Je mwanandoa aliyesababisha ndoa kuvunjika naye anastahili mgao wa mali?


B

Bashir Yakub

Verified Member
Joined
May 27, 2013
Messages
36
Points
400
B

Bashir Yakub

Verified Member
Joined May 27, 2013
36 400
JE MWANANDOA ALIYESABABISHA NDOA KUVUNJIKA NAYE ANASTAHILI MGAO WA MALI ?.

Na Bashir Yakub.
0784482959


Watu wengi wamekuwa wakijiuliza ikiwa mmoja wa wanandoa aliyepelekea ndoa kuvunjika kama anastahili mgao wa mali. Mfano,mwanamke katika ndoa anaanzisha chokochoko makusudi ili ndoa ivunjike apate mgao wa mali aendelee na maisha yake.

Au mwanaume kwa tabia zake mbaya za ulevi au kutokuwa mwaminifu anapelekea ndoa kuyumba hadi kuvunjika kabisa. Je kwasababu amesababisha matatizo na ndiye chanzo cha tatizo mpaka ndoa kuvunjika anastahili mgao wa mali ?.

Mara nyingi tumeeleza kuhusu ndoa kuvunjika na misingi ya kugawana mali ambayo imewekwa na sheria hususan Sheria ya ndoa. Kifungu cha 114 cha Sheria ya ndoa kwa ujumla kinaeleza misingi ya kuzingatia wakati wa kugawana mali ndoa inapovunjika.

Lakini kifungu hichohicho kifungu kidogo cha 2(b) kinaeleza kwa umahsusi kuwa kitu kikubwa ambacho kinapaswa kuzingatiwa wakati wa kugawana mali ni mchango wa kila mwanandoa katika kupatikana kwa mali husika. Yaani ni swali la mwanandoa amechangia nini mpaka hii mali imepatikana.

Tafsiri ya mahakama kuhusu mchango wa mwanandoa katika kupatikana mali ni pamoja na mchango wa pesa, mchango wa kazi(nguvu), pia kazi za nyumbani ambazo mara nyingi hufanywa na mwanamke kama kufua, kupika, kulea watoto, kutunza nyumba nazo zinahesabika ni mchango katika kupatikana mali ambazo zitachumwa na mwanaume moja kwa moja huko kazini anakoenda.

Hii ni tafsiri katika rufaa namba 9 ya 1983, TLR 32 katika kesi maarufu ya Bi Hawa, ikifuatiwa na utitiri wa tafsiri nyingi kama hizo kutoka mahakama kuu na ya rufaa. Huu ndio msimamo wa sheria na haya tumeyarudia mara nyingi.

Swali kuu la mada ni ikiwa aliyeleta chokochoko mpaka ndoa kuvunjika kama naye anastahili kupata mgao wa mali, au asipate kabisa kwakuwa ndiye aliyeleta ugomvi, au apate kidogo.

Mahakama kupitia kesi ya ROBERT ARANJO v ZENA MWIJUMA ( ) [1985] TZHC 5; (14 March 1985); 1984 TLR 7 (TZHC) itatujibia swali hili. Katika kesi hii mkata rufaa ambaye ni mwanandoa ndugu Robert Aranjo alikata rufaa mahakama kuu ikiilalamikia mahakama ya mwanzo na ya wilaya kwa kumpatia mke wake robo ya mali kama mgao wake wakati mwananmke huyohuyo ndiye aliyesababisha ndoa kuvunjika baada ya kuamua kuondoka mwenyewe nyumbani kwasababu anazozijua yeye.

Kwahiyo ndugu Robert aliamini kuwa mwanamke huyo hastahili mali aliyopewa kwakuwa yeye ndiye sababu ya kuvunjika kwa ndoa. Jaji Maina(kama alivyokuwa), alitoa uamuzi kuwa suala la nani amesababisha ndoa kuvunjika halina uhusiano wowote na suala la nani anatakiwa kupata nini.

Alisema kuwa katika mambo yanayozingatiwa wakati wa kugawana mali pale ndoa inapovunjika swali la nani amesababisha ndoa ivunjike halina nafasi.

