Swadaktaaaaaaa!
1.Na kazi ya mume ni ipi?
2.Je wanaokaa majuu huko mnafanyaje maana kila mtu anaenda kwenye mihangaiko kwa faida ya familia na hakuna cha hausigeli kwa walio wengi.
3.Je mke akisafiri, ina maana mume hali, haogi, hatandiki kitanda, wala hafanyi usafi chumbani hadi mke arudi?
Haya maswali ni mazuri. Imenikumbusha last week, nilikuwa nasikiliza mahubiri ya Dr Myles Munroe. Nitajaribu kujibu maswali yako kutokana na uelewa wangu wa point zake.
1. Kazi ya mume ni ipi?
Kazi ya mume imebadilika kutokana na jinsi hali ya dunia ilivyobadilika. Ukiangalia historia ya mwanadamu na hata physical appearance ya mwanadamu, mwanaume alikuwa ndo mfanyakazi. Na hichi kilifanya marriage kuwa rahisi. Kila mmoja alitambua role yake, na kuitekeleza ipasavyo. Mwanaume alienda alienda kazini au kuwinda (yaani kutafuta mlo), na mwanamke alibaki nyumbani na kutunza watoto na nyumba. Hii ndo ilikuwa hali ya maisha iliyofuatwa kwa muda mrefu sana.
Lakini vita vya pili vya dunia, vilibadilisha huu mfumo. katika vita vyovyote wanaume ndo walienda kupigana. Lakini kutokana na urefu na kusambaa kwa vita hivi kulisababisha kusombwa kwa wanaume wengi zaidi kwenda vitani na hivyo kuacha viwanda, mashamba, nk bila wafanyakazi. Hali hii iliwabidi wanawake waingie na kuchukua sehemu ya wanaume katika jamii kwa madhumuni ya kuendeleza production.
Tatizo lilianza baada ya vita kuisha. Wanaume kurudi nyumbani wakakuta kazi yao inafanywa na wanawake. Na wanawake pia wakabutuka kuwa na wao pia wanaweza. Basi kwa ufupi, hii ndo ime-distort mfumo mzima, na kusababisha high divorce rates, nk.
Kwa hiyo sasa inabidi wanaume ku-adopt katika huu mfumo mpya, na hivyo kutambua role yao mpya katika marriage. Na kujua hiyo role yao mpya - inabidi tuwaulize nyie - What do you want from your man? Kwa hiyo wewe unatafuta mwanaume, tafuta yule atakayekupa jibu utakalo wewe. Kama ni chai asubuhi kitandani, nk. Sio unatafuta mwanaume alafu ndo unajaribu kumfanya awe kile unachotaka. Sidhani kama inafanya kazi hivyo. Unatakiwa kumpata yule anayefit mahitaji yako.
2. Je wanaokaa majuu huko mnafanyaje maana kila mtu anaenda kwenye mihangaiko kwa faida ya familia na hakuna cha hausigeli kwa walio wengi.
Kwa ufupi, mimi ninavyoona, wanawake wengi huolewa kwa ajili ya kupata watoto. Na wakati mwanamke akiwa na mimba na hata kitoto kichanga, huweza kuchukua muda off kazini kwa ajili ya kumhudumia mtoto. Tatizo linakuja hapo baadae, na ndio ukiangalia stats utaona ndipo palipo na divorce nyingi. Mwanamke anapomaliza maternity yake na kurudi kazini, basi msuko-suko wa maisha unawazidi nguvu wana-ndoa na kusababisha divorce.
Lakini pia kumbuka huku majuu kazi za ndani zimerahisishwa kidogo kwa vitu kama washing machines, dryers, dish-washers, vacuum cleaners - maana nyumba nzima ni carpet hivyo hakuna kupiga deki, rice cooker, frozen foods, nk. Hivyo maisha ya kutunza nyumba sio magumu kama ya bongo. Kutengeneza chai ni kitu cha muda mfupi sana. Vitafunio ni vya kununua. Hivyo maisha yanaenda tu. Na labda ndo maana huku hakuna nyumba ndogo, maana hakuna mtu wa kukuogesha, au sijui hivi na vile. Huku ninachoona zaidi ni one-night stands.
3.
Je mke akisafiri, ina maana mume hali, haogi, hatandiki kitanda, wala hafanyi usafi chumbani hadi mke arudi?
Hivi vinaendelea kama kawaida kutokana na maelezo yangu ya huko juu. Maisha yamekuwa simple sana, kuishi kama bachelor ni rahisi.
Sina uhakika kama nimekujibu swali lako kisahihi, lakini nimeandika kwa mtazamo wangu tu.