Je Mastaa Bongo Wanalipa Kodi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Mastaa Bongo Wanalipa Kodi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kuntakint, Jun 30, 2012.

 1. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,111
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  Imekuwa na kawaida ya mastaa wa bongo hasa wa Kitengo chakucheza sinema na wanaopiga muziki (Bongo Flava) kutambiana wao kwa wao kwa pesa. Na kweli tunaona hata matumizi yao au magari, nyumba, Party ni ya mamilioni Je wanachangia pato la serikali. Kwasababu yule mama nitilie, wamachinga ambao wanatembea kilometer karibu 20 kwa siku wanatozwa kodi na hata kunyanganywa bidhaa zao. Sasa inakuwaje kwa hawa mastaa ambao wanamagari ya paund ya Uingereza£30,000.00 sawa na tshs 75,000,000.00. Nitatoa mifano hapa kwa wachache kwa mfano inapotolewa kwenye magazeti na kuonyesha picha inamaana ni kweli na inatakiwa TRA kufuatilia hizi habari kwani magazeti ni sehemu ya taarifa hivyo TRA inatakiwa wafuatilie. Mfano

  1. Diamond Juzi juzi hapa imetolewa ana gari la Tshs 68,000,000.00
  2. Wolper gari lenye thamani ya Tshs 75,000,000.00
  3. Wema Kafanya party na kununua nyumba, shooping dubai,gari jumla yake kama Tsh 150,000,000.00
  Jumla Tshs 293,000,000.00

  Ukiangalia kwa haya machache yaani wasanii watatu tu karibu Tshs. 293,000,000.00 ni sawa kuachiwa tu pasipo kuchangia pato la taifa.
  Wakati baba, mama yangu na kaka, dada zangu wenye mtaji wa kuanzia sh. 2000.00 mpaka 10,000.00 wanakamatwa na kutozwa kodi popote pale wanapokuwa na wanamgambo na hata sokoni.

  TRA fuatilieni na hata gari la Wolper doc zinaonyesha gari ni ya 1999 na imelipiwa kodi kwa mwaka huo wakati ilo gari ni la kuanzia mwaka 2009 hadi 2012. Matokeo yake mnawabana watanganyika waliojinyima nje ya nchi akanunua gari lake kwa £500.00 mpaka £1200 mnapandisha mpaka £2500 hadi £3000.00. hamkubaliani na ukweli kwa sababu ya mazoea waliyozoea TRA kudanya kwa kushirikiana na wafanyabiashara na watu binafsi.
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Inakuuma? si system yetu ndivyo inavyofanya kazi? Usiwalaumu mstaa kwa kula maisha kutokana na system yetu; ukiona mbaya, badilisha system yenyewe kwanza. Umeshawahi kuwaliza wabunge kama wanalipa kodi?
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Kwani Wameshakuwa Wanasiasa? Kwanini Hoja yao ijadiliwe kama Wanasiasa? au kuna Sanction?
   
 4. Tutafika

  Tutafika JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2009
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 160
  Magari wanalipa kodi, mfumo wa sasa hauhitaji kujua umelinunu bei gani.

  Tatizo lipo kwenye mapato yao. Hawalipi P.A.Y.E kwa mapato kutoka matamasha mbali mbali. Wengine vipato vyao vinatokana na kazi haramu kama umalaya, watalipaje kodi?
   
 5. m

  majebere JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  wivu mwingine bana.
   
Loading...