Je kwetu Afrika hili linawezwkana kufanyika?

papag

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
1,137
1,609
BBC News, Swahili

Ruka hadi maelezo

Yaliyomo

Habari

Michezo

Video

Vipindi vya Redio

'Kwanini nilifanyiwa upasuaji kupunguza ukubwa kiungo cha uke wangu’

[https://ichef]

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Hakuna 'saizi inayofaa' kwa kiungo hiki cha uke lakini ikiwa unapata usumbufu wowote, tafuta msaada wa matibabu

13 Januari 2023, 17:52 EAT

Imeboreshwa Saa 5 zilizopita

Kuwa na kiungo cha ndani cha uke (Clitoris) kikubwa sio ugonjwa, bali ni hali inayoitwa clitoromegaly. Sababu za hali hii zinaweza kutofautiana, kutoka kwa masuala ya maumbile hadi matatizo ya homoni, kama vile matumizi ya anabolic steroids.

Hivi majuzi, Shule ya Uzazi ya Assis Chateaubriand, kaskazini-mashariki mwa Brazili, ilifanya clitoroplasti mbili - upasuaji wa kurekebisha kisimi.

María*, mmoja wa wagonjwa waliofanyiwa upasuaji, ana umri wa miaka 22 na alizungumza na BBC kuhusu utaratibu wake.

Mwanamke huyo mdogo alisema kwamba alikuwa amelalamika kwa timu ya matibabu kuhusu saizi kiungo hicho chake na amekuwa akitibiwa homoni tangu Desemba 2021.

Kiungo cha uke cha Maria ambacho tayari alichokitaja kuwa kikubwa kiliongezeka ukubwa wakati wa tendo la ndoa kitu ambacho kilimkosesha raha sana.

"Nilipoanza kufanya mapenzi, nikiwa na umri wa miaka 18, niliona kiungo changu kikivimba sana. Na hilo lilikuwa jambo ambalo lilinisumbua sana," alisema.

Kutafuta suluhisho

Kisha msichana huyo aliuliza daktari wa magonjwa ya wanawake ikiwa kuna uwezekano wa kupunguza ukubwa wa kiungo chake.

Maria baadaye aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa maumbile uliosababisha ukuaji usio wa kawaida wa kiungo hiki.

[https://ichef]

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kuna operesheni ya kupunguza ukubwa wa kiungo hiki cha uke(Clitoris)

"Haikunisumbua katika maisha yangu ya kila siku, lakini wakati wa kujamiiana nilikuwa nikiiangalia na kufikiria sio kawaida. Ndio maana nilitaka ipunguzwe," Maria alielezea.

Aliongeza kuwa mwenzi wake wa ngono hakuwahi kuonyesha kutoridhika na hali hiyo, ingawa alimshauri atafute matibabu kwani ilimkosesha furaha.

Hakukuwa na daktari bingwa wa upasuaji huko Ceara, jimbo ambalo Maria aliishi, kwa hivyo ilimbidi kungoja hadi mtaalamu kutoka Sao Paulo alipokubali kusafiri karibu kilomita 3,000 kufanya upasuaji huo. "Operesheni ilienda vizuri sana. Sasa ninahisi kama mwanamke kamili, kwa sababu haikuwa kawaida yangu hapo awali," alisema. "Kwa watu wengi hili ni tatizo dogo tu, lakini kwa wale wanaoishi na hili, ni gumu"

'Sio ugonjwa'

Marcelo Praxedes, daktari wa magonjwa ya wanawake aliyehusika na upasuaji huo, anaonya kwamba kuwa na kiungo hiki kikubwa ni "shida ya kawaida ya ukuaji" na alikiri kwamba inaweza kuathiri kujistahi kwa wanawake. "Lakini kuwa na kiungo kirefu sio ugonjwa," alielezea Praxedes.

