Jimmie Gatsby
JF-Expert Member
- Mar 7, 2013
- 3,588
- 7,254
upo sahihi kabisaWewe sasa ndio umeongea kitaalamu na kwa uzoefu. Kimsingi 4GR-FSE (Crown na Mark X) ni engine iliokuja ku replace 1JZ japo haiifikii kwa pulling ila imefanyiwa modification isile sana mafuta hata katika uendeshaji wa kawaida tu tofauti na ulaji wa 1JZ engine ilioko kwenye Brevis.
Kinachowaponza wabongo wengi ni poor car maintanance na poor driving skills. Economical driving watu hawazingatii wamekazana kusema gari flani ni 6 cylinder inakula wese. Kuna jinsi ya kuendesha gari sio ukishuka bumps unagandamiza mguu mpaka injini inavuma, taa zikiruhusu unabonyeza wese mpaka gia zikishift gari inastuka. Kwa uendeshaji mmbovu hata IST utaona inakula wese tu hamna namna.
Eco driving: Hakikisha mshale wa RPM hauvuki pale kwenye namba 2 kabla ya gear kuongezeka. Weka mguu taratibu kwenye pedeli ya mafuta hakikisha gari inaenda gear ya pili kiwepesi bila kuvuka zaidi ya namba 2 kwenye mzunguko wa engine. Hapo hata ukitumia V8 utaona haili wese!