Je, majini na mashetani ni chanzo cha ajali?

Oct 14, 2016
9
45
Wakati tunaelekea kumaliza mwaka 2016 na kuukaribisha mwaka 2017, nimeona ni vyema nikaongelea suala zima la ajali za barabarani hasa katika kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Katika uchunguzi niliofanya tangu nikiwa kijana mdogo mpaka kufikia utu uzima ni wazi kabisa baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha ajali hizi na imani za nguvu za giza kama vile uchawi, majini na mashetani.

Ni ukweli usiopingika kwamba viumbe hawa wamekuwa wakichangia katika matukio ya ajali za barabarani, majini na hata angani na ndio maana kwenye vyombo vya usafiri kabla havijaanza safari wasafiri hupewa muda wa kufanya dua au maombi kwa ajili ya kuvunja nguvu hizo.

Natumaini utaweza kuona kuwa huo ni udhibitisho tosha wa kukuonyesha kuwa mashetani na majini wanahusika kwa namna moja ama nyingine ndio maana kunakuwa na silaha za kujikinga dhidi yao kama hizo nilizotaja hapo juu.

Pia kitu kingine watu wengi wasichofahamu ni aina za majini na namna wanavyofanya mipango yao katika kutekeleza kafara za damu, ikiwa ni moja ya maagano au maagizo wanayokuwa wamepatiwa na wale wanaowaongoza.

Binadamu tumeumbwa kwa udongo lakini majini tunaelezwa hata kwenye vitabu vitakatifu kuwa wameumbwa kwa moto, hapo utaweza kuona utafauti mkubwa uliopo baina yao na sisi.

Ndio maana tukapewa mamlaka ya kumiliki vyote vilivyomo Duniani wakiwemo wao, wapo majini wazuri na wapo majini wabaya, naposema majini wazuri namaanisha wale wanaosaidia watu kwenye masuala ya kipato, maradhi na mambo mengine mengi.

Majini wabaya ni wale wanaotumiwa na watu kwa nia ya kufanya uharibfu, kafara au kudhuru, majini hawa ni hatari sana na usiombe hata kukutana nao katika maisha yako yote.

Kwa leo ningependa niishie hapa ndugu msomaji, tukutane tena siku nyingine kwa rehema zake Allah akijalia.

Kwa wale wanaosumbuliwa na majini, mashetani na maruhani na wanahitaji kusomewa dua, napatika kwa namba 0655 79 33 35

Wabillahi Taufiq
 

Attachments

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom