Je, kuna uwezekano wa Papa kuchagua Askofu mwingine Tanzania baada ya Thaddeus Ruwa'ichi kuugua?

Yeye hajastaafu ukadinali,amestaafu uaskofu kama ambavyo Maaskofu wengine wanavyostaafu kwa sasa anaitwa Bishop emeritus.Cardinali ni cheo kule Roma yaani kwenye Roman Curia yeye ni mmoja wa wateule na ni mjumbe wa kule.Ndio maana yeye baada ya kuwa askofu wa dar mwaka 1992 hakuwa kadinali mpaka mwaka 1998.So Ruwaichi sio kadinali wala sio mkuu wa kanisa katoliki tanzania,Mkuu wake ni mwenyekiti wa TEC ambaye ni Bishop Nyaisonga.
Umepotosha hierarchy ya Kanisa Katoliki. Askofu Nyaisonga ni Rais wa Baraza la Maaskofu (Tanzania Episcopal Confetence), ni cheo kina rotate kila miaka mitano kwa kuchaguliwa kwa kura. Mkuu wa Kanisa Katoliki Tanzania kama ilivyo duniani kote ni Baba Mtakatifu ambaye kwa sasa ni Pope Francis. Kila Askofu wa Jimbo anawajibika kwake.
 
Waislam na wakatoliki huwa mnafurahisha sana. Kila mmoja anavutia upande wake kwa uhalali wa dini.
 
Hujathibitisha Mungu yupo.
usijisahaulishe mijadala mingapi tumeiacha hewani kwa ukwepaji wako pale tunapokuja na hoja za kuvunja contradictions mfu....au maoni butu kutoka kwa watu mfano wenu.....ni mijadala mingi mno...na lau tungeiendeleza nakuahidi mwisho wake ungekuwa siku nitakapokufa mimi au wewe.....au kifo pia mpaka ukione ndio utathibitisha kuwa kipo..
 
Nafikiri Mungu yupo,Je wewe unafikiri Mungu hayupo?Je wewe upo?Uthibitisho wa uwepo wa Mungu una msingi wake katika uwepo wetu.Uwepo wetu ni uthibitisho wa uwepo wa Mungu.Kama unaweza kukanusha uwepo wako basi kanusho hilo laweza kukanusha uwepo wa Mungu na kama waweza kuthibitisha uwepo wako basi waweza thibitisha uwepo wa Mungu.Hakuna uwepo wetu nje ya uwepo wa Mungu wala hakuna uwepo wa Mungu nje ya uwepo wetu na na wala kutokuwepo kwetu hakuondoi uwepo wa Mungu wala kutokuwepo kwa Mungu hakuondoi uwepo wetu.Uwepo wa Mungu unathibitishwa na uwepo wetu/wako.Je wewe Upo?Unaweza kuthibitisha uwepo wako?Na katika kutafakari usisahu kwamba Si Mungu anayehitaji uthibitisho wetu kwake bali sisi ndio tunaohitaji uthibitisho wake kwetu.Nakutakia amani ya moyo.
Sijakuuliza kama unafikiri Mungu yupo, nimekutaka uthibitishe Mungu yupo.

Hujaeleza kwa nini uwepo wetu ni lazima unathibitisha uwepo wa Mungu.

Unalazimisha kitu kinaitwa "logical non sequitur".
 
usijisahaulishe mijadala mingapi tumeiacha hewani kwa ukwepaji wako pale tunapokuja na hoja za kuvunja contradictions mfu....au maoni butu kutoka kwa watu mfano wenu.....ni mijadala mingi mno...na lau tungeiendeleza nakuahidi mwisho wake ungekuwa siku nitakapokufa mimi au wewe.....au kifo pia mpaka ukione ndio utathibitisha kuwa kipo..
Hujathibitisha Mungu yupo.
 
Asante kwa ufafanuzi
Kwahiyo cardinal Pengo atakuwa anaingia kwenye Baraza la maamuzi la Rome mpaka umauti wake ukifika?

Itakuaje kama akikosa Nguvu za kusafiri anaweza kupendekeza MTU wa kumrithi?
Makadinali wote wenye umri usiozidi miaka 80 wako eligible kuingia kwenye conclave ambalo ndiyo 'bunge' linalomchagua Pope. Anaweza asihudhurie tu kama ana changamoto ya afya kama ilivyotokea mwaka 2013 wakati Cardinal Emeritus Julius Riyadi wa Jakarta Indonesia aliposhindwa kuhudhuria uchaguzi uliomleta Baba Mtakatifu Francis kwa sababu ya matatizo ya macho.

Kuna aina mbili ya Makadinari;
(1) Makandinari wanaoweza kumchagua Baba Mtakatifu au kuchaguliwa kuwa Baba Mtakatifu (Wanaingia kwenye Conclave)
(2) Na wale wanachaguliwa kwa heshima hawawezi kumchagua au Kuchaguliwa kuwa Baba Mtakatifu (Hawaingia kwenye Conclave)
 
Nami nauliza, cadinali lazima atoke jimbo kuu la Dar es salaam?
Siyo lazima atoke jimbo Kuu la Dar es Salaam. Angalia hata historia ya Cardinal Laurean Rugambwa.
1943 -Upadirisho
1952 - Vicar General
1953- 1960 Askofu Jimbo la Rutabo
1960- 1968 Askofu Mkuu/ Cardinal wa Jimbo Kuu la Bukoba
1968- 1992 Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam
Kwa hiyo siyo lazima Cardinal atoke Dar es Salaam
 
Sijakuuliza kama unafikiri Mungu yupo, nimekutaka uthibitishe Mungu yupo.

Hujaeleza kwa nini uwepo wetu ni lazima unathibitisha uwepo wa Mungu.

Unalazimisha kitu kinaitwa "logical non sequitur".
Kwa hiyo wewe unataka uthibitisho bila fikra wakati unachohoji ni kwa mujibu wa fikra.Je twawezaji jadili hoja bila kufikiri vizuri,wataka uthibitisho utokao nje ya fikra?je kuna chochote kithibitikacho nje ya fikra?"Does anything exist outside the thought system?"
 
Kuna aina mbili ya Makadinari;
(1) Makandinari wanaoweza kumchagua Baba Mtakatifu au kuchaguliwa kuwa Baba Mtakatifu (Wanaingia kwenye Conclave)
(2) Na wale wanachaguliwa kwa heshima hawawezi kumchagua au Kuchaguliwa kuwa Baba Mtakatifu (Hawaingia kwenye Conclave)

Ahsante kwa Maelezo mkuu
Kwahiyo cardinal Pengo anaangukia wapi katika hilo moja au mbili
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom