Davidmmarista
JF-Expert Member
- Apr 11, 2024
- 2,766
- 5,677
Wadau Nina maswali machache hapa ningependa kufahamu:
1. Chanzo cha Dini: Ilianzia Wapi?
Je, dini ziliundwa na Mungu au binadamu? Je, zilitokea lini na kwa nini kila tamaduni ina dini yake? Kabla ya Uyahudi, Ukristo na Uislamu watu waliamini nini?
2. Kabla ya Yesu (na Mitume), Watu Waliamini Nini?
Biblia na Qur’an zimekuja kwa njia ya mitume, lakini kabla ya hao watu waliishi vipi kiimani? Walikuwa na dini? Walimjua Mungu vipi?
3. Sadaka Zinakwenda Kwa Mungu au Kwa Binadamu?
Tunambiwa tukitoa sadaka tumempa Mungu. Lakini pesa hizo zinabaki kanisani au kwa viongozi wa dini. Je, hizo huduma ni Mungu? Sadaka kwa miamala ya simu au benki bado ni tendo la kiroho au limekuwa biashara?
4. Maandiko Yameandikwa na Binadamu Kwa Nini Tuyachukulie Kama Neno la Mungu?
Hakuna kitabu kilicholetwa na Mungu mwenyewe. Vyote vimeandikwa na wanadamu. Je, kwa nini tuyaamini kama Neno la Mungu? Nani alithibitisha Roho Mtakatifu aliwaongoza?
5. Kwa Nini Hofu ya Moto wa Milele Hutumika Kwenye Dini?
Tunaambiwa tukikosea tutachomwa moto. Je, ni nani alishawahi kwenda huko na kurudi kutuambia? Je, hofu ni njia sahihi ya kuendesha imani? Jehanamu ipo wapi? Na mbona dini hutufundisha zaidi hofu badala ya upendo?
6. Mambo Kama Kurusha Mawe Kupiga Shetani Maana Gani Halisi?
Watu hufanya vitendo kama kurusha mawe wakisema wanampiga shetani. Je, haya ni maonyesho ya kiimani au ni ishara ya kupinga uovu? Je, tuna uhakika haya mambo si maigizo ya kiroho?
7. Je, Dini Zinajenga Hofu Badala ya Maarifa?
Wengi hushindwa kuuliza maswali ya msingi kwa hofu ya “kukufuru.” Lakini swali ni hili: Imani inapaswa kujengwa kwa maarifa au kwa hofu?
Kiranga