Je mnajuwa chimbuko la mgogoro nyamongo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je mnajuwa chimbuko la mgogoro nyamongo?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by TUNTEMEKE, May 23, 2011.

 1. TUNTEMEKE

  TUNTEMEKE JF-Expert Member

  #1
  May 23, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 4,582
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  CHIMBUKO LAM MGOGORO KATI YA MWEKEZAJI NA VIJIJI VINAVYOZUNGUKA MGODI WA NYAMONGO NI HII HAPA Barrick haina kitalu(MINING lICENCE) hata kimoja kinachochimbwa dhahabu hapo Nyamongo hadi sasa. Maeneo yote yanayochimbwa dhahabu ni vitalu vya vijiji vya Nyangoto, Nyamwaga, Genkuru, Kerende na Kewanja, na cha Ndg Chacha Msabi maarufu kama KengÂ’anya Enterprises.

  Vijiji hivyo vilikabidhi hati za vitalu vyao vya kuchimba dhahabu kwa kampuni ya Afrika Mashariki Gold Mines ambayo iliuza kwa kampuni ya Placer Dome ambayo nayo iliuza kwa mwekezaji wa sasa Barrick Africa Gold inayomiliki mgodi wa North Mara Gold Mine Limited.

  Kulingana na makubaliano hayo Barrick ilipaswa kuunda mfuko wa dhamana (Trust Fund) ambao ungewekwa fedha hizo kwa sababu ni nyingi na kwamba kampuni nayo ingechangia asilimia moja kwa kila asilimia moja inayopata ya vijiji.

  Miongoni mwa masharti ya vijiji ambayo Barrick iliyakubali ili ikabidhiwe hati za vitalu vyao ni kila kijiji na KengÂ’anya kuteua mwakilishi mmoja mmoja atakayewawakili sha kwenye UCHIMBAJI na KUKAGUA mahesabu kuhakikisha HAVIDHURUMIWI na Barrick.

  WANA NYAMONGO WANACHODAI NI HIKI: hadi leo hii pamoja na Barrick kuchukua hati za vijiji na kuchimba tangu 2004 haijaanzisha, haijaunda wala kusajili mfuko wa dhamana na kwa maana hiyo Barrick haijawahi kuvilipa vijiji hivyo chochote kulingana na mkataba uliowezesha ipate kibali cha kuchimba eneo hilo.

  HIVYO Barrick inatumia hati za vijiji kuchimba dhahabu lakini hailipi asilimia moja kama ilivyokubaliwa na hakuna anayefanya chochote badala yake Mkuu wa Wilaya ya Tarime (KADA WA CCM), anavilazimisha vijiji eti vipokee dola za Marekani 100,000 ili viingie mkataba mwingine IACHE ULE WA MWANZO na Barrick na kuacha madai yao yote!


  KISHA WanaNYAMONGO WAKIDAI HAKI YAO WANAPIGWA RISASI

  WanaCCM SEMENI SASA kuwa WanaNYAMONGO WANADHURUMIWA AU HAWADHURUMIWI?
   
Loading...