Je mastaa wa bongo wanalipa kodi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je mastaa wa bongo wanalipa kodi

Discussion in 'Entertainment' started by Kuntakint, Jun 27, 2012.

 1. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #1
  Jun 27, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,112
  Likes Received: 469
  Trophy Points: 180
  Imekuwa na kawaida ya mastaa wa bongo hasa wa Kitengo chakucheza sinema na wanaopiga muziki (Bongo Flava) kutambiana wao kwa wao kwa pesa. Na kweli tunaona hata matumizi yao au magari, nyumba, Party ni ya mamilioni Je wanachangia pato la serikali. Kwasababu yule mama nitilie, wamachinga ambao wanatembea kilometer karibu 20 kwa siku wanatozwa kodi na hata kunyanganywa bidhaa zao. Sasa inakuwaje kwa hawa mastaa ambao wanamagari ya paund ya Uingereza£30,000.00 sawa na tshs 75,000,000.00. Nitatoa mifano hapa kwa wachache kwa mfano inapotolewa kwenye magazeti na kuonyesha picha inamaana ni kweli na inatakiwa TRA kufuatilia hizi habari kwani magazeti ni sehemu ya taarifa hivyo TRA inatakiwa wafuatilie. Mfano

  1. Diamond Juzi juzi hapa imetolewa ana gari la Tshs 68,000,000.00
  2. Walper gari lenye thamani ya Tshs 75,000,000.00
  3. Wema Kafanya party na kununua nyumba, shooping dubai,gari jumla yake kama Tsh 150,000,000.00
  Jumla Tshs 293,000,000.00

  Ukiangalia kwa haya machache yaani wasanii watatu tu karibu Tshs. 293,000,000.00 ni sawa kuachiwa tu pasipo kuchangia pato la taifa.
  Wakati baba, mama yangu na kaka, dada zangu wenye mtaji wa kuanzia sh. 2000.00 mpaka 10,000.00 wanakamatwa na kutozwa kodi popote pale wanapokuwa na wanamgambo na hata sokoni.

  TRA fuatilieni na hata gari la Wolper doc zinaonyesha gari ni ya 1999 na imelipiwa kodi kwa mwaka huo wakati ilo gari ni la kuanzia mwaka 2009 hadi 2012. Matokeo yake mnawabana watanganyika waliojinyima nje ya nchi akanunua gari lake kwa £500.00 mpaka £1200 mnapandisha mpaka £2500 hadi £3000.00. hamkubaliani na ukweli kwa sababu ya mazoea waliyozoea TRA kudanya kwa kushirikiana na wafanyabiashara na watu binafsi.
   
 2. P

  Paul S.S Verified User

  #2
  Jun 27, 2012
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu you got a point in here..........
  Na bado wakiumwa tunachangishwa mamilioni kuwatibia wakati mama ntilie mwenye mtaji wa sh elf5 analipa kodi au anasombwa na city na akiumwa ni au kudra za mungu au kifo
  Hii ndio Tanzania zaidi ya uijuavyo
   
Loading...