MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 19,291
- 39,975
Nimeona Istagram Mhe. PM akiagiza kukamatwa kwa kijana aliyechukua hati za mama fulani na mumewe ambao wana kampuni yao binafsi kuchukulia mkopo wa Tsh 600m taslimu. PM kasema kuwa huyo mama na mumewe walikubaliana kijana awasaidie kutafuta mkopo na kumkabidhi hati ila kijana akajiombea yeye mkopo na mbaya zaidi harejeshi.
Ninalaani kitendo cha huyo kijana maana ni utapeli huo. Lakini swali la kujiuliza ni kuwa kijana aliwezaje kupewa 600m na benki bila wenye hati kuthibitishwa na benki ikiwemo kusaini makaratasi benki? Pia swali kwamba huyu mama na mumewe hadi wanaweza kuwa na kampuni na mali isiyohamishika yenye uwezo wa kuchukulia 600m kushindwa kushughulikia mkopo wenyewe nadhanni sio la muhimu sana.
TAKUKURU pigeni kambi kwenye hiyo benki huenda kuna uhuni unafanyika.
View: https://www.instagram.com/reel/DS2oi4ECGea/?igsh=NjNrZHRtc3ZscXJ5