Je mke mmoja anatosha kweli tuweni wawazi?

Anatosha,kwa hakika anatosha,jana nilitimiza miaka kumi na mke wangu.yeye pekee alinitosha kwa miaka sita ya uchumba,na minne ya ndoa!amenitosha kwa miaka kumi,atanitosha kwa miaka kumi mingine ijayo,na mingine na mingine mpaka itakapoitwa milele

hivi kumbe miaka ya uchumba inahesabiwa?? basi wengine i wazee dah! manake 11 ya ndoa tu ukieka saba ya uchumba ni 18 mama yangu silver jubilee hii hapa dah!
 
mke mmoja anatosha,si lazima kwa mwanaume kila siku kula nyumbani ukizidiwa sana nenda kale hotelini, ila kuongeza wake wengine mnh nahisi ni matatizo.
 
Tunaongozwa na unafiki. Fanya utafiti uone ni wanaume wangapi wanaotakiwa kuwa na mke mmoja tu wanatoka nje ya ndoa? Ukilijua hilo utafahamu kuwa wanatumia vinywa lakini matendo yao yanaeleza. Ni mabingwa wa kutumia vinywa.
 
Naomba kudandia mada,swali juu ya swali,kwa mnaosema mke mmoja hatoshi,je katika hao kadhaa utakaokua nao( namaanisha wake wa kuwaoa sio vimada vya nje) kuna utakayempenda zaidi? au upendo utaugawa sawa kwa sawa? hebu nisaidieni hapo
 
1 Anatosha kaka yangu, ukiendekeza hata 10 hawatakutosha. Sulemani alizidi 300 mwisho wa siku akaishia kusema yote ni batili.
 
Hakika tusiwe wa wanafiki kwa mazingira aliyotaja huyu ndugu hatoshi. na amini hili hata wanawake wanalijua ndio maana wengine wanajiuza ili kutoisheleza hamu na shauku ya mume eti. Kuwa na mke mmoja ni imani na tena ni Ukiristo maana sidhani kama kuna dini nyingine inasisitiza mke mmoja chini ya jua.

We ndugu unajua kuna dini ngapi chini ya jua? Hebu fuatilia ujue wayahudi, wabudha, na wahindu imani zao zinasemaje. Usikurupuke na assumptions za ajabu ndugu!
 
Mh!hata tukisema anatosha haisaidii na tukisema hatoshi haisaidii.wanadamu tumezidi tamaa.tunashindwa hata na ndege aina ya njiwa.Mungu alipoiumba Dunia alimuumba Adam na Eva .na akasema mkaijaze Dunia.alijua Eva atabeba mimba na anazaa watoto na hakuona umuhimu wa kumwongezea adam mwanamke mwingine.sisi wanadamu tunatamaa sana.
 
Mmoja hatoshi hebu tuwe serious....binafsi watatu wangenitosha!..ila ndio hivyo tena tunakomaa na mmoja...
 
Katika shida na raha...Si uliapa mbele za watu? Huo muda ndio unapaswa uwe karibu na mke wako, si kuenda vimada au kijipooza kwa nyumba ndogo. C-section, kushonwa kizazi, kushonwa ulikochanika baada ya kujifungua, kazi za kulea mtoto baada ya kujifunza pia yataka moyo na nguvu ya zaidi ya mtu mmoja. Jaribu kuwa mume mwema kwa muda huo badala ya kijifikiria mwenyewe. Akipona utapewa mapenzi motomoto.


Sasa hiyo ya kijifungua tu at least unajua ina muda wake halafu mambo yata improve. Sasa akiugua kansa je? Utamuacha kabisa? Ikishindikana tumia Revola. Nyie ndo mnaooa kwa ajili ya kufuliwa, kupikiwa, na ngono.


Naomba niulize, wewe mambo yako yakiwa hayaendi vizuri kazini au kibaruani na pesa zikapungua utaona sawa mkeo atoke nje kutafuta mwanamme mwingine wa kutimiza mahitaji yake ya kifedha? If not , why?
 
Mke akibeba mimba na kujifungua unaweza kumsubiri hadi miezi mitatu ndiyo muendelee na tendo la ndoa.Kama umeoa mwanamke ambaye akibeba mimba anakuwa kwenye bed rest (mapumziko) mpaka ajifungue ndio kabisa itabidi uvumilie mpaka ajifungue na amalize miezi angalau miwili, na kama ameshonewa nyuzi kwenye cervix ili kuzuia ujauzito kutoka vivyo hivyo utajihitaji kumpa muda wa kutosha ili kukuza kiumbe vizuri (namaanisha kwa wanawake wale ambao kizazi chao hakina uwezo wa kubeba kiumbe).

Je Hiki ndiyo chanzo cha baadhi ya wanaume kutoka nje ya ndoa?Je kuoa mwanamke zaidi ya mmoja kama Daudi na seleman ndiyo itakuwa suluhisho?

Kiukweli mimi binafsi nina mke mmoja na nina uwezo kufanya tendo la ndoa hata kila siku hivyo changamoto hii hunikumba. Siku zote hujitahidi kufanya kazi muda mwingi ili kuweza kupotezea tamaa za ngono hivyo hulazimika kuchelewa kazini ili nikifika nyumbani nakula chakula na kulala.

Je wana JF wenzangu mnakabilianaje na changamoto hii? Hata kina dada mnaweza kutupa ujanja wa jinsi ya kukabiliana na changamoto hii.

Kibaolojia tunatofautiana sana, kuna wengine mwanamke mmoja anamtosha sana na angependa asaidiwe ikiwezekana (kama mwanamke ana hamu sana) ila kwa wengine wanawake wawili, watatu, wanne hata wengine wanawake 10. inategemea mwanamke aliyenaye anaridhika vipi.

Cha muhimu ni wewe mwenyewe kujiangalia na kumuangalia uliyenaye! mnafanana
 
Back
Top Bottom