The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 10,959
- 13,428
Dini zinasema kuwa Mungu anaishi mbinguni. Hapo hapo, zinajipiga mtama na kusema kuwa Mungu yuko kila mahali. Nyingine zinasema eti Mungu ametuumba kwa mfano wake!
Je mashonga, majambazi, chawa, madikteta, wauaji, wanyang'anyi, na wabaya wote, nao wameumbwa kwa mfano wa Mungu? Dini zinasema eti kila kitu ni mali ya Mungu. Je na shetani ni mali ya Mungu? J
e kwanini Mungu aliumba shetani na 'akampa' mamlaka ya kuharibu wanadamu? Je Mungu anafaidikaje na uwepo wa shetani? Mbona shetani ana wafuasi wengi kuliko Mungu?
Je kwanini Mungu akiguswa vibaya hata kutukanwa, anatetewa na binadamu na sio ajitetee? Kwanini 'kazi' za Mungu zinaendeshwa kwa michango ya binadamu kama kweli tunaambiwa ni tajiri kuliko tajiri yeyote na ndiye mwenye kumilki kila kitu? Je kwanini, kama kweli ni yeye, Mungu anapenda sana vitisho?