Je kweli Kuna viumbe wanaoitwa Alien katika Galaxy/Ulimwengu mwengine?

Bugsy

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
225
304
Habari za Jioni wakuu?

Ki sayansi inasemekana ya kwamba Jua, ni moja wapo ya nyota katika Galaxy universe system..

Hivyo Basi jua/nyota yeyote ina Solar System yaani, kila nyota/jua lina sayari zake mfano dunia hii tunayo ishi sisi binadamu na wanyama tofauti...

Na Kama tunavyo fahamu au kuona usiku angani Kuna nyota nyingi Sana, na kila nyota Ina sayari zake....

Sasa swali langu Ni hivi, je Kuna uwezekano wa kuepo na masayari yenye mandhari Kama yetu katka hayo kila majua/nyota nyengine, Sayari yenye mandhari yenye uwezo wa kussaport life kwa mimea na viumbe wengine ambao hatuwajui eg. Aliens huko kwenye solar system zingine?

By Bugsy the Wise Guy
 
Mars kuna uwezekano ina viumbe wa aina hiyo ama nyingine.
Kisayansi inasemekana Sayari ni kipande Cha jua kilicho chomoka na kupoa kutengeneza crust yaani ardhi, uwezekano wa Sayari kusupport life unategemea na distance kutoka katika jua, yaani Sayari isiwe karibu/mbali Sana kutoka katika jua ili iweze kusupport life mfano mzuri Sayari yetu ni ya tatu kwa umbali kutoka katika jua, kwa umbali wake kutoka katika jua mandhari yake Ni rafiki Sana kusupport uhai wa viumbe hai, Inasemekana kabla ya Sayari ya Mecury kuchomoka katika jua, ambayo ni ya kwanza, Sayari ya Mars ilikua ya tatu takribani Miaka Mabilioni iyopita, hivyo ilikua na uwezo wa kusupport life kwa viumbe... Ndio maana maastrologist wa kimarekani wanajaribu kutafuta uwezekano wa viumbe kuendelea kuishi kule Kama inawezekana, wamegundua structure nyingi za Mars iliwahi kusupport life.. mfano mandhari ya uwepo wa oxygen, japo sio kwa wingi Kama hapa duniani, uwepo wa mabonde inayoashiria kulikua na maji yaani maziwa, mito na bahari
 
Mpaka sasa hamna aliyegundua uwepo wa hawa viumbe, darubini zimeangazwa mbali sana, light years away na hadi sasa bila bila, na siku tutaibukiwa na huyo kiumbe atakua mwenye uwezo mkubwa sana zaidi yetu maana yeyote mwenye uwezo wa kusafiri umbali wote huo na kuja huku kwetu lazima atakua ametuzidi kwa mbali sana kiteknolojia na kisayansi.
Na ndio maana movies za Hollywood huonyesha kiumbe anayetuibukia hutugaragaza sana kabla tuje kumdhibiti.
Wewe fikiria namna hugharimu kufikisha binadamu kwenye mwezi au kupeleka chombo chochote Mars, sasa waza kiumbe mwenye uwezo wa kusafiri umbali wa mwezi kisha uzidishe mara milioni moja......
 
Back
Top Bottom