[https://ichef]

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Wataalamu wanasema mabadiliko ya ukubwa wakiungo hiki cha uke yanaweza kuathiri kujithamini kwa mwanamke, lakini haipaswi kuonekana kama ugonjwa.

Clitoroplasty ni nini?

Upasuaji wa kupunguza ukubwa wa kiungo hiki cha uke (Clitoris)haulengi utendakazi wake kama chanzo kikuu cha furaha ya ngono ya mwanamke.

Isitoshe, kiungo hiki kina zaidi ya neva 8,000. Sawa na "kitufe kidogo", kiungo hiki hutofautiana kwa ukubwa kutoka kwa mtu hadi mwingine.

Dk Praxedes aliorodhesha baadhi ya sababu zinazosababisha hypertrophy yake, inayojulikana kama clitoromegaly: matatizo ya kijeni au homoni pamoja na matumizi ya anabolic steroids - vitu ambavyo mara nyingi hutafutwa na watu walio tayari kupata misuli haraka.

Ukuaji usio wa kawaida wa kiungo cha uzazi pia unaweza kuchochewa na matumizi ya homoni wakati wa ujauzito, kutokea kwa baadhi ya uvimbe ambao huongeza uzalishaji wa homoni za kiume, na katika hali mbaya zaidi ukuaji usio wa kawaida unaweza kuwa ni matokeo ya ugonjwa wa ovari ya polycystic (PCOS). .

"PCOS inachukuliwa kuwa ugonjwa wa kawaida wa endocrine kwa wanawake wa umri wa uzazi. Maambukizi yake ni kati ya 5% hadi 17% katika kundi hili la umri," Dk Praxedes anasema.

"Inaweza kusababisha ukiukwaji wa hedhi, chunusi, nywele nyingi mwilini, na upanuzi wa kiungo hiki katika hali mbaya zaidi."

[https://ichef]

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kiungo hiki kina miisho ya neva 8,000, ambayo inachangia raha wakati wa tendo la ndoa



Kiungo hiki kawaida huongezeka kwa ukubwa wakati kuna tukio ama shughuli ya kusisimua kwa tishu zinazojaa damu. Hii ni ya kawaida kwa wanawake wote, lakini kwa wale walio na clitoromegaly inasisitizwa zaidi.

Hii inaweza kusababisha ‘ukubwa’ kuliko inavyotarajiwa, ambayo inaweza kusababisha usumbufu wakati wa kujamiiana.

Pia, kulingana na wataalamu, wanawake wengi walio na kiungo hiki kikubwa hawajisikii kuvaa bikini au nguo za kubana sana, kwa sababu saizi ya sehemu zao za siri zinaweza kuvutia umakini.

"Katika upasuaji, tunaondoa kwa usahihi tishu hizo ambazo zimepanuliwa. Lakini tunaziacha sehemu zote nyeti na za mishipa, ambazo ni muhimu zaidi," anaelezea Dk Praxedes.

Je, kiungo hiki kina ukubwa unaofaa?

Hakuna saizi ya kawaida. Kwa hiyo, ni vyema kushauriana na daktari wakati kuna usumbufu unaotambulika wakati wa tendo la ndoa

[https://ichef]

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Kuwa na kiungo hiki kikubwa kunaweza kusababisha maumivu kwa baadhi ya wanawake wakati wa kufanya ngono

"Mgonjwa hapaswi kupima ikiwa kiungo hiki ni kikubwa au la, kwa sababu, kwa kweli, hili ni suala la kibinafsi sana. Na ikiwa ni kikubwa kidogo na akaridhika, hakuna shida," Dk Praxedes anashauri.

Kuna uainishaji katika fasihi ya matibabu inayoitwa Prader, ambayo ni kati ya nambari moja hadi nne na hutumiwa kufafanua kiwango cha upungufu wa viungo vya uzazi lakini tathmini hii inaweza tu kufanywa na mtaalamu.
 
Back
Top Bottom