Fanya yafuatayo ili kuondoa tatizo la mdomo kutoa harufu mbaya

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
20210201_142732_0000.png


Safisha kinywa kwa kutumia dawa ya meno na mswaki, kisha sukukutua na maji safi na kutema.

Pata matibabu ya magonjwa ya kinywa- endapo kinywa chako kina maambukizi, utapatiwa dawa za kutibu maambukizi hayo. Kuna wakati utahitaji kusafishwa meno na daktari wako ili kuondoa bakteria kwenye vijishimo vilivyo kwenye mashina ya meno.

Safisha meno yako kila siku hata baada ya kula chakula, endapo unaenda kazini, nenda na mswaki wako kwa ajili ya kuutumia baada ya kula chakula.

Badilisha mswaki wako mara kwa mara unapokuwa umechakaa au kuchanuka chanuka, chagua mswaki laini usioumiza kinywa chako.

Rekebisha mlo wako kwa kuepuka kula vyakula vyenye vitunguu swaumu au vitunguu maji na vyenye sukari kwa wingi ambavyo husababisha kinywa kutoa harufu mbaya.

Sukutua kinywa chako kwa maji safi ya uvuguvugu angalau mara tatu kwa siku, hii husaidia kuondoa mabaki ya chakula kinywani mwako, hii inasaidia sana kupunguza harufu mbaya ya kinywa.

Hakikisha unasafisha ulimi wako wakati unapiga mswaki, ulimi unapaswa kuwa safi, hii ni kwa sababu uchafu unaobaki kwenye ulimi huozeshwa na bakteria wa kinywani na kuleta harufu mbaya ya kinywa.

Safisha vidani vyako au meno ya bandia unayovaa kinywani angalau mara moja kwa siku ili kuondoa kuta za bakteria katika vidani hivyo vya kuvaa kinywani

Hakikisha kinywa chako hakiwi kikavu, kunywa maji safi ya kutosha na siyo kahawa, pombe au vinywaji vingine laini, epuka kuvuta sigara ili kuepuka kinywa kuwa kikavu na kutoa harufu mbaya.

Unaweza kutafuna pia bablishi au kulamba pipi ambazo zitakuongezea uzalishaji wa mate na kufanya kinywa chako kisiwe kikavu na kutoa harufu mbaya.

Onana na daktari wako kwa uchunguzi wa kinywa endapo tatizo lako linaendelea licha ya kufanya mambo hayo.
 
Njia rahisi, rafiki na ya asili ni kutafuna tu vitunguu swaumu.... Baada ya kula vitunguu vyako piga mswaki ili kuondoa mabaki ya chakula na kuyafanya meno yako kuwa meupe
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom