Je, Kweli wapo watu wanaoamini katika haya?

KALINZI NYUMBANI

JF-Expert Member
Jan 7, 2015
1,776
1,536
Wakuu mpo salama,

Najiuliza sana sipati jibu.

1. Je, kweli wapo watu wanaoamini waganga wa kienyeji katika kutatua matatizo yao na wakafanikiwa?.

2. Je, inakuwaje baadhi ya watu wanadai wanganga wakienyeji wanaweza zuia mvua?.

3. Je, kweli zipo radi za kutumwa kuuwa baadhi ya watu.

4. Je, kweli wapo waganga wa kienyeji wanaweza muona mtu alieoko Dar, hali ya kuwa mganga huyo yupo kijijini ndani ndani kabisa kama Kalinzi?

5. Je, kama wapo waganga wanaweza leta au zuia mvua, kwa nini sijawahi sikia wapo wanaoweza lazimisha jua litoke magharibi na kuzama mashariki?

Wakuu naombeni mnisaidie katiko hayo, na wanafanyaje mpaka wanafanikiwa.

Asanteni.
 
Heeee.? iyo namba 5 mtihani mkubwa. Ila hao waganga zaidi nawaonaga nao wanaganga na njaa zao tu hakunaga ukweli wowote.

Ila uchawi upo.
 
Mkuu, hiyo ya tatu binafsi nilikuwa siamini lakini mwaka 2005 nikiwa nasoma advance lutengano high school tukuyu mkoani mbeya niliamini hilo.

Kuna mzee alikuwa mchawi katika kijiji cha jirani nakikumbuka kile kijiji kinaitwa bugoba sasa wanakijiji wakaamua kwenda ileje kumtafuta mganga ili aje kumtoa uchawi yule mzee yule. Basi mganga akawaahidi atakuja siku fulani. Ikawadia ile siku ya mganga kuja pale kijijini.

Kwa kuwa yule mzee mchawi alijiandaa kukabiliana na yule mganga basi akaiandaa radi kwa ajili ya kumtandika yule mganga ili ashindwe kufika pale kijijini, kumbe yule mganga bwana alijiandaa, basi ilikuwa majira ya nane hivi, tena tukiwa kwenye chumba cha mtihani wa NECTA, yule mzee akaituma radi yake na mganga naye akaituma ya kwake kwa wakati mmoja ili zipambane. Mama yangu nakuhakikishia sijawahi na pengine sitakuja sikia mshindo wa kufanana na ile radi.

Sasa kilichotufanya tuamini ni kwamba hakukuwa na dalili yoyote ya mvua na wala haukuwa msimu wa mvua kama tulivyozoea. Lakini pia baada ya kutoka kwenye pepa katika kuwauliza wazee jirani walituelezea juu ule mkasa wa radi kwamba haikuwa ya kawaida bali ilikuwa ni vita kupitia radi.

Sorry kwa maelezo mengi, ila ni katika kusisitiza nilichowahi kukishuhudia juu ya radi za kutumwa. Na kwa taarifa ilionekana radi ya mganga ilikuwa mshindi na mganga akafika kijijini na kumtoa uchawi yule mzee.
 
UCHAWI UPO.
Haya ni maono ya rohoni, hata Mungu anatambua uwepo wa uchawi na uganga na anauchukia na ameukataza sana. Mchawi anaweza akakuona hata kama ukiwa chini ya maji unaogelea.

-Uchawi unaweza ukaharibu ufahamu wako.
-Uchawi unaweza ukaziba mafanikio yako.
-Uchawi unaweza ukaiba nyota yako.
-.......................

Uchawi upo ila usipende sana kuamini kila kinachotokea ktk maisha yako basi kuna mkono wa Ushirikina, zaidi ya sana usiwe muoga. Ukiwa unajiamini sana inapunguza hata wachawi kukuchezea. Na kiboko ya yote ni Jina La Yesu.
 
Asiye amini uwepo wa uchawi bas haamin uwepo wa MUNGU
 
Back
Top Bottom