Je, Lowassa kuziba pengo la Ndesamburo CHADEMA?

Martin George

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,695
1,470
Mzee Ndesamburo alikuwa kama ndiye mfadhili mkuu pale Chadema, na kwa kweli nimekuwa nikilinganisha nafasi yake kama cheo cha KC anachohudumu Zitto Kabwe pale ACT wazalendo.

Ninakumbuka ofisi za mwanzo kabisa kutumiwa na Chadema baada ya kusajiliwa mnamo mwaka 1993 zilikuwa pale kisutu majamatini kwenye ofisi ya mzee Ndesa.

Ndio kusema huyu mzee alijitolea kwa hali na Mali kwa ajili ya Chadema japokuwa hakuwa MTU wa promo sana.

Nikiangalia ile safu ya mabepari wa Chadema sioni mtu wa kubeba mikoba ya Ndesa zaidi ya Lowassa, lakini swali ni je ataweza kuziba pengo?!
 
Back
Top Bottom