Je, Mwamkinga Auction Mart wako juu ya sheria?

Je, Mwamkinga Auction Mart wako juu ya sheria?

Joined
Apr 5, 2014
Posts
39
Reaction score
8
Hawa jamaa inaonekana wamepewa tenda na Jiji la Dar, bila kukubaliana mipaka ya kazi au kwa kujisahaulisha ili kuweza kupitisha mambo yao ndani yake.

Tamko la mkuu wa mkoa wa Dar MECK SADIKI, lililotolewa mwanzoni mwa mwaka huu, ni marufuku kwa kampuni yeyote ya auction mart kuvuta kwa brake down gari ya mtu bila ya ridhaa yake, maana yake ni nini kwamba kwa gari nzima, itakayokutwa na kosa lazima mwenye gari apatikane, aelezwe kosa lake then aelekezwe namna ya kulipa faini ktk ofisi ya jiji kwa kosa alilolitenda, akikaidi gari ifungwe ktk tairi na nyororo na si kuvutwa kwa brake down, isipokuwa ni kwa ridhaa ya mwenye gari.

Sasa basi hawa MWAMKINGA AUCTION MART, wanachokifanya wanachukua polisi, na brake down wakikuta gari, bajaji, wanavuta bila ya kuhusisha mwenye gari, mwenyekiti wa mtaa, wala diwani JE KIBURI HIKI WANAPATA WAPI?hawatoi taarifa yoyote kama wanaiba ila wanajiamini sababu wanakuwa na polisi waliojikoki kama wanaenda vitani bunduki, mabomu ya machozi yaani wamejiandaa.

Tumesikia jana walikuwa Msasani na leo wamekuja kwetu mabibo na wataendelea ktka maeneo mengine, tafadhali mnaohusika mlifanyie kazi hili kwani inaonekan ni dili yao ya kujipatia fedha haramu, ukifika TAMESA wanakohifadhi magari hayo unaambiwa ukalipe 45,000/= jiji, hlf urudi hapo ofisin kwao ulipe 105,000/= ya brake down na ukamataji, ukishindwa kuito siku hiyo kila inapoendelea kukaa ktk yard yao utalipia 29,000/= kila siku.

Swali kwa jiji
Je, hawa watu mnajua wanachokifanya huku kwetu na je ndicho mlichokubaliana ktk kutuumiza watanzania kwa kutuwekea magharama makubwa ili hali hamjatuandalia maeneo rasmi ya kuegesha magari wala bajaji'?'

Pili, mh mkuu wa mkoa mmetengua kauli yake kwamba mtaendelea kuvuta kwa brake down kwasababu mna pesa za kulipa gari za watu mtakazoharibu wakati wa uvutaji?

Tatu,hamshirikishi viongozi wa mitaa ili muweze kujipatia fedha haramu bila kipingamizi kwa watu mliokubaliana kutafuta nao pesa km mnavyokua mmejipanga polisi wanaoacha kazi ya kukamata wezi, wenye magari ya brake down, na nyie mwamkinga tu.

Wahuskia fanyieni kazi hili kabla hatujachoka na hii adha, tamesa gari zimejaa kama yard ya kuuza magari, wenye magari yao wanatafuta bila kujua yaliko kumbe wao wameyavuta bila taarifa wala kuacha barua ya ukamataji wao ili ujue mali yako ilipo.tafadhali.
 
wizi wa mchana mchana.... nchi ishauuzwa hii

Nimekutana nao leo wanavizia watu wanaotoka Bank. Ujambazi wa mabenki unarudi sasa hivi (mtasikia tu). Na police wanawalea. Hii ni kwa Kova moja kwa moja.

Halafu hawana risiti za serikali (TRA mnalo) (janga jingine hili). Leo walinikuta vizuri, siku nyingine watasikia mlio wa bastola nikiona wanavizia mtu Bank.

Nimewasilisha ishi kwa wazee wa nchi, watawashughulikia!
 
Hii nchi itafika mahali kila mtu atamiliki silaha, maana uonevu umezidi mno.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Lkn hawa jamaa wanapewa kiburi na watu fulani jiji wala sio bure!lakini kamanda IGP Mangu mtendaji mahiri ndani ya jeshi, sina hakika kama anafahamu wanachokifanya askari wake wa polisi, sina imani kama wamekosa kabisa kazi za msingi za kupangiwa wakafanye kwa ulinzi na usalama wa mtanzania, badala yake wanachukua masilaha na mabomu ya machozi kwaajili ya kuwalinda hawa wazee wa MWAMKINGA wanapokuja kutudhurumu watanzania.KWA MARA NYINGINE TUNAOMBA TENA MNAOHUSIKA FANYIENI KAZI HILI ASUBUHI HII NIMEONA WANATEGEA KUFUNGA GARI YA MTU HAPA MAGOMENI HOSPITALI, WAKIDAI KAEGESHA BARABARANI ILI HALI KUNA STK NYINGI ZIMEPAKI PALE NA NI PARKING KBS YA JIJI JIRANI NA TANESCO KWA WANAOPAFAHAMU,
 
jiulizeni huyo mwamkinga ni nani?????ni bosi mmoja wa usalama ndo mwenye hiyo kampuni na anaitwa hivyo hivyo mwamkinga.hao jamaa ni kiburi sana kwa kweli
 
Unajua siku mmoja wao akipigwa paaa ya mguu hatarudia
 
Back
Top Bottom