Je,Mkapa.Kikwete,Lowassa, Yona nk walitoa Machozi ya Mamba Kifo cha Nyerere? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je,Mkapa.Kikwete,Lowassa, Yona nk walitoa Machozi ya Mamba Kifo cha Nyerere?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, Nov 10, 2011.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Waingereza wana msemo, "crocodile tears": machozi ya mamba. Mamba anapokula minofu ya mnyama aliyemwuuwa hulia, hutoa machozi. Machozi haya siyo ya majonzi au huzuni la hasha, ni machozi ya furaha na shangwe ya ushindi. Tukirudi nyuma wakati ule mwl. Nyerere angali hai viongozi wengi walijifanya "walokole" kwa itikadi na maadili ya chama-CCM ( mfano, sitopokea wa kutoa rushwa,rushwa kwangu ni mwiko; sijui, labda mwiko wa kupakulia na kujiandalia chakula). Mara baada ya kifo cha Mwl. Nyerere ndipo hata yule kipenzi cha mwalimu, W. Mkapa akawa dhahiri sawa na Lowassa, sawa na Kikwete. Nyangenyange wote hufanana na huruka kwa mstari mmoja. Na katika familia ya kambale, wote wanashrafa baba, mama, dada,kaka nk. huwezi kuwatofautisha.

  Watu hawa ni miongoni mwa Watanganyika waliotoa machozi wakimlilia Hayati Mwl. Nyerere. Kpt. Komba na wasanii wa JWTZ wakawaongoza kumlilia mwalimu. Hao wote, wakatoa salaam zao za rambirambi kila mmoja kwa wakati wake wakisema tutamuenzi Mwalimu, kumbe visogoni waliwalamba watanganyika. Leo hii, watu hao hawataki kabisa kulishika na kulienzi japo jambo moja zuri la Mwl. Nyerere. Utajiri wao unatisha, wote wamewahi kudiriki kumiliki vinu vya kufua umeme. Wawili kati yao wamekwama kiasi,mmoja kaweza. Utajiri wao umepatikanai kwa gharama za uhai na maisha ya watanganyika kuanzia walipokuwa madarakani hadi vizazi kadhaa vijavyo.

  Watoto wa watanganyika wanapata utapiamlo, kwashiakoo, kwa kugharamia utajiri wa watu hawa. Shule, hospitali hazina vifaa wala wataalam kwa gharama za utajiri wa watu hawa na wenzao kadhaa ndani ya CCM na serikali yake.

  Ndipo tunaposema, tulipomlilia Mwl. Nyerere na hata tunapomkumbuka'machozi' yetu hayakufanana na wala hayatafanana. Mjane wa Mwalim; familia yake;na watanganyika wanyonge tulilia tofauti na watu hao na mafisadi woote!
   
 2. J

  Jujuman JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2011
  Joined: Dec 7, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  avata,
  Unapozungumzia matatizo na shida zinazowapata watoto wa Watanganyika: Utapiamlo, Malaria nk. Elimu duni, majengo ya shule na vifaa vya ufundishiaji hakuna au ni duni kuliko na Waheshimiwa hao na wengine kadhaa wamejirundikia lukuki ya utajiri!! Hawana Haya wala hawajui vibaya,Hawana fiikra wala hisia, dhahir kilio cha ni kilio cha Mamba!
  Dawa ni nini/gani tutumie kupambana na Mafisi hawa? Wakati fulani nlitegemea Vyama vya upinzani vingetuletea suluhisho,kwa bahati mbaya au nzuri inategemea mtazamo wako CUF wameshamaliza kitabu chao, hawana jipya tena. Nikategemea CHADEMA baada yakupandisha namba ya wawakilishi Bungeni na Mgombea urais wao kuvuna 26% yakura za 2010 ingewasaidia kujipanga mapema kwa matumaini ya kufanya vizuri zaidi au hata kulazimisha Serekali ya mseto kama si kuchukua serekali kamili.Badala yake CHADEMA wanalazimisha yasiyowezekana hatua ndogo waliopiga imewalevya! Na vyama vilivyobaki unajua hata majina havina, hivyo lazima itafutwe dawa ya kuwakomboa watoto wa Tanganyika.
  Baba wa taifa aliseme "IT CAN BE DONE PLAY YOUR PART".
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Kulia? Watalia lakini wote ni wanafiki? angalia walivyoifanya nchi hii a big U-TURN; Nani sasa hivi anajali mtu wa kawaida?

  Angalia mabomu Mbeya kunyamazisha Wamachinga, Unadhani wakati wa Nyerere hayo yangetokea? Kiongozi angetumwa kwanza kusikiliza matatizo yao.

  Hao wote walikuwa wanafikiria Matumbo yao; kuwa sasa nitakuwa Rais; sasa nitaibadilisha CCM kuwa CHama CHa Malafi

  WEZI WOTE but wawe waangalifu the Income GAP hiyo kubwa itawatoa Majumbani Mwao na Chupi kama Rais wa Ivory Coast au kaka Gadhaffi au Wagonjwa kama Rais wa Egypt Mubarak == UTAMU WA MADARAKA Mmmm
   
Loading...