Je naweza kukopeshwa benki

Mbuna

JF-Expert Member
Jul 3, 2013
269
71
kwa sasa nipo field mbeya nasoma tanga chuo kkuu cha eckernforde! nina kiprot kama heka 1 je naweza enda bank na kukopa ili nifungue biashara? hati milik nnayo
 
hauwezi kupata kwa sasa mabenki wanatoa mikopo kwa biashara iliyopo sio kwenda kuanzisha,pia dhamana wanazokubali ni kitu kilichopo juu ya ardhi km jengo,ingawa vyombo vya moto km gari ikiwa bima kubwa inaweza kutumika km dhamana.
 
kwa sasa nipo field mbeya nasoma tanga chuo kkuu cha eckernforde! nina kiprot kama heka 1 je naweza enda bank na kukopa ili nifungue biashara? hati milik nnayo

nadhani ukilipima unaeza pata mkopo
 
nadhani ukilipima unaeza pata mkopo

Mkuu umetumia sentesi nzuri sana. Anaweza pata au akakosa. Kiukweli ni kwamba bank yeyote kabla hawaja mkopesha mteja wanatizama vigezo na uwezo wa mkopaji. Kukopa kwa'jili ya kuanzisha biashara ni ngumu kupata mkopo. Labda tunatakiwa kuelimishana kwamba benki nyingi zinatumia pesa za wateja wao kuwakopesha wateja wao wenye kuitaji mikopo. Kupata security haimaanishi kwamba unafaa kukopeshwa, ni sifa zinazigatiwa. Kutokana kwamba marejesho ni kila baada ya siku 30 lazima uwe na biashara inayoweza kustaamili mzunguko.
Kwa ushauri wangu, ni vyema kuanza biashara uliokusudia kidogo kidogo kwa kufanya hivyo una create demand katika soko lako. Kuliko kukimbilia kukopa kabla ya kuanza biashara. Hii itakusaidia sana. Kumbuka a customer to buy from you it is just a favor hata kama ni pacha wako.
Pia ukitaka kukopa lazima ujiulize maswali; mfano kama unataka kukopa 5m kwa miezi 12 na riba yake ni 20% or 22% ukijumlisha 5m + 22% = 6,410,256.41 if you divide by 12 months = 534,188 ambayo utatakiwa kulipa kila mwezi pia ukiigawa kwa siku 30 (534,188 / 30 = 17,806.27) unlike your fixed expenses lazima biashara yako kwa sasa kabla huja kopa iwe na uwezo wa kuingiza zaidi ya 18,000 kwa siku. Chini ya hapo utapata shida ya kulipa kwa kutegemea biashara husika. Pia lazima uwe na discipline na pesa za kazi.
Mkuu kwa ufupi kama huna uwezo wa kupata rejesho la mkopo unaoitaji kabla huja kopa jipange upya.
otherwise you will end up putting your financial status on a drip.
 
Back
Top Bottom