JF imejaa vijana wengi wa mwendo kasi hata hilo Azimio la Arusha wanalisikia tu.Afrika kwa ujumla na hususan Tanzania (baada ya Uhuru) Polisi wamekuwa ni watu wa kuogopewa na jamii kama vile nyoka.
Nnakumbuka miaka ya mwanzoni mwa nchi yetu kupata Uhuru Polisi walikuwa ni watu wanaopendwa na jamii, enzi hizo ilikuwa utawakuta polisi wa Kizungu, Kihindi, Kiarabu na Kiafrika.
Kama watoto, kila mmoja wetu alikuwa anatamani siku moja awe askari Polisi. Kilichotupelekea kuwa hivyo ni jinsi enzi hizo polisi walivyokuwa na upole kwa watoto, nnakumbuka wakija mashuleni kutupa mafunzo ya kila aina na kutueleza vipi tuwe raia wema wenye kusaidia wengine. Nnakumbuka pia olisi wakituvusha barabara kwa upole na ingawa magari yalikuwa si mengi.
Nnachokikumbuka zaidi kwa polisi wa siku hizo ni tabasamu zao, awe wa kiume au wa kike (wa kike walikuwa wachache sana), ilikuwa siku zote nikiwaona polisi amma njiani amma wakija mashuleni walikuwa na tabasamu lisilokwisha na wenye nyuso za furaha kiasi cha kukufanya ulie karibu nao uwe na amani.
Hayo yaliisha mara tu baada ya kutangazwa azimio la Arusha.
Baada ya hapo mpaka hii leo, Polisi wamekuwa ni watu wasiocheka na watu, polisi imekuwa ndiyo tishio kwa watoto, mtoto wako akikosa ukimtajia polisi basi anaingiwa na uoga.
Jee, tumejiuliza kwanini? Mimi nnamajibu mengi sana kuhusu hilo lakini nnawachia wachangia mada nanyi mjinafasi na kutoa dukuduku lenu kwa mtazamo wenu.
Paul Makonda, ameweza kuwasema polisi hadharani, tena kinaga ubaga. Mwiko ambao hata wakubwa zaidi ya Makonda kwenye uongozi wameshindwa kuuvunja kwa hapa kwetu Tanzania na nchi nyingi za Kiafrika kwa ujumla. Jee, kwanini?
Binafsi nnaona kitendo cha Makonda ni cha kishujaa sana. Wewe jee?
Nnaomba tuchangie hii mada huku tukielekeza maoni yetu kwa viongozi wa nchi pamoja na viongozi wa majeshi ya polisi kwa nia ya kuitaka polisi iwe rafiki zaidi wa wananchi na iwe ni kwa ajili ya wananchi na si kwa ajili ya viongozi wa nchi au watawala wa nchi pekee.
Lema ana ushujaa gani? Wa "kuota" wakati hajalala??"Ushujaa" nadhani hata Makonda alidhani hivyo..,,anzia kwa Kabwe.....ngoja nikueleze Makonda angekuwa shujaa Kama angesema hayo katika hali gani...
1. Mpinzani wa serikali.
2. Angekuwa Na cheo cha chini kabisa nje ya kamati ya ulinzi Na Usalama.
3. Angekuwa yeye Mwenyewe Ni polisi...
Neno "Shujaa" lingefi"t Sana hapo
Kwa ujumla, Makonda sio "Shujaa" na huwezi kuwa "shujaa" kwa kusema Tu, Na kitafuta umaarufu hewa.....
Ngoja nikwambie baadhi ya mashujaa WA siasa za Bongo baada ya uchaguzi mkuu hadi Leo Nov. 2016.
1.Bashe
2.Lema
3.Lissu
4.NA wengine wengi...
Nakubaliana nawe mkuu mia ya mia. hongera kwa andiko zuri"Ushujaa" nadhani hata Makonda alidhani hivyo..,,anzia kwa Kabwe.....ngoja nikueleze Makonda angekuwa shujaa Kama angesema hayo katika hali gani...
