Je, kutema mate huondoa harufu mbaya?

Josey j

JF-Expert Member
May 26, 2017
466
902
Wasalam ndugu zangu wa JF natumai mko na afya njema kabisa , na wale ambao hawako vizuri Mwenyezi Mungu awatie Nguvu na awafanyie wepesi mrudi kwenye Afya Imara.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,

Nauliza hivi kuna uhusiano gani kati ya harufu mbaya au vitu vichafu na mate mdomoni

Ni Mechanism gani huwa inafanyika pindi mtu akiona kitu kichafu sana (faeces) au ukipata Harufu mbaya katika mazingira fulani, utajikuta unatema mate tena inaweza isiwe mara moja , unaweza kutema hata zaidi ya mara 3.

Je, kutema mate hupunguza Harufu au huondoa kinyaa juu ya kile ulichokiona?

WAJUVI KARIBUNI MTUJUZE
 
Mi mwenyewe nashangaa,,ingeleta maana zaidi mtu ukisikia harufu mbaya apenge kamasi sababu pua ndiyo imesikia harufu na sio mdomo.

Ngoja wajuvi wengine waje.

#dumesuruali...
 
Wasalam ndugu zangu wa JF natumai mko na afya njema kabisa , na wale ambao hawako vizuri Mwenyezi Mungu awatie Nguvu na awafanyie wepesi mrudi kwenye Afya Imara.

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza,

Nauliza hivi kuna uhusiano gani kati ya harufu mbaya au vitu vichafu na mate mdomoni

Ni Mechanism gani huwa inafanyika pindi mtu akiona kitu kichafu sana (faeces) au ukipata Harufu mbaya katika mazingira fulani, utajikuta unatema mate tena inaweza isiwe mara moja , unaweza kutema hata zaidi ya mara 3.

Je, kutema mate hupunguza Harufu au huondoa kinyaa juu ya kile ulichokiona?

WAJUVI KARIBUNI MTUJUZE
Ndio,

Hiyo hali ni matokeo ya mfumo wa mwili baada ya pua kunusa harufu.

Inatokeaje katika mfumo wa mwili?

Pale pua linapo nasa harufu husafilisha taarifa haraka kwenda kwenye ubongo kwa kupitia neva zinaitwa olfactory nerves haraka haraka hizi taarifa kutokea kwenye ubongo hunaswa na na neva zinaitwa vagus nerves ambazo hupenyeza taarifa hii kwenye tumbo na matokeo yake kiwango cha tindikali huanza kutolewa ndani ya tumbo (acid influx) sasa kitendo hiki cha tindikali kuanza kupanda tumboni husababisha ubongo kutuma taarifa kwenye tezi za mate mdomoni (salivary gland) kutoa mate kwa wingi ikiwa na tafusiri ya kuja kuzima kiwango au kupunguza kiwango cha tindikali kilicho tolewa tumboni kwani ndani ya mate kuna alikali nyingi (alikal au base) ndio maana mate yanamtoka mtu au ndio maana mtu anatema mate pale anapo nusa harafu
Na huu mfumo kimwili tunahuita
NEGATIVE FEEDBACK MECHANISM.

Na ndio maana baada ya kutema mate na hata bado ukiwa ndani ya eneo hilo la harufu marathani chooni hujikuta unazoeana na hiyo harafu na hii ni kwa sababu baada ya hii negative feedback mechanism kinachofuata kwenye neva zako za pua hukumbwa na kitu kinaitwa ADAPTATION ndio maana hutasikia harufu endapo ukiendelea kuwa eneo la harufu kwa mda.

Sent from my SM-J400F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom