Amina Thomas
JF-Expert Member
- Mar 9, 2008
- 272
- 129
Mh! Jamani, sasa wengine wanafanya ionekane kama huyo mume ni mtoto wa 2yrs au mlemavu! Afuliwe, apangiwe nguo, awekewe maji. Mh!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mh! Jamani, sasa wengine wanafanya ionekane kama huyo mume ni mtoto wa 2yrs au mlemavu! Afuliwe, apangiwe nguo, awekewe maji. Mh!
Yessssss ni muhimu kwa mwanamke kumwandalia mme chakula. Inaonyesha mapenzi. House girl ni kwa watoto na nyumba. Wanawake wa kizungu pia wanafanya hio, esp east europe.
Mapenzi ni zaidi ya kufanyiwa hiki na kile maana hiyo ni conditional love. Mfano wengine waume zetu hawapendi mikono yetu iwe migumu na sura ziharibike maana mama ndo pambo la nyumba. Kuepusha hayo wao pia husaidia kufanya kazi, so twafanya kwa kusaidiana na kurahisisha baadhi ya mambo kwa ku mechanise nyumba through various machine pale uwezo unaporuhusu. Mama na baba huwa viongozi kwa nyakati tofauti na wakati mwingine kwa pamoja pale wawapo nyumbani. Housegirl ni part ya watoto wetu ila yeye huwa mkubwa wa watoto maana yu mkubwa ki umri na wote hufanya haya kwa upendo bila one kuwa mtumwa na wengine kuwa mabwana.
Swadaktaaaaaaa!
1.Na kazi ya mume ni ipi?
2.Je wanaokaa majuu huko mnafanyaje maana kila mtu anaenda kwenye mihangaiko kwa faida ya familia na hakuna cha hausigeli kwa walio wengi.
3.Je mke akisafiri, ina maana mume hali, haogi, hatandiki kitanda, wala hafanyi usafi chumbani hadi mke arudi?
Chaku kwani hujui kazi ya mwanamke ni nini?
Chakula kikiwa kitamu unataka mmeo amsifie nani house girl? We utajiskiaje? Nimeshuhudia ndugu yangu akimpa talaka mke wake na housegirl akachukua nafasi ya mywaifu hivi hivi mtoto alikuwa anakaanga jamani.
hahahahaa..ndivyo itavokuwa endapo mai waif anamwachia kila kitu housegirl.....
Chaku kwani hujui kazi ya mwanamke ni nini?
Chakula kikiwa kitamu unataka mmeo amsifie nani house girl? We utajiskiaje? Nimeshuhudia ndugu yangu akimpa talaka mke wake na housegirl akachukua nafasi ya mywaifu hivi hivi mtoto alikuwa anakaanga jamani.
Yessssss ni muhimu kwa mwanamke kumwandalia mme chakula. Inaonyesha mapenzi. House girl ni kwa watoto na nyumba. Wanawake wa kizungu pia wanafanya hio, esp east europe.
Nyumba ni ya mama, siku zote. Mwanamke jiulize hivi mgeni akija kwako akakuta mume kavaa nguo imejikunja kama imetoka mdomoni kwa ng'ombe au nyumba iko hovyo hovyo tu, unadhani nani atachekwa? wewe, mumeo au housegirl? Je ulivyokubali kuolewa hukujua position yako kama mwanamke?
mimi ni mwanamke, am sorry to say this lakini wanawake tumezidi kutake advantage ya hawa ma housegirl. Enzi za wazazi wetu how many divorces have u heard compared to know? Mwanamke fikiria.. when u were young jinsi mama,shangazi,mamdogo, binamu walivyokuwa wanajali waume zao.
kuwa na fulltime job and kuwa fulltime mother hainizuii kutekeleza majukumu yangu ya nyumbani kama mama, its how u plan ur time and ur tasks.At the end of the day hata mume nae anajikuta ana adopt tabia zako, ukirudi home unakuta kaosha vyombo, au kapika n.k.
Dada ukiona hafanyi yeye sio malaika kujua kuwa ungependelea afanye hivyo, kaa nae chini mueleze jinsi unavyojisikia na jinsi ambavyo ungependelea akusaidie. Tatizo letu sometimes we just assume kuwa mwanaume atafanya tu. Communication ndani ya nyumba ni muhimu.
Housegirl wala simhitaji nyumbani kwangu coz kama mwanamke niliyekamilika I can handle tasks zangu kwa msaada wa mume wangu. Wanawake tuache uvivu sometimes,just because huyo housegirl yupo ndio unaona huwezi, je asingekuwepo?
Mumeo hawezi kumsaidia housegirl kutandika kitanda, but kama ni wewe atakuambia "honey shika kule na mimi huku tu tandike shuka".
Ujumbe: hata siku moja wanawake hatuwezi kushindana na wanaume, at the end mwanaume atashinda tu na tena ukimletea kujua utabaki unalia na wanao ndani yeye huyoooo kwa nyumba ndogo tena huko anapata full service na mgongoni anabebwa sembusi kupigiwa pasi?
Usiri wa nyumba aujua mke na mume. Heshima na upendo hujengwa na hao wawili ambao ni mwilli mmoja. Housegirl ni mfanyakazi kama wafanyakazi wengine, anatafuta kipato. Yeye hawezi kuamua tu kufanya hivyo, ni utaratibu ambao hao wawili wanakuwa wameupanga. Lakini tusiwe busy sana hadi tukaja kusabanisha vishawishi ambavyo sii vya lazima. Kila upande utambue wajibu wake-mume, mke na housegirl.
AKATAE MIZIZI YA MITI NA ASISUBIRI MATUNDA YAKE.
Wakuu ebu nisaidieni kuna umuhimu wowote kumwandalia chakule mumeo wakati housegirl/houseboy yupo na analipwa kwa ajili ya kuhakikisha kila kitu kuanzia usafi hadi chakula kinaenda vizuri?
Yes ni muhimu kwa mke kufanya hivyo kwa mumewe labda mke awe amesafiri, anaumwa, hayupo na labda siku fulani kachoka na kumuomba housegirl amsaidie.
Anaweza pia akakusaidia usafi huyo mfanyakazi ila siyo chumbani mnapolala wanandoa, humo ni wewe tu kuwajibika.
Hayo ni kati ya majukumu ya mwanamke kwenye mji wake.