Je Mh.Kikwete alishinda kihalali 2005?

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Shahada za kura zachomwa moto

na Asha Bani

SHAHADA za kupigia kura zinazokadiriwa kufikia milioni moja, zimeteketezwa kwa kuchomwa moto katika mazingira ya kutatanisha jijini Dar es Salaam.

Shahada hizo ziliteketezwa na watu wasiojulikana ndani ya eneo la Bohari Kuu inayohusika na utunzaji wa nyara za serikali, iliyoko eneo la Keko, wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya shahada hizo zilizoshuhudiwa na waandishi wa habari wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, zilikuwa za wapiga kura wa Mkoa Morogoro, Tanga, Pwani na Dar es Salaam za mwaka 2005 na 2008.

Shahada zilizoandikishwa jijini Dar es Salaam, nyingi zimetoka katika maeneo ya Manzese na Mwananyamala.

Hadi sasa haijulikani namna gani shahada hizo za kupigia kura zimekusanywa kwa wingi na kupelekwa kuteketezwa ndani ya eneo la Bohari Kuu ya Serikali.

Kuwapo kwa shahada hizo ndani ya Bohari Kuu na mpango wa kutaka kuziteketeza, kuligunduliwa na viongozi wa CUF ambao walipata tetesi kuanzia juzi.

Inasemekana kuwa, shahada hizo ambazo zinaonyesha picha na majina ya wapiga kura mbalimbali nchini, ziliteketezwa juzi, lakini baadhi yake zilibaki ndipo Profesa Lipumba aliwakusanya waandishi wa habari na kuingia nao kwenye bohari hiyo kwa siri kwa kutumia gari yake yenye vioo vya kiza.

Mara baada ya kushuka ndani ya eneo hilo la bohari, Profesa Lipumba aliwaongoza waandishi wa habari hadi lilipokuwa lundo hilo la shahada na kuanza kuzichambua moja baada ya nyingine na kisha kuzifunga kwa mafungu kwenye mifuko ya plastiki na kuzipakia kwenye gari lake.

Wakati Profesa Lipumba aliyeongozana pia na baadhi ya wabunge na viongozi wa CUF wakichambua shahada hizo, wafanyakazi wa Bohari hawakujitokeza, lakini baada ya kuanza kuzungumza na waandishi wa habari juu ya tukio hilo, baadhi yao walijitokeza katika eneo la tukio na kushangaa.

Akizungumzia tukio hilo ndani ya eneo hilo la Bohari Kuu, Profesa Lipumba, alisema tukio hilo linadhihirisha mbinu chafu zikifanywa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya uratibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

“Angalieni kadi hizi, haya ndiyo matunda ya kutokuwa na Tume Huru ya Uchaguzi, kila kukicha ni wizi tu hakuna uwazi wala ukweli,” alisema Lipumba huku akionyesha mabaki ya shahada zilizoungua.

Alisema vitambulisho hivyo vinatumika katika kupiga kura za utapeli na viongozi mbalimbali wa CCM wanaovinunua kwa ajili ya kurubuni na kuvuruga uchaguzi.

Alibainisha kuwa, kamwe demokrasia haiwezi kuendelea kama hila za kupata idadi kubwa ya hesabu za kura hizo zinazofanywa na CCM hazitakomeshwa.

Aliongeza kuwa, bohari ni sehemu ya kutunzia nyara za serikali, hivyo kukutwa kwa shahada hizo zikichomwa moto katika eneo hilo ni ushahidi kuwa serikali inahusika.

Alisema serikali inayopora haki ya mpiga kura kwa kupata ushindi kwa njia isiyo halali, haiwezi kuwaletea maendeleo wananchi na ndivyo tuonavyo hakuna maendeleo zaid ya kukwiba na ufisadi kulindwa.

Naye Mbunge wa Michewani, Shoka Hamisi Shoka, alisema hila hizo za kuwepo kwa shahada bandia, aliwahi kuzizungumzia bungeni kwamba CCM inahusika na ununuzi wa shahada za wapiga kura, lakini walipinga.

Alisema wakati akiwawasilisha hoja hiyo bungeni, Spika wa Bunge, Samuel Sitta, alipinga kwa nguvu hoja hiyo na kumtaka atoe ushahidi wa hicho anachokisema.

“CCM walinitolea macho, Spika wa Bunge Samuel Sitta alinitaka kutoa ushahidi wa kununua shahada za kura, na huo ndiyo ushahidi mmojawapo.

