Hebu tuangalie historia inatuambia nini juu ya mtoto wa kike na wakiume. Hebu tutumie Biblia kama reference yetu ktk hili.
Utaona tangia enzi za Adamu na Eva, hadi walivyoondelea mpaka kina Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Tukija mpaka hata kipindi cha Agano jipya, utaona mtoto wa kiume alikuwa anapewa nafasi kubwa katika jamii. Tena walikuwa wanatumia lugha hii watoto wakiume waliitwa WANA na wa kike BINTI. Kwa hiyo utasikia ana wana wawili na binti mmoja.
Akizaliwa mtoto wa kike bila kuwepo wa kiume na ikatokea hata baba akafariki, lazima ifanyike njia azaliwe mwana (kiume) wakumuinulia huyo mwanaume aliyefariki jina.
Mtoto wa kiume ndio mrithi, ndio mwenye kuendeleza ukoo, ndo wa kuhifadhi jina la nyumba husika!!
Na hata Mungu alianza kumuumba Adamu ndo akamuumba Eva!!
Nafikiri dunia iliumbwa hivo,iliumbiwa kumtazama mwanamke kama kiumbe dhaifu na kinachotegemea sana uwepo wa mwanaume!! Na mimi binafsi naona pamoja na yote mwanamke hawezi kuwa sawa na mwanaume hata siku moja!!
Haina maana tusisome au tusifanye kazi hapana, na jamii inatakiwa imsaidie mtoto wa kike ajikomboe kutokana na ujinga, na aweze kusimama kwa miguu yake pale inapobidi. Mwanamke tangia mwanzo ameumbiwa roho ya huruma na upendo na ndio maana sio rahisi mtoto wa kike kuwatupa wazazi wake hata kama hawakumtendea mazuri.
Kwa hiyo sasa watoto wote wana nafasi yao katika familia. Nafasi ya mtoto wa kiume ipo na ya wa kike ipo.Ingawa pia inategemea huyu mtoto atakuwa vipi na tatokea mtu wa aina gani katika ukubwa wake!!!!!
Injili imetulia, Ni mpango wa Mungu, naamini kama Mungu yupo basi hizi vurugu za usawa zitaishia kama ile ishu ya mnara wa Babeli. Lakini kwa vyovyote vile Mungu hakuumba Mwanamme amtese mke wake/wanawake wateswe na wanaume , bali kila mmoja asimame katika nafsi yake na wala kusiwe na ubaguzi.
Kuchachuliwa inategemea na malezi kama hujamfundisho dos and donts atachakachuliwa mapema tu!Mi wacwac wangu kwa mtoto wakike coz ndo wanachakachuliwa mapema.
Wapenzi wa JF, kwa heshima na taadhima ninawasalimu wote.
Nimejikuta ninawaza jinsi mimi kama mtoto wa kike ndani ya familia yetu ambaye nina majukumu ya not only to take care of my own family i.e. mwanangu kipenzi pamoja na familia ya wazazi wangu i.e. wazee na wadogo zangu- by the way mimi ni mzaliwa wa kwanza kwetu).
Nimejikuta nikitingwa na mawazo ya umuhimu wa sisi wazazi wa leo (wote wake kwa waume) kung'ang'ania kutafuta au kupata mtoto wa kiume kwanza (Ingawa hali hii inaanza kidogo kubadilika now days but to many families it is an issue).
Nahisi inakuwa na logic sana iwapo wazazi mna jiwweza na mnabiashara ambazo mna uhakika kuwa mtoto wa kiume tu ndiye atakayeweza kuziendeleza i.e. kwa kuwa yeye huwa haondoki kwenye familia- akioa anaongeza familia na si kupunguza kama mtoto wa kike.
Lakini najiuliza iwapo mzazi/wazazi hawana asset yoyote ambayo wanahisi wanawezakumrithisha mtoto wa kiume kwa manufaa ya familia hapo baadae. Experience imeonyesha kuwa watoto wa kiume huwa wana attachment ndogo sana kwa wazazi wao (especially pale wanapoanza kujijengea familia zao) kuliko watoto wa kike. Watoto wa kike wanatend kujali wazazi zaidi ya wale wa kiume...........
Je kuna umuhimu bado wa kukazania mtoto wa kiume? Yaani je bado kina mama tunastahesabiwa wanawake wa shoka kama tunauzao mkubwa wa watoto wa kiume zaidi ya wa kike?? Je nafasi ya mtoto wa Kike hasa katika kumwendeleza kielimu inastahili kupuuzwa?
Ninajiuliza sipati jibu, ninakuomba msaada ewe kaka, dada, baba na mama, mjomba, shangazi, Babu na bibi yangu......
Aksanteni, karibu tuchangie........
Sasa mwanajami1 siumesha jua nini sababu ya familia kuhitaji mtoto wa kiume. anaongeza hapunguzi na kuhusu swala la kuwa karibu na wazazi hiyo ni maumbile mungu kawapa imani. ninyi mioyo yenu ina huruma. na pia mwanaume anamajukum yakulea familia yake na wazee. wewe umesema una mtoto una mzazi mwenzio ankusaidia kulea hebu jaribu kushekecha hapo utapata jibu zuri. au ndo tayari ile haki inayozungumzwa kilakukicha inawapa mwanya wakuamini kuwa kweli nanyi hamna tofauti na wanaume? kuna maswala ambayo ni necha huwezi kubadili kama ulaya na magharibi wanvyo idanganya dunia huko kwao yamewashinda, nafasi ya kumuendeleza mtoto wakike ni hakiyake aendelezwe kielim bila kubaguliwa na hakizote apewe lakini zina mipaka yake naimani mwanajami1 unajua Africa na Asia ni tofauti maana yangu kusemna kuna mipaka yake kwakuwa sisi tuna tamaduni zatu. huwezi wewe binafsi yako ukawa kama mwanaume mbele ya wazee wako kuna utofauti hapo japo unawalea lakini kuna sehem fulani mwenyewe huwezi kuikeuka mfano huwezi kuwa nje ya nyumbani kwa muda mwingi kila siku. huu ni mfano mmoja lakini mwanaume ni kawaida akisha fikia umri flani nazani naeleweka. ispokuwa kuna familia zinafanya makosa kutowashirikisha wanawake kenye mfumo wa kiuchumi haya ni makosa.
LAKINI NIMAONO YANGU
Tumeona watoto wengi wakike wanachakachuliawa na misela mtu kavaa buti kubwa kupita mguu halafu ni kinyozi wakati demu kwao zipo za ku mwaga na elimu anapewa - matokeo yake mimba tena ya masela hapo ndo huwa na kwazika sana, yaani fimbo inamchanganya kiasi kwamba hasikii la mzazi
Haya mapenzi ya uzao wa kwanza wa mtoto wa kiume hayapo kwa wanaume pekee yao....naamini wanawake wengi wanatamani wapate uzao wa kwanza wa mtoto wa kiume kuliko hata wanaume....
Kwa wanaume (labda) wanatamani wapate mrithi wa jina+miji+tamaduni zao....wapate atakayeendeleza ukoo wao (majina ya wanawake na koo za wazazi wa wanawake hayarithishwi kwa uzao wao)....nadhani hii kwamba uzao ni kwa nia ya matunzo ya baadae sio sahihi sana (au labda ni sio sababu ya kwanza)....
Mtoto wa KIKE hawezi kuendeleza "family tree"!