Chipsi yaipembeni
Senior Member
- Jan 8, 2015
- 128
- 93
Siku moja nilikuta watu wakibishana kama mapenzi yana hali ya upofu ama hapana. Wale waliokuwa wakiamini mapenzi yana upofu wanasema wanaamini hivyo kwa sababu mtu anayependa hata kama anayempenda ana chongo yeye husema ni makengeza tu.
Waliendelea kusisitiza kuwa ndiyo maana hata mwanamke akiwa na sura mbaya kupindukia, bado atapata mtu atakayempenda. Wale waliokuwa wakiamini mapenzi si upofu walisema kuwa kama yangekuwa ni upofu wapenzi wawili wasingekuwa wanatofautiana, wakabishana na hata kupigana. Wanaume na wake wasingehitilafiana na kuvunja ndoa.
Kwa maelfu na maelfu ya miaka wanamziki na washairi wameimba na kutunga mashairi wakieleza kwamba mapenzi ni mapofu yaani yanapotokea hayaoni. Hata hivyo, wanasayansi wamefanya tafiti nyingi kutaka kuthibitisha kama dhana hii ni sahihi.
Vipimo vya kuchunguza jinsi ubongo wa binadamu unavyofanya kazi vimethibitisha kuwa mtu anapoathiriwa kwa mapenzi kwa kiwango fulani penzi humfanya abadili mwenendo wake wa kawaida. Hali hii ndiyo inayowafanya wengi wafikirie kuwa mapenzi ni mapofu.
Lakini ni kitu gani huwafanya waliokumbwa na mapenzi wawe na uamuzi wa pupa katika suala la mapenzi? Uchunguzi wa kina umebainisha kuwa mapenzi huchochea sehemu ya ubongo inayovutiwa na vitu mbalimbali na kuipumbaza ile sehemu ambayo huwa na uwezo wa kupembua mambo kwa makini.
Mwisho naona nimalizie kwa kusema kuwa watu wawili wataweza kuwa na penzi la kweli, iwapo baada ya kuwa na utashi wa kuwa pamoja, watachukuwa muda wa kutosha wa kujenga moyo wa kupendana bila kuwa na haraka hadi hapo upendo utakapochipuka kati yao na kuwafungamanisha katika mapenzi ya kweli.