Je, Maisha yako yanategemea ajira pekee?

WISE 2012

JF-Expert Member
Mar 13, 2012
634
460
.

JE MAISHA YAKO YANATEGEMEA AJIRA PEKEE?

BASI SOMA HAPA.

Kuajiriwa bila kuwa na kitu cha ziada cha kukupa kipato ni sawa na kujenga #gereza kwa mikono yako mwenyewe halafu ukaingia humo ndani ukajifungia halafu ufunguo ukamtupia #mpitanjia usiyemjua anakotoka wala anakokwenda. Eti kisa yeye ni binadamu eti ipo siku atanifungulia nitoke. Akienda moja kwa moja je, si utafia humo gerezani.

Gazeti la #ForbesAfrica toleo la April 2016 limeandika kuwa watu waliofanikiwa kiuchumi wana vipato tofauti tofauti kati ya vitano hadi saba. Wewe una kimoja tu. Think about it.

Plan B inayokupa kipato cha ziada ni muhimu sana kwa mwajiriwa. Hata wafanyabiashara wana vipato vingi. Bakhressa anapata hela kutokana na sehemu ngapi? Lakini fikiria dereva wa boti za Bakhressa.Huenda anategemea kipato kimoja tu yaani malipo kwa kuendesha boti. Halafu jiulize kati ya yeye na Bakhressa nani kasoma kuliko mwenzake. You see?

Usitumike tu kwenye ajira mpaka ujuzi wako na nguvu zako zije kuishia kwa mtu halafu kazini kwako wakishaona hivyo watakufanyia visa visa tu mpaka uache kazi mwenyewe kwa frustration. Halafu badala ukafanye mambo yako ungali na nguvu wewe unatafuta kazi nyingine ya kuajiriwa tena.

Sikia. Jenga maisha yako mwenyewe. Usitegemee hela ya mwisho wa mwezi. Kuna mtaalamu mmoja tajiri na mwanauchumi anasema "KUWA NA HELA NYINGI MWISHO WA MWEZI NI DALILI YA UMASKINI"

Hata kama wewe ni mwanafunzi sasa. Unaonaje ukijifunza kujenga kipato pembeni kuliko kuja kutegemea ajira tu.Think about it.

Angalia matajiri. Hela zao nyingi hazipatikani mwisho wa mwezi. Ni any time. Jifunze sasa. Jenga kitu kingine pembeni part time. Kama umenielewa lakini. Maana kama hujanielewa labda utaelewa baadaye miaka ijayo siwezi jua.

ANGALIZO:
Kuna mambo ya kuzingatia kama utataka kufanya biashara ili kupata kipato cha ziada

1. Usiende kufanya kitu ambacho hakuna mtu mwingine anayekifanya atakayekuwa anakufundisha namna ya kuanza na kufanya nk.

2. Usianze kitu kwa gharama kubwa hususan kwa mara ya kwanza. Ukajikuta unakopa milioni 5, 10, nk ili ukafanye biashara mpya ambayo hata hayupo mtu wa kukuelekeza kwa dhati namna ya kuifanya. Utaishia kupoteza hela za watu na kudaiwa na labda kupata stress. Na kama utakuwa umeajiriwa bado utaathiri hata ajira yako sababu ya stress.

3. Fanya research kuhusu chochote ambacho mtu atakwambia ukafanye. Google. Angalia infirmation kuhusu hicho kitu. Ili ujiridhishe. Usisisimke tu.

4. Kama utaona moyo ni mwako kuwa kuna manufaa basi usijiulize mara mbili. Fanya. Maana ukianza kujiuliza na wakati umeshafanya research yako vizuri ni dalili tu ya moyo wenye woga woga na wasiwasi ambao kwenye biashara itakuwa kikwazo cha mafanikio. Jifunze kuamini utafiti wako mwenyewe.

5. Usiombe ushauri kwa mtu asiyejua hiyo biashara. Mfano umeamua kuuza nguo. Unaenda kuomba ushauri kwa muuza magazeti kuhusu biashara. Yeye biashara yake ni leo kwa leo. Yaani leo kama habari ni Lowassa. Kesho habari ikawa Makongoro Nyerere mambo ya jana siyo dili. Sasa unadhani atakushauri nini?
 
Vizur mkuu, ILA Kuna mambo lukuki yanawafanya watu kutegemea ajira pekee, if it was easy, everybody would do it
Africa Kuna changamoto kubwa Sana kwa Mtu kuwekeza kipato kidogo na kupata faida ya ziada na moja Yao Ni extended family.....
Mada nzur Sana, ina hamasisha kufikiri nje ya box, thanks
 
Leo umekuja kwa hekima, ni kweli....wastaafu wengi wana maisha ya huzuni, I like your Idea

Attachments

  • Ubongo Kids Webisode 11 - Redio ya Desimali.mp4
    3.6 MB · Views: 36
Vizur mkuu, ILA Kuna mambo lukuki yanawafanya watu kutegemea ajira pekee, if it was easy, everybody would do it
Africa Kuna changamoto kubwa Sana kwa Mtu kuwekeza kipato kidogo na kupata faida ya ziada na moja Yao Ni extended family.....
Mada nzur Sana, ina hamasisha kufikiri nje ya box, thanks
Mkuu ukitaka kutoka katika familia zetu yafaa kujitoa akili na kuwa na misimamo. Aliwahi kusema nick wa 2 siri ya utajili ni ubahili sasa ukisema uwe na huruma kwa kila mwanafamilia wallah hutotoka.
 
Mada zenye manufaa kama hizi utakuta zina wasomaji wachache. Lakini za hovyo utakuta zina wasomaji na wachangiaji wengi. Bado tuna safari ndefu sana kufika kwenye kilele cha mafanikio. Mungu tunakuomba uiponye Tanzania yetu.
 
Back
Top Bottom