Je, kweli CHADEMA ni mpango wa Mungu?

Je, kweli CHADEMA ni mpango wa Mungu?

Kwa siku za karibun, Nimekuwa nikifuatilia kwa umakin sana maneno yanayozungumzwa na viongozi wa Chadema kwenye mikutano na kugundua kuwa wamekuwa wakimtaja Mungu mara kwa mara.wanaonekana kutuaminisha kuwa kila wanachofanya wanatumia nguvu za mungu.Mungu hatumiwi kwa namna hiyo.MUNGU ANA MAHALI PAKE PA KUMTAJA TAJA.Itafika wakati mtu akiruhusu kuwa tegemiz sana kwa Mungu hukosa uwezo wa kujituma ktk kufanikisha jambo eti Mungu hajamjalia.Mungu husingiziwa kwa kila dosari au mafanikio.nashauri ktk majukwaa Mungu asitajwe kihivyo na chadema.tuige mfano wa MWALIMU NYERERE alikuwa mhudhuriaji sana ibada lakini ktk majukwaa ya kisiasa hakumtaja Mungu.

Wewe utakuwa umetumwa na askofu leizer aliyeshangilia lema kuvuliwa ubunge
 
Wewe utakuwa umetumwa na askofu leizer aliyeshangilia lema kuvuliwa ubunge

Hilo ndio tatizo letu kubwa humu jamvini badala ya kujibu hoja anakuambia umetumwa sasa sijui na wewe umetumwa na nani.
 
Mungu ni kichaka cha wazembe na wanaotaka ku manipulate wenzao.

Natumaini wewe kama sio kichaa ni punguani, kwani huwezi kusema Mungu ni kichaka cha wazembe. Kumbuka uhai ulionao na mali ulizonazo ni kwasababu ya Mungu uliyemtukana
 
Hilo ndio tatizo letu kubwa humu jamvini badala ya kujibu hoja anakuambia umetumwa sasa sijui na wewe umetumwa na nani.

Nimetumwa na moyo wangu kuitumikia nchi yangu kwa kufichua uovu wote unaotendwa na magamba, waliotuletea maisha magumu. Halafu mpuuzi mmoja anasema wanotaja Mungu ni wazembe
 
Well,mkuu hutakiwi kuwa mlokole kumtaja mungu na hutakiwi kutokuwa mwanasiasa kumtaja mungu.

Mkuu nashukuru kwa kunifahamisha...mkuu kuna vitu vingine ni vya imani kwa upande wako unaweza kuona ni vya kawaida sababu akikuhusu.

Unaposema Mungu wa Yakobo na Mungu wa Yohana ndio Mungu Chadema.

Uoni kama unawagawa wapenzi wa Chadema ambao hawaamini hivyo?

Kwa nini usiseme Mungu wa wote?
 
Mungu ni kichaka cha wazembe na wanaotaka ku manipulate wenzao.
mungu gani unayemzunguzia? kwa mungu wa ukweli uzembe na uvivu ni dhambi kubwa...asiyefanya kazi na asile...nadhani unamzungumzia mungu wa tunguri za nigeria tunaomuona vijiweni kila uchao...!
 
Mkuu nashukuru kwa kunifahamisha...mkuu kuna vitu vingine ni vya imani kwa upande wako unaweza kuona ni vya kawaida sababu akikuhusu.

Unaposema Mungu wa Yakobo na Mungu wa Yohana ndio Mungu Chadema.

Uoni kama unawagawa wapenzi wa Chadema ambao hawaamini hivyo?

Kwa nini usiseme Mungu wa wote?
Ni kweli kabisa mkuu unavosema, kwenye public mungu hana surname wala initial, so kama wanamtaja kiivo ilihali kuna watu wa dini mbalimbali basi laweza kuwa kosa.
 
Kama kumtaja Mungu ni kosa mbona hamhoji kwa nini wimbo wa taifa unasema Mungu ibariki Tanzania..? Hata speech za raisi huwa anasema Mungu ibariki tanzania..
 
Magamba yana mapepo hivyo kila CDM wanapotaja Mungu wanaweweseka na kuanguka so kwao ni habari mbaya sana.
 
Huu ni mwanzo mwema kwa CDM jibu la dhuruma ni Mungu; ikulu, mahakama, polisi, usalama wa taifa, takukuru na serkali yote ya magamba hawatendi haki sasa ndo maana wanaodhurumiwa wanamwita Mungu awasaidie.

