Jacobus
JF-Expert Member
- Mar 29, 2011
- 4,700
- 1,721
Wakuu, mie ni muumini wa Roman Catholic na nimepakana na kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania ( FPCT) . Tatizo tulilonalo majirani ni kitendo cha kanisa hilo kucheza nyimbo zao kwa sauti kubwa mno si usiku wala mchana. Tumejaribu mara kadhaa mpaka kwa mwenyekiti wa mtaa lakini yaonekana kazi bure na sasa wameamua kutoa music system yao nje na kucheza kama wanarecord hivi. Hawana siku maalum na muda. Wakuu je tunaweza kuchukua hatua gani sasa?