1. Mpinzani wa serikali.
2. Angekuwa Na cheo cha chini kabisa nje ya kamati ya ulinzi Na Usalama.
3. Angekuwa yeye Mwenyewe Ni polisi...
Neno "Shujaa" lingefi"t Sana hapo
Kwa ujumla, Makonda sio "Shujaa" na huwezi kuwa "shujaa" kwa kusema Tu, Na kitafuta umaarufu hewa.....
Ngoja nikwambie baadhi ya mashujaa WA siasa za Bongo baada ya uchaguzi mkuu hadi Leo Nov. 2016.
1.Bashe
2.Lema
3.Lissu
4.NA wengine wengi...
Hapo kwa bibie FF anaweza akawa kamlenga baba wa taifa na azimio la Arusha.JF imejaa vijana wengi wa mwendo kazi hata hilo Azimio la Arusha wanalisikia tu.
Ungewasaidia tu kujua nini kimetokea kuliko kuwapa mtihani wa Harvard Univ.
Amekuandikia kitu roho inapenda eeeh, haya zungusha zungusha!!!Nakubaliana nawe mkuu mia ya mia. hongera kwa andiko zuri
Ufinyu wa akili ni pale unapolalamika kuwa kitu hakiko sawa ila haupendekezi kirelebishwe vipi.CCM ndio chanzo cha yote hayo,wacha wafu wazikane.Kila siku wapinzani wanapiga kelele juu ya reform ya jeshi la polisi mnawaona wapuuzi.Leo Makonda kazungumza kidogo mnakimbilia Jf kumuita shujaa,shame.Hv mmerogwaa au?Hao polisi wameanza pigiwa kelele toka lini?Si ndio mkawapa kiburi cha "kupiga tu"?toeni upuuzi,mnatukumbusha machungu
Tatizo JPM akijaribu kupanga mbowe and co., wanapangua!Heshima yako mkuu.
Kwa sasa ni vigumu sana kwa polisi kuwa rafiki kwa raia kwasababu;
1: Serikali haiwajali kwenye maslahi ya yao(mishahara, nyumba za kuishi, usalama wao na mazingira mazuri ya kazi.). Hiyo imepelekea pokisi kujiingiza kwenye rushwa ili kujikimu ki mahitaji. So uzalendo na urafiki kwa raia haupo tena.
2: Ugumu wa maisha unaopelekea kuongezeka kwa uharifu mfano majambazi,wizi na vikundi viovu mfano panya road. Hupelekea polisi kuto kuwa na imani na upendo kwa raia. Miaka ya nyuma matukio ya kuuawa kwa polisi yalikuwa machache lakini sasahivi hali ni tofauti. Hii inawafanya polisi kuondoa ukaribu na raia kwa sababu raia wenyewe kwa asilimia kubwa ni wahalifu.
MAONI YANGU:
serikali ijali na kutatua kero na matatizo ya polisi kwa kuwapa haki zao za msingi.
Pili, serikali itengeneze ajira kwa wananchi ili kupunguza wimbi la uhalifu unaohatalisha usalama wa nchi.
Sawa kabisa, sasa hivi wanamuangalia kama chui mwenye njaa anapomuangalia ngedere au baboon aliyepo kwenye mti mrefu huku akiomba kwa Mungu ateleze na kuanguka chiniAjira ya Paul Makonda kwa sasa inamlinda... Polisi wanamuangalia tu...
Jeshi la polisi linadumu...
Ajira ya Makonda itakapoisha ndio tutajua kama Makonda kavunja mwiko au polisi wanasubiri muda ufike...
Ajira yake iishe afu aseme hadharani namna ileile kuwa Sirro kapewa Rushwa... hapo ndio tutalijua jeshi la polisi lina uvumilivu.