“Bohari ni mali ya serikali ambayo inaongozwa na CCM, kutokana na suala hili wanahusika moja kwa moja na ununuzi wa kura,” alisema Shoka.

Naye Mkurugenzi wa Ulinzi wa CUF, Mazee Rajabu Mazee, alisema siku zote CUF wamekuwa wakilalamika kutokuwapo kwa tume huru ya uchaguzi, lakini wamekuwa wakipuuzwa.

Alisema tukio la kukutwa shahada hizo zikiteketezwa, kumedhihirisha jambo hilo ambalo watu walikuwa hawaamini.

“Siku za mwizi arobaini, CCM walizoea kuiba na leo ndiyo wamefikia tamati, shahada hizi ni nyingi sana, zaidi ya milioni moja. Ni Watanzania wangapi wametangaziwa kiongozi asiye chaguo lao?” alihoji Mazee.

Akizungumzia sakata hilo kwa njia ya simu jana, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi (NEC), Rajabu Kiravu, alisema ofisi yake haihusiki kwa aina yoyote ya uchomaji huo wa shahada za kupigia kura.

Hata hivyo, Kiravu alieleza kushangazwa na namna ujumbe wa Profesa Lipumba na waandishi wa habari walivyoweza kuingia katika eneo la tukio.

“Ofisi yangu haihusiki na uchomaji huo, kwanza mliingiaje maeneo ya Bohari?” alihoji Kiravu
 
5904d1252597333-je-mh-kikwete-alishinda-kihalali-2005-alert-kadikura.jpg


Kaaaziii kweli kweli.
 

Attachments

  • kadikura.jpg
    kadikura.jpg
    10.1 KB · Views: 105
Mkuu

Hakuna nakala hata moja ya hizo shahada iliyopatikana kama kuweka msisitizo wa ushahidi...?
Si unaelewa unapochoma makalatasi mengi kwa kawaida huwa hayaunguagi yote ,kama kwenye habari ulivyoona Mheshimiwa Lipumba alitinga hapo kama FBI akiwa kwenye gali lenye vioo vyeusi,afu wakaondoka kwa mwendo wa kasi baada ya kukusanya ushahidi kwenye vipolo ,hii ni kesi dhidi ya serikali au tume ya uchaguzi ,japo huyo Kiravu4 ameanza kubabaika na kuruka futi mia,na haswa palipotumika ni pahala patakatifu kwa maana panapomilikiwa na serikali.
Sijui hii aibu serikali wataificha wapi.
 
Hivi kwa matukio kama haya hakuna wana sheria wanaweza kuona kwamba kuna hujuma wakafungua kesi na uchunguzi ukafanywa ? Siku za mwisho za CCM zimefika na jamabo hili nadhani sasa lisimamiwe . Tundu Lissu anaweza kufanya lolote ?Maana mawakili wengi wa Tanzania ni kama Lamwai tu .Kusoma kwingi lakini ujinga ule ule . Serikali inatoa tamko gani ?
 
Hivi kwa matukio kama haya hakuna wana sheria wanaweza kuona kwamba kuna hujuma wakafungua kesi na uchunguzi ukafanywa ? Siku za mwisho za CCM zimefika na jamabo hili nadhani sasa lisimamiwe . Tundu Lissu anaweza kufanya lolote ?Maana mawakili wengi wa Tanzania ni kama Lamwai tu .Kusoma kwingi lakini ujinga ule ule . Serikali inatoa tamko gani ?


Come on Mkuu Lunyungu...mpe Dr Lamwai credit zake....wakati yeye Serikali inamshughulikia Tundu Lissu alikuwa mpiga kura wa kawaida kama wewe na mimi. Michango ya kina Lamwai et al ina nafasi yake kwenye mageuzi ya siasa zetu...kama leo hatuoni basi pengine huko mbeleni.

Wakati mwingine yule anayenza kuongoza msafara sio yule anayewafikisha wasafiri...lakini ni vema tumpe heshima yake japo kwa kuanza.
 
Mimi huwa kila siku ninasema tatizo si wananchi kuichagua CCM, Tatizo ni Tanzania kuwa na tume ya uchaguzi ya CCM. Katiba yetu haitoi uhuru wa kuwa na demokrasia Tanzania kwani kikundi cha watu wachache walioiwahi nchi wanaojiita CCM ndicho kimejimilikisha nchi. Hata siku moja tusitaraji Democracy Tanzania bila ya kuipigania kwa mikono yetu. Nasema mikono yetu kwani maneno matupu hayavunji mfupa, CCM wao wamejikita kwenye propaganda ya "kuvuruga amani" Lakini mvurugaji mkubwa wa Amani ni CCM. Na ninawahakikishia kuwa hawa jamaa wapo Tayari watanzania waangamie ili wao waendelee kuitafuna nchi.
 
Last edited:
Come on Mkuu Lunyungu...mpe Dr Lamwai credit zake....wakati yeye Serikali inamshughulikia Tundu Lissu alikuwa mpiga kura wa kawaida kama wewe na mimi. Michango ya kina Lamwai et al ina nafasi yake kwenye mageuzi ya siasa zetu...kama leo hatuoni basi pengine huko mbeleni.

Wakati mwingine yule anayenza kuongoza msafara sio yule anayewafikisha wasafiri...lakini ni vema tumpe heshima yake japo kwa kuanza.


Yebo Yebo mkuu wangu , mimi na Lamwai tumepigania haki kibao na hata siku Lamwai na genge lake wana amua kumuondoa Tambwe kwenye kugombea muulize Tambwe mimi nilifanya nini .Alinifuata kwangu usiku wa manane mkutano una endelea pale Salvation Army .Bado niko hapa nambana . Kitendo cha Lamwai kuingia CCM na kuanza kuwatukana watu nikiwemo mimi ambaye nimebakia upande wa n dhambi kubwa sawa na ile ya Kaburu kule Kigoma kuwa hadaa wana Chadema . Kwa sasa historia haiwezi kumkumbuka Lamwai na Kaburu kwa mazuri .
 
Yebo Yebo mkuu wangu , mimi na Lamwai tumepigania haki kibao na hata siku Lamwai na genge lake wana amua kumuondoa Tambwe kwenye kugombea muulize Tambwe mimi nilifanya nini .Alinifuata kwangu usiku wa manane mkutano una endelea pale Salvation Army .Bado niko hapa nambana . Kitendo cha Lamwai kuingia CCM na kuanza kuwatukana watu nikiwemo mimi ambaye nimebakia upande wa n dhambi kubwa sawa na ile ya Kaburu kule Kigoma kuwa hadaa wana Chadema . Kwa sasa historia haiwezi kumkumbuka Lamwai na Kaburu kwa mazuri .

point taken
 
Serikali ya CCM inatumia mabilioni kutengeneza shahada za wapiga kura. Halafu inatumia mamilioni mengine kuwanyang'anya kwa nguvu wapiga kura hizo shahada kwa kupitia mabalozi wa nyumba kumi kumi. Wanachota mabilioni kwenye akaunti za EPA kuja kununua zile ambazo wanashindwa kuzikamata kwa nguvu. Inatumia mabilioni mengine kufanya uchaguzi wakati inajua uchaguzi huo ni kutuhadaa sisi Watanzania na wafadhili wa nje kwani mshindi anakuwa ameshapatikana kabla hata ya uchaguzi. Halafu inaingia hasara ya mamilioni kuzikusanya na kuzichoma moto. Halafu inapoteza mabilioni mengine kuwatengenezea hao wapiga kura shahada nyingine ambazo mwisho wa siku watakuja kuzinunua na kuzichoma tena moto.

Bado tuna njia ndefu sana kufikia demokrasi ya kweli. Lipumba angewapeleka hao wafadhili wakajionee wenyewe labda ingesaidia maana bila vitisho vyao hii serikali ya CCM haitaacha haka kamchezo kao.
 
Nadhani kuna umuhimu wa kutumia huu ushahidi kuandaa mkakati utakaowahusisha wote wapenda mageuzi kushiriki ,ni kuanzisha maandamano ya kitaaifa kupinga tume ya uchaguzi kwa sababu hata uchaguzi wa mwezi ujao wa serikali za mitaa utaharibiwa kwani wengi hawatapiga kura,tayari zimeshanunuliwa ,wanatumia umaskini a wanachi na ujinga wao wao kujineemesha kwa vyeo nani aliwambia wanahodhi hii nchi ni yetu wote, nikuandamana nchi nzima tuu labda haki ya Mtanzania itarejeshwa,mbaya sana kunyang'anya haki ya mtu .CCM wanataka nini jamani nia yao nikuteketeza nchi hii ili mradi wao wanabaki madarakani no wonder kila siku kuna magomvi kwenye chama chao
Lakini wanapaswa kujua pia jinsi watanzania ambavyo wamechoka nao ni vipi wafanyakazi wa bohari ya serikali wanaweza wakamwaga siri mpaka Prof Lipumba akaingia kininja kwenye bohari la serikali ha ha ha Serikali ya CCM wataendelea kuumbuka sana mwaka huu
 
