Je, mwamba wako ni nani?

Je, mwamba wako ni nani?

Tetengo

Member
Joined
Jan 21, 2023
Posts
50
Reaction score
23
Mwamba ni jiwe kubwa ambalo limekaa imara bila kutikisika.MTU awaye yote akiwa juu ya mwamba anaweza kujilinda juu ya mafuriko kutegemea na ukubwa na urefu kwenda juu.
Pia ajengaye juu ya mwamba anakuwa yuko salama sana dhidi ya mvua kubwa na za Mara kwa Mara kuliko ajengaye juu ya mchanga.

Zaburi 40:1
Nalimngoja BWANA kwa saburi, Akaniinamia akakisikia kilio changu.

Zaburi 40:2
Akanipandisha toka shimo la uharibifu, Toka udongo wa utelezi; Akaisimamisha miguu yangu mwambani, Akaziimarisha hatua zangu.

Mungu wetu amekuwa akitupigania katika changamoto nyingi,akitupandisha toka kwenye uharibifu,katika mambo yanayotuangusha,lakini baada ya kutoka huko tunamsahau!.
Tukipatwa na mambo mengine mazito tunaanza kutafuta miamba mingine tunasahau ya kwamba yupo aliyetuumba,anatupenda na kutupigania mambo yote.

Chunga sana juu ya mwamba unaosimama kwako!

Wengine hugeukia hirizi ambazo zimetokana na uumbaji wa Yehova kuwa Mwamba wao,wengine wapenzi wa kuwategemea na kuwatumaini kiasi cha kuwa tayari kutokuhudhuria ibada ili akaonane naye,wengine mabosi wao,wengine biashara zao.


Zaburi 40:4
Heri aliyemfanya BWANA kuwa tumaini lake, <br>Wala hakuwaelekea wenye kiburi, Wala hao wanaogeukia uongo.

Mkumbuke MWAMBA wako!

Kumbukumbu la Torati 32:18
Humkumbuki Mwamba aliyekuzaa, Mungu aliyekuzaa umemsahau.

Yupo Mungu aliye muumbaji wa vyote,tunapaswa kumtumaini na kumwamini yeye peke take.

Mwamba upo mmoja tu ambao nakupendekezea usimame kwako.

1 Samweli 2:2
Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA; Kwa maana hakuna ye yote ila wewe, Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.

Mungu akubariki unapotafakari ujumbe huu na karibu kwa kuchangia mada.


192-Mwamba Wenye Imara
Rock Of Ages (SDA300)
Doh ni C

Mwamba wenye imara Kwako nitajificha!
Maji haya na damu Yaliyotoka humu,
Hunisafi na dhambi, Hunifanya mshindi.

Kwa kazi zote pia Sitimizi sheria.
Nijapofanya bidii, Nikilia na kudhii,
Hayaishi makosa; Ndiwe wa kuokoa.

Sina cha mkononi, Naja msalabani;
Nili tupu, nivike; Ni mnyonge, nishike;
Nili mchafu naja, Nioshe nisijafa.

Nikungojapo chini, Na kwenda kaburini;
Nipaapo mbinguni, Na kukwona enzini,
Roho yangu na iwe Rahani mwako wewe.
 
Back
Top Bottom