Je, majinni/mapepo ni watu halisi? Kama siyo, inakuwaje .......

BekaNurdin

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
2,267
2,041
Swali: Je, majinni ni watu halisi? Kama siyo, inakuwaje tunapopiga majinni/mapepo kwa maombi (kwa jina la Yesu) madhara huonekana kwa binadamu?

Kisa hiki ni tukio la kweli kabisa!

Mimi nasali kanisa la Tanzania Assemblies of God. Kila usiku wa Ijumaa kuamkia Jumamosi huwa tunafanya mkesha wa maombi kanisani ili kuharibu ufalme wa Ibilisi na mitandao yake yote (wachawi, waganga wa kienyeji, mapepo/majini, nk), kuombea kanisa na nchi na pia kuwaombea wanadamu wote ili wamjue Mungu wa kweli ili waokoke.

Usiku wa Ijumaa tarehe 22/4/2016 wakati tunaomba, binti mmoja alipagawa na mapepo/majini na yakajitambulisha kuwa yanaitwa HABIBA na FATUMA na kwamba yametumwa na BIBI yao kumkomesha huyo binti (15 yrs) eti wamekasirika kwa kuwa ni mlokole na anatangaza habari za Yesu mtaani kwao jambo ambalo hawataki. Pia yakasema yalimwibia sh. 25,000/= alizoweka ili kununua Biblia, yakaiba vitabu vyake (Civics, Biology na Maths) na kwamba wao ndio wanamfelisha kimasomo na kushika nafasi ya 7 badala ya nafasi ya kwanza aliyokuwa anashika hapo mwanzo. Pia juzi ya siku hiyo walitumwa vijana wambake hata hivyo walishindwa kumbaka. Yakasema watatumia njia zozote zile ili auche ulokole. Yakasema pia yatapambana na mchungaji wetu na walimu wa Neno la Mungu hapa kanisani maana ndio wanaomfanya azidi kuwa mlokole. Mimi nafundisha darasa la waongofu wapya!

Ni kweli kabisa binti huyo baada ya kufunguliwa alikiri kuibiwa vitabu hivyo na pesa, akanusurika kubakwa siku iliyosemwa na mapepo na pia hushika nafasi ya 7 darasani.

Huwa tunakemea mapepo kwa kusema hivi: Kwa jina la Yesu tunawavunja mikono, miguu, meno, tunawatoboa macho. Kwa jina la Yesu Kristo, tunanyonga shingo zenu, tunawachoma moto, ungua kwa jina la Yesu!

Kwa jina la Yesu tunachoma na kuteketeza uchawi wenu, tunguli na mikoba yenu, tunatuma moto wa Yesu Kristo tunaunguza makao yenu huko mlikotoka!

Jinni HABIBA alilia sana akasema mnaniua, nakufa jamani. Tukasema kufa na ufe kisha jinni HABIBA akaondoka after 40 minutes, akabaki jinni FATUMA. Tulipokuwa na tunamshughulikia jinni FATUMA akalia akasema jamani mmemuua HABIBA wetu, msiniue na mimi jamani. Tukasema mtoke binti huyu sasa hivi la sivyo tunakuua. Jinni/pepo FATUMA akaondoka. Baada ya dakika moja pepo jingine likapanda likasema mimi ni BIBI, mmewafukuza wajukuu zangu sasa nimekuja mimi mwenyewe. Nawaambia hamuniwezi, nyie ni watoto wadogo sana! Tulianza kumpiga kwa maombi kama tunavyofanya, alipigwa sana hadi akaanza kuomba msamaha akasema anarudisha vitabu, pesa na kumfungua akili zake binti huyo walizofunga. BIBI akaomba asiuawe, kisha akamtoka binti huyo na akawa mzima hata sasa!

Binti aliporudi nyumbani kwao akakuta umati mkubwa wa watu nyumba ya jirani. Alipouliza akaambiwa kuna msiba na aliyefariki ni mdada anaitwa HABIBA na kafariki alfajiri kuamkia siku hiyo. Pia mdada mwingine anayeitwa FATUMA na BIBI yao wamekimbizwa hospitali wako hoi. Fatuma kaungua sana kwa moto, Bibi ameng'oka meno, miguu na mikono haifanyi kazi.

