Sazira kwetu
Senior Member
- Aug 23, 2015
- 155
- 104
Salama wana jukwaa?
Juzi nilipokea simu ya shemeji yangu ikiwa na malalamiko juu ya kitendo kibaya anachotaka kukitenda ndugu yangu, kitendo chenyewe ni kuombwa kuzaa nje ya ndoa na Mzazi mwenzie.
Kisa kiko hivi, ndugu yangu huyo ana mke na watoto wawili aliozaa na shemeji yangu huyo aliyenipigia simu ya malalamiko, lkn kabla ya kumuoa shemeji yangu aliwahi kuzaa na mwanamke mwingine ambae anaishi kwao na mwanae huyo.
Mwanae kwa sasa ana miaka 5 na hivyo anataka kupata mwingine na mwanaume wa kuzaa nae ni yule aliyezaa nae mtoto wa kwanza kwa madai ya kwamba hataki kuwaachanisha watoto wake wazazi anataka baba yao awe mmoja japo hataki kulelewa kwa madai ya kuwa ndoa za leo ni migogoro isiyoisha na ndoa nyingi hazina raha na furaha.
Anasema haitaji msaada wa aina yeyote ile ili kumlea mtoto yeye anachohitaji ni kubebeshwa mimba tu mengine yote amwachie yeye maana ana kazi yake nzuri ya kuweza kumlea mwanae maana hata mtoto wa kwanza amemulea bila matumizi ya baba maana wakati huo ndugu yangu hakuwa na kazi.
Sasa mzazi mwenzie alimpigia simu ndugu yangu akimweleza kuhusu ombi lake la kubebeshwa mimba nae kwa kumjibu akamwambia yeye kwa sasa ni mme wa mtu ampigie mke wake amuombe wakikubaliana ndio na yeye ataamua cha kufanya.
Bila hiana mzazi mwenzie na ndugu yangu akamvutia waya shemeji wangu na kuelezea shida yake na shemeji akamulushia mpira mme wake kwa kumwambia hayo hayanihusu hayo ni maelewano kati yake na mzazi mwenzie.
Hata baada ya kuongea nae bado wivu uliendelea kumtafuna na kumtesa na ndipo alipoamua kunipigia simu mimi kujielezea kilichojiri baina yao na kuniambia atahakikisha hatoki ndani kwake kwenda kwa mwanamke mwenzie tena kufanya zinaa.
Akasema atampa mtihani mgumu kama Interview ya kifo ikiwa ni pamoja na kumnyima haki yake ya ndoa mpaka atakapo sema ameahilisha zoezi lake na mpango wake wa kwenda huko.
Dunia ina mambo na wahenga walishasema kuwa uyaone na wala sio magorofa, nimeona wanajukwaa wenzangu niwashilikishe kisa hiki, Je kwa hili kwa wanandoa linawezekana?