Alisema kinachozingatiwa na kuangaliwa ni kile kilichoelezwa katika kifungu cha 114 cha Sheria ya ndoa ambacho ni pamoja na mchango wa mwanandoa katika kupatikana kwa kila mali husika. Kwahiyo kwa wale waliotaka kujua kuhusu hatima ya waanzilishi wa chokochoko katika ndoa basi hili liko hivi.

Suala la nani ameanzisha ugomvi haliangaliwi wakati wa kugawana mali. Aidha, suala hili linaweza kuangaliwa katika mazingira mengine kwa mfano zinapokuwa zinajadiliwa sababu zilizopelekea ndoa kuvunjika, na katika masuala ya fidia kwa mwanandoa, lakini si katika kugawana mali. Kwahiyo hivi ndivyo ilivyo.
 
shungurui

shungurui

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2008
Messages
3,013
Points
2,000
shungurui

shungurui

JF-Expert Member
Joined Sep 1, 2008
3,013 2,000
Shukrani kwa darasa, umelitoa wakati muafaka kabisa, je nini inatokea endapo mwanandoa mmoja amefariki mgawanyo utazingatia vigezo hivyo hivyo?
 
K

kigogo warioba

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Messages
4,086
Points
2,000
K

kigogo warioba

JF-Expert Member
Joined Jul 11, 2015
4,086 2,000
je kama mwanamke kadangaywa ili tugawane ili akaanzishe maisha na bwana mwingine, Ila kaficha kueleza na chanzo cha ndoa kuvunjika ni yeye, sasa hapo tukigawana sawa hio sheria haioni kama haijanitendea haki? na usikute Mali nikechuma Mimi yeye akiwa nyumbani na watoto!
 
K

kinyama nje

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Messages
1,712
Points
2,000
Age
53
K

kinyama nje

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2017
1,712 2,000
Kuna mtu alishinda kesi
Kwa kauli ''nimejenga nikiwa nae siku jenga nae hizi ni kauli mbili tofauti?
 
K

kinyama nje

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2017
Messages
1,712
Points
2,000
Age
53
K

kinyama nje

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2017
1,712 2,000
Kuna mtu alishinda kesi
Kwa kauli ''nimejenga nikiwa nae siku jenga nae hizi ni kauli mbili tofauti?
 
tozi25

tozi25

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2015
Messages
5,336
Points
2,000
tozi25

tozi25

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2015
5,336 2,000
Tafsiri ya mahakama kuhusu mchango wa mwanandoa katika kupatikana mali ni pamoja na mchango wa pesa, mchango wa kazi(nguvu), pia kazi za nyumbani ambazo mara nyingi hufanywa na mwanamke kama kufua, kupika, kulea watoto, kutunza nyumba nazo zinahesabika ni mchango katika kupatikana mali ambazo zitachumwa na mwanaume moja kwa moja huko kazini anakoenda.
1) Jee ikiwa mume ameajiri house girl hapo hukumu itakuwaje?
2) Ikiwa mume/mke amejenga kabla ya ndoa itakuwaje?
3) Mali zimeandikwa kwa majina ya watoto hapa itakuwaje?
4) Mume/Mke ana deni benki hapa napo inakuwaje?
5) Ndoa ya miaka mingapi inayo ruhusu mke na mume kugawana mali?


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
nkumbison

nkumbison

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2013
Messages
896
Points
1,000
nkumbison

nkumbison

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2013
896 1,000
Asante Mkuu..
Mada ni nzuri na inamsaada mkubwa.

1. Ikiwa mwanamke kaamua kuondoka kabeba na viombo, je mumewe akifariki bado ana nafasi ya kurithi alivyoviacha.?

2. Ikiwa mke alinunua kiwanja akafa mumewe akakijenga, na hawakua na watoto, mume akifa hiyo nyumba itarithiwa na ndugu wa upande upi?

3. Na kama mmoja wa wanaondoa aliondoka kwa hiyari yake mwenzake akaamua kuuza mali yote. Je hapo kuna kesi?
 

Forum statistics

Threads 1,295,922
Members 498,479
Posts 31,228,141
Top