Usiku huo huo nyumba waliyokuwa wanaishi Habiba, Fatuma na bibi yao iliungua moto. Ndugu zao wakawa wanashangaa ulikotokea moto kwani nyumba hiyo haina umeme wala hakuna jiko, mshumaa, koroboi au chemli iliyowashwa usiku huo. Wakawa na mpango kwenda kupiga ramli kwa mganga ili kujua chanzo cha masaibu hayo.

Bibi na Fatuma mpaka sasa bado wako hospitali. Bibi anasema yaliyowapata ni kwa sababu ya Yesu,eti walipeleka uchawi kumdhuru mlokole hapa mtaani kwao ndipo yakawakuta yaliyowakuta. Alipoulizwa ni nani mlokole huyo, hataki kusema!

Binti (mlokole) amepata vitabu vyake, pesa bado.


Swali: Je, majinni ni watu halisi? Kama siyo, inakuwaje tulipopiga majinni/mapepo kwa maombi madhara yakaonekana kwa binadamu?
 
Walokole na wavaa vusuruali vifupi ndio wanaharibu dunia hii..na hasa Africa kusini mwa jangwa la Sahara.
 
Kama ni kweli hili suala limetokea..tuambie ni wapi ili twende tukahakikishe....acheni hizo abrakadabrah zenu bhana.
 
Kama ni kweli hili suala limetokea..tuambie ni wapi ili twende tukahakikishe....acheni hizo abrakadabrah zenu bhana.
Tukihubiri Yesu peke yake ndiye njia na kweli na uzima pasipo yeye huwezi kumwona Mungu wa kweli, mnakataa!
Ndiye mwokozi wa wanadamu na dhambi zao, mnakataa!
Anaweza yote ukimwamini, mnakataa!

Haya bhana, kuamini hakulazimishwi!
 
Kwa jinsi ninavyo faham mimi, jinni/pepo km ulivyo sema ni ROHO... Na wala sio fresh body km tulivyo sisi binadam wa kawaida.... Isipo kuwa jinni ana uwezo mkubwa sn wa kujibadili vyovyote vile atakavyo, anaweza akawa km binadam mwenye jinsi mke/me at a time.. Anaweza akawa mnyama... n.k sasa kwa nn mmepiga hayo mapepo/majinni kisha madhara yakatokea kwa binadam halisi wa hapo mtaani!??? Ipo hv.. Kuna viumbe ving hapa duniani hususani Binadam tunawaona, kupishana nao njian, au kuishi nao ktk jamii yetu lkn si binadam hali, huwa ni maroho kutoka kuzimi au ma-agent from devil's kingdom, huwa inakuwaje utakutata pengne Fatuma na Habiba kuzaliwa kwao hakukuwa kwa kawaida inawezekana ni watoto wa maagano au kuna mimba zingne zikisha tungwa tu bus huwa tunaita zinaibiwa kwa maana kwamba mama mjamzito ana pandikizwa mimba ya kipepo na kulea ujauzito usio halisi had kujifungua kwake. Na kwa kawaida si rahis kwa yeye kufaham kuwa amebeba kiumbe ambacho si halisi/si binadam wa kawaida.... Mtoto huyo atakuwa ktk mazingira haya haya tulio yazoea na kumuona kawaida tu km watoto wengne ijapokuwa wengne huwa wanaanza kuonesha element zao ambazo si za kawaida tangu utotoni... Kumbe hao si binadam wa kawaida ni ma-agent kutoka kuzimu na huwa wana kuja duniani kwa njia tofauti na kwa kazi maalum. Na mambo haya huwa yana fanyika ktk uli mwengu wa roho. Mungu atusaidie sn ktk hili.
 
Yesu anapoitwa anafanya,!! Neno lasema us8ache mchawi aishi!! Okoka upate Raha ya milele
 
Back
Top Bottom