonyesha umakini na busara zake ili kudhihirishia watanzania kuwa hawakufanya makosa kumchagua kuwa Rais wa nchi hii. Pamoja na hilo, Rais Kikwete hatopenda CCM kumpasukia mkononi mwake. Kikwete atapenda afuate nyayo za watangulizi wake (Nyerere, Mwinyi na Mkapa) ambao kwa pamoja walirudisha CCM mikononi mwa wale waliowakabidhi baada ya muda wao wa urais kumalizika.

  Sipendi na sitaki kumsemea Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama. Nionavyo mimi, Katibu Mukama atapenda kuliwaza wapenzi wa CCM na wote wasiokuwa na ushabiki wa vyama kwamba CCM kipo tayari kuwatumikia jamii yote pasipo kujali wenye nacho na wasio nacho.


  Hakika dhana ya kujivua gamba litang'arisha kikao hicho na kutumika kuunganisha makundi ndani ya chama hatimaye wajumbe watatoka na azimio lanye kuzingatia msemo wa wahenga lisemwalo "Wagombanao ndio wapatanao"


  Naamini kuna watu wasioitakia mema CCM kuendelea kuwa chama tawala. Watu kama hawa watanirushia madongo huku wakinikebehi kwa kila sifa za matusi. Mimi nawaambia wote: Tunajenga jumba moja, kwa nini tugombanie ufito?


  Tuangalie wenzetu wa Zambia, walijaribu kubadilisha chama tawala, lakini yaliyokuja kuwakuta kinajulikana. Wamebadilisha tena chama walichodhani kingewakomboa wametafuta mbadala. Somo la Zambia linatufundisha kuwa hakuna chama kinachoweza kuleta maajabu zaidi ya kile kilichopo madarakani. Kinachohitajika ni kuwaondoa viongozi ambao wameonyesha kutumia dhamana waliyopewa kwa maslahi yao binafsi aidha ndani ya chama au serikalini.

  Ili vyama hivi viweze kushindana na CCM, vinapaswa kuungana na kubaki chama kimoja chenye nguvu kama ilivyo Marekani (Democrats na Republican) au Uingereza (Labour na Conservative). Vinginevyo nasema kuwa kikao kijacho cha NEC Taifa CCM kitaandika historia mpya kwani "Wagombanao ndio wapatanao"

  Tupende tusipende Chama Cha Mapinduzi kina hazina kubwa ya wazee wenye busara nyingi ndani na nje ya nchi.


  Sitarajii kusikia kwamba hawa wazee wameshindwa kurudisha amani ndani ya chama. Matukio mengi yamekuwa yakiinyemelea chama hicho lakini siku zote viongozi walitumia busara kumaliza mitafaruku yote. Naamini Mwenyekiti Rais Kikwete atatumia uweledi wake wa kidiplomasia na bila shaka kikao hicho kitaweka azimio mpya ya upatanisho. Wahenga walinena "Zimwi likujualo halikuli likakumaliza" wajumbe wa CCM wanajua tangu enzi za TANU.   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  CCM kana inataka kufanikiwa inahitaji kuviondoa Vizee ambao wako Madarakani kwa Karne 2

  1. John Malecela
  2. Pius Msekwa
  3. Anna Abdalla

  Na wengine Wengi -- yaani watupwe Nje Acha wanao walio sasa
   
 3. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Haaa haa, kwahiyo wakiondolewa hawa vikongwe na magamba yatavuka?
  Nyie magamba kubalini ni siku ya kufa nyani miti yote ilisha teleza
  bye bye magambaz
   
Loading...