Nimefurahia kuona wananchi wamechoka na CCM,sasa hilo ndio moja limejulikana na kukamatiwa,waliotonya habari hiyo bila ya shaka wamo ndani ya CCM kwa maana wamechoka na ukiritimba na sasa inaonekana wameshindwa kuvumilia.
Kila siku nasema hapa kuwa siku hizi siri ni mali na zinanunulika ,hivyo CCM wafanye wafanyayo lakini rupia itapenyezwa ili kupata ukweli kama wao wamenunua shahada na kuzichoma kwa siri ,upinzani umenunua process nzima ya siri yao ,sasa hata akijifungia Kikwete na Pinda basi wajue mmoja wao atauza siri yao kwa bei itakayonunuliwa.
Hivyo nawatangazia wapenzi na wanachama wa CCM kuwa siri zao ni mali au hotcake zinauzika ,ila wajue njia za kuziuza na kama zinanunulika kutokana na uzito wake ,hivyo hivyo wazitayarishe kimaandishi kwa mpangilio wa washiriki ,waamuzi wanaounga mkono ,saa wakati na sehemu kama haitoshi hata vyombo wanavyotumia kukutania ka baiskeli,plate number za magari ,yaani siri itakuwa na bei nzuri kama mambo hayo yatakamilika pamoja na kideo au picha za washirika wa uovu.
Mambo sasa ni mbele kwa mbele tu.
 
Date::9/10/2009NEC yadai CUF wameokota takataka siyo shahada
broken-heart.jpg
Ramadhan Semtawa na Salim Said

SIKU moja baada ya CUF kubaini zoezi la kuchoma kiholela shehena ya shahada za kupigia kura, Tume ya Uchaguzi (NEC) imethibitisha kwamba, imeteketeza zaidi ya kadi 800,000 ambazo zilikuwa ni takataka.

Jana kikosi cha askari wa CUF, maarufu kama Blue Guards, kikiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kilivamia Bohari Kuu ya Serikali na kukuta shahada hizo zikichomwa moto na kufanikiwa kupata baadhi ya kadi.

CUF imedai mpango huo ni hujuma za CCM kwa ajili ya uchaguzi mkuu ujao, lakini mwenyekiti wa NEC, Jaji Lewis Makame alisema jana kwamba shahada zilizoteketezwa ni zile ambazo zilikusanywa wakati wa zoezi la uboreshaji daftari la wapiga kura na hivyo hazihitajiki.

"Jana (juzi) mlivyoniuliza (Mwananchi) niliwaambia ngojeni kuna vitu ni-establish (nifahamu zaidi), nilitaka kujua zimepatikana kwenye ofisi ipi na je, bado ziko hai?"

"Sasa baada ya kuwasiliana na wenzangu makao makuu, maana mimi niko Dodoma, nimethibitisha ni kweli kadi zaidi ya 800,000 ziliteketezwa jana (juzi)."

Hata hivyo, Jaji Makame alifafanua kwamba, shahada hizo za kura zilikusanywa katika mfumo na utaratibu ambao uko wazi baada ya kuanza kwa mpango wa kuboresha daftari la wapigakura.

Mwenyekiti huyo wa NEC alisema CUF imevuruga zoezi hilo la uteketezaji wa kadi hizo kwani lilikuwa likiendelea vizuri.

"Sasa CUF walipovamia na kuondoka na baadhi ya shahada hizo, waliharibu zoezi la uteketazaji ambalo lilikuwa likiendelea vizuri," alisikitika Jaji Makame.

Kuhusu utaratibu wa kuteketeza nyaraka hizo muhimu bila ya kuwepo na ulinzi mzuri, Jaji Makame alisema zoezi hilo lilikuwa la wazi na lilikuwa likijulikana siyo kwamba kulikuwa na usiri wowote.

Mkuu huyo wa NEC aliongeza kwamba shahada hizo zilikuwa ni pamoja na za watu ambao wamehama kutoka eneo moja la nchi kwenda jingine, waliofariki na ambao waliomba kupatiwa mpya.

"Nyingine mtu alitoka labda Muheza, Tanga huko kwenda Nzega, wengine walifariki dunia na wengine walipewa nyingine baada ya zile za kwanza kuwa na matatizo," alifafanua zaidi.