Lakini kwa nini magamba yana roho mbaya ya kikatili? Ni kwa sababu wanamweka Mungu pembeni na wakati wa kampeni toka enzi za awamu ya kwanza wanaenda mlingotini, kwa shehe yahya nk kupigiwa ramli. Kana kwamba hiyo haitoshi sasa wamewapa wachawi ubunge eti akina prof deep water kusudi wawachanje wabunge wa upinzani makalioni??!!! Hii nchi imeongozwa kishetani shetani kwa muda mrefu na matokeo ya laana yake ndoo huu ufisadi uliotukuka na maisha duni kwa raia.

Bi up CDM mabadiliko ya kweli ni pamoja na kuondoa ushetani kwenye siasa na kwa viongozi ili nchi itoke kwenye hii laana ilioletwa na magamba
 
Kabla hatujahoji Mungu atayetajwa na CDM, tujue Mungu:
-wanasali bungeni ni yupi
-tunayeimba kwenye national anthem
-anayetajwa kila mwisho wa hotuba ya rais n.k

Tunajadili jambo lisilotujenga na kutushikamanisha! Sioni tatizo la wafanyacho CDM, maana Mungu anahusika sana na taifa letu
 
kumbe hujajua kwanini cc chadema tunamwomba Mungu,this is becoz chama che2 ni cha kanisa, na ndiyo maana kwenye mikutano ye2 ha2kosi maaskofu wawili wa3.

1. Mtaje askofu anayetembea na Chadema
2. Tuhakikishie kuwa CHADEMA ni chama cha kanisa na CCM siyo chama cha....MAFISADI
3. Tuhakikishie kuwa wewe ni mwana CHADEMA, ikibidi scan kadi yako uiweke humu jamvni.

Mnafki mkubwa weeee....unataka kupotosha umma kwa njaa zako na hizo fedha za KIFISADI ANAZOKUHONGA FISADI MKUU CCM...UFIE MBALI.....GAMBA WEEE TENA USHINDWE KATIKA JINA LA MUNGU ALIYE HAI.....SHINDWA PEPO MCHAFU WEWE.
 
Suala la kumtaja Mungu ni kuonyesha imani kwa unachokitegemea kwamba kina uwezo juu ya vitu vyote kama mtoto mdogo anavyomtegemea baba yake. Kama CHADEMA wanaamini Mungu ndiye baba anayeweza kuwatendea haki na kuwapa wanachohitaji wako sahihi kabisa kumtaja Mungu na ili Mungu ajue hawa watu wanamtegemea yeye na siyo kama CCM wanategemea akina maji marefu na kule mlingotini Bagamoyo. Mtoa mada tumaini lake ni Bagamoyo na ndoo maana anashangaa mbona hawaoni CDM Bagamoyo.
 
Kabla hatujahoji Mungu atayetajwa na CDM, tujue Mungu:
-wanasali bungeni ni yupi
-tunayeimba kwenye national anthem
-anayetajwa kila mwisho wa hotuba ya rais n.k

Tunajadili jambo lisilotujenga na kutushikamanisha! Sioni tatizo la wafanyacho CDM, maana Mungu anahusika sana na taifa letu

Mkuu pokea likes zangu kama mia hivi. Enyi wanafiki naomba mjibu kwanza hiyo hoja hapo juu ili twende sawa. Toeni kwanza maboriti yaliyowajaa ndipo muone vibanzi vya wenzenu enyi wanafiki!

Leo hii Chadema au kundi lingine lolote kumtaja Mungu imekuwa kosa wakati Serikalini na Bungeni wanafanya hayo? Unafiki huu utatufikisha wapi enyi wajameni? Mbona unafiki ndio imekuwa style yetu ya maisha ya kisiasa badala ya kuuona na kuukubali ukweli kama ulivyo? Hila hizi za kipuuzi zinatupeleka wapi?

Mungu ni Mungu wa wote na ana haki ya kutajwa na yeyote katika kazi iliyo njema kwa taifa letu - si Mungu wa Bunge, Serikali, Rais, au mwingine yeyote! Hata Mungu naye mwataka kumhodhi?

Au naye ni miongoni mwa "alama za taifa" ambazo hutumiwa na wakuu tu? Mola apishe mbali hili lisitokee!
Pandeni mkampe rushwa kama mnaweza!
 
Back
Top Bottom