Chief lubengulla
Member
- Oct 16, 2012
- 15
- 2
Nimekuwa nikifuatilia shughuli zinazoendelea hapa Mwenge stendi ya Daladala cha kushangaza naona hata viongozi wako kimya niliongea na kijana mmoja mfanyabiashara akiwa amebeba meza yake ya biashara kichwani akasema mbona viongozi wa manispaa wanajua maana ukitaka upate sehemu ya kuweka angalau meza yako ya biashara lazima ulipe kiingilio cha TZS 50000 na baada ya hapo kuna ushuru wa Elfu 5000 kila ijumaa ya wiki.
Sasa sijui baadaye stendi hii itafungwa na kugeuzwa kuwa soko maana sioni juhudi zozote za makusudi zikifanywa na serikali. Ina sikitisha sana kuona watu kujiamlia tu sawa biashara ni nzuri lakini basi kuwepo na ustaraabu abiria wanahangaika sana hasa nyakati za jioni huku unatafuta gari na pia uwe makini na vibaka.
Ahsanteni