Jaji Makame alimtaka Profesa Lipumba kutumia muda wake kufanya maandalizi ya maana kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa na si kufanya mambo ambayo hayana tija.

"Lipumba ni mtu ambaye namheshimu... kama kuna kitu anafikiri ni kikubwa na ameona kinampa shaka ni vema akawasiliana na NEC kuliko kufanya vitu ambavyo mwisho wa siku anakuwa kapoteza nguvu bure," alisema Jaji Makame.

Naye Lipumba, akizungumza jana makao makuu ya CUF, alitangaza msimamo wa chama hicho kutokuwa na imani na NEC pamoja na sekretarieti yake.

Profesa Lipumba alisema kutokana na tukio hilo wameamua kutangaza rasmi kutokuwa na imani tena na NEC pamoja na sekretarieti yake katika kusimamia shughuli za uchaguzi nchini.

“CUF hatuna imani kabisa na tume ya uchaguzi ya taifa na sekretarieti yake. Tunaamini kwamba kazi kubwa ya NEC ni kuhakikisha kuwa CCM inapata ushindi wa tsunami,” alisema Profesa Lipumba.

“NEC na Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC)) lao ni moja. Ni wizi mtupu; kuhakikisha ushindi wa tsunami kwa CCM, maana utashangaa kama hivi vitambulisho vya ZEC vimefikaje NEC, kama si kuandaa mazingira ya wizi kwa ajili ya kuiandalia ushindi CCM.”

Alisema kutokana na hali hiyo, Jaji Makame hana tena sababu na hadhi ya kuendelea kuongoza taasisi hiyo na anapaswa kujiuzulu mara moja.

“Kama ni muungwana, Jaji Makame kama anastahili kujiuzulu kwa sababu hana sababu na hadhi ya kuendelea kuongoza tume hii, kutokana na madudu haya,” alisema Profesa Lipumba.

Profesa Lipumba pia alilaani nchi wahisani kutoa fedha kwa NEC ili isimamie wizi wa kura na Tanzania iendelee kutawaliwa na serikali aliyoiita ya kifisadi ya CCM, inayoachia mali za asili zikifilisiwa na wajanja.

Alisema vitambulisho hivyo vinatoka katika mikoa mbalimbali nchini, ikiwa ni pamoja na Dar es salaam ambako takwimu zinaonyesha kulikuwa na upungufu mkubwa wa wapigakura katika uchaguzi wa mwaka 2005.

“Wilaya ya Kinondoni, waliopiga kura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 walikuwa asilimia 59.8 kwa Jimbo la Kawe na asilimia 60.3 Kinondoni huku Ubungo kukiwa na asilimia 48.6. Hawa waliopunguwa walienda wapi? Vitambulisho vyao ni hivi vilivyochomwa,” alisitiza Profesa Lipumba.

Kwa muda mrefu vyama vya upinzani vimekuwa vikilalamikia kuwepo mchezo mchafu kwenye mchakato wa uchaguzi, ikiwemo wizi wa shahada za kura ambapo hivi karibuni mbunge Shoka Khamis (CUF), alibanwa bungeni baada ya kushutumu kwamba, CCM inanunua shahada za kura kutoka kwa wananchi. Hatua hiyo ilimfanya Naibu Spika Anne Makinda, kumbana na kumtaka athibitishe tuhuma hizo vinginevyo afute kauli yake, ambapo baadaye aliwasilisha ushahidi wa magazeti yalivyoandika uchaguzi mdogo wa Busanda, lakini Spika Samuel Sitta alikataa akisema baadhi ya vyombo vimekuwa vikiandika habari za uongo na kurusha kombora kisha kuomba ulinzi zaidi kwa Waziri Mkuu.
Tuma maoni kwa Mhariri
 
Ahsante Pr Lipumba kwa kugundua ufisadi huo unaofanywa na NEC.. Maelezo ya Mwenyekiti wa tume ni pumba tupu,yaani mfa maji hawachi kutapatapa,hajui hata anachokiongea.. Kwa nakubaliana na Tamko la Cuf kuwa hawana imani na tume zote mbili za uchaguzi..

NA SASA SISI KAMA WANACHI NA WANA JF NI WAKATI WA KUTOA MAONI YETU KUHUSU NINI KIFANYIKE ILI KUONDOA UCHAFU HUU WA TUME NA THEN TUWAPELEKEE VIONGOZI WA VYAMA VYA UPINZANI ILI WAYAFANYIE KAZI.
 
Wapinzani siku zote wanafanya vizuri katika chaguzi zote kinachowaangusha ni hii tume ya kina Kingunge na genge lake la mafisadi wanachezea matokeo kwa namna wanavyotaka.Wapinzani lazima waungane kupigania tume huru ya uchaguzi kama kweli wanataka kuja kushika dola.

Nani asiyejua mwaka 1995 Maalim Seif alishinda kiti cha urais Zanzibar lakini masultan wakapindua demokrasia kwa kumpatia ushindi Komando,tena nasikia Mwl alihusika sana na hili sakata la kuminya demokrasia nashangaa sana watu wanaangaika kumfanya mtakatifu.
 
Ashukuriwe Mungu Baba yeye atupaye amani.

"Ukweli hauhitaji mabavu kuutetea, ila ni gharama kubwa mno isiyo kifani kujaribu kuuficha uongo"

Nasema hivi, inawezekana hata wewe ulipiga kura na ulikuwa hujui hata kipengele kimoja cha ilani ya uchaguzi ya CCM, au chama kingine chochote. Uongo?

Elimu ya siasa mashuleni ni muhimu sana kwa sasa.

Tunapaswa kujua sheria na utaratibu kamili unaopaswa kufuatwa kabla ya kuharibu ama kuteketeza vitambulisho vya wapiga kura. Watanzania tunahakika gani kuwa vitambulisho hivyo vinastahili kuchomwa?

Uchaguzi uliopita uliomweka JK madarakani kila mtu anajua, Takrima ilitumika, inwezekana ilikuwa haijulikani kuwa ni rushwa, lakini hata hivyo tayari ilifanya lililokusudiwa, japo kwa sasa linatambulika kama RUSHWA.

Ukweli ni kwamba viongozi wengi waliopo madarakani kwa sasa na wengi wao wakiwa chama Tawala CCM wamechafuka kwa kashfa za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka na mali za uma.
Ukiwa una akili timamu na unaitambua vizuri nchi hii, ni wazi kuwa watu hawa hawakuwa na nia njema walipokuwa wakigombea nafasi hizo, au walipokuwa wakipeana nafasi hizo.

Na haitakuwa suala gumu mtu au watu wa aina hiyo kutumia kila liwezekanalo kupata madaraka ama kubembeleza kupewa madaraka au wadhifa. Hivyo basi, kiongozi mlafi na mtesaji wa raia wa Tanzania kwa kuwa mafisadi si ajabu hata kuchaguliwa kwake au kuteuliwa kwake kuwa kwa ujanja ujanja.

Ni vigumu sana kuisafisha nguo inapokuwa mwilini, Ni ngumu na nachelea kusema kuwa haiwezekani CCM kujisafisha ikiwa madarakani. Sheria zetu bado ni dhaifu, mawakili wa serikali na mahakimu uwezo wao kiutendaji unatia mashaka, Mali nyingi za umma zimechotwa ama kutumika kiujanja ujanja tu na hata wanopaswa kuandaa mashitaka na hata kuendesha kesi hizo wamo ndani ya chungu hicho hicho ambacho kimewapa viongozi fursa kufanya ufisadi. Hata sasa kuna kila dalili ya chama kusambaratika, na kukosa umoja na hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi. Wengine wapo ndani ya chama ila walifika ndani bila kujua kuna nini hasa. Kama unadhani ni rahisi CCM kujisafisha ikiwa madarakani, nipatie sababu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA
 
Last edited:
mods tafadhali naomba muunganishe hii ni ile thread ya shahada zachomwa moto, kwani zina maudhui sawa
 
Come on Mkuu Lunyungu...mpe Dr Lamwai credit zake....wakati yeye Serikali inamshughulikia Tundu Lissu alikuwa mpiga kura wa kawaida kama wewe na mimi. Michango ya kina Lamwai et al ina nafasi yake kwenye mageuzi ya siasa zetu...kama leo hatuoni basi pengine huko mbeleni.

Wakati mwingine yule anayenza kuongoza msafara sio yule anayewafikisha wasafiri...lakini ni vema tumpe heshima yake japo kwa kuanza.

Lamwai alipoteza credibility pale alipokubali kununuliwa na CCM, akahama upinzani, akauponda, akazawadiwa ubunge wa kuteuliwa na Mkapa. Baada ya hapo - finished kabiisa!
 
Back